Kwanini wengi wanapenda kujifanya TISS wakati kazi hii ni kada ya ulinzi kundi moja na mgambo?

Kwanini wengi wanapenda kujifanya TISS wakati kazi hii ni kada ya ulinzi kundi moja na mgambo?

Nakataaaaaa
Hakuna TISS ninaye mjua Mimi halafu familia yake haimjui kuwa yeye ni TISS.

Hizo za kutokujulikana kafa nazo Nyerere.

Siku hizi ile tu kapata chance kwenye Bagamoyo basi masela woteee tunajua.

#YNWA
watu lazima wafahamu kwamba kuna usalama ambao ni wakawaida na wale ambao ni undercover.

Hiko kitengo cha undercover kipo majeshi mengi.

Ukienda jeshini unawakutwa intelligence officers hao ni usalama wa jeshi,yaani undercover hauwezi kuwajua hawavai uniform hao ni wakusanyaji taarifa tu.

hata ukija kwa watu wa usalama wenyewe wanacho kitengo cha undercover ambacho usalama hao huwezi kuwajua kamwe wanakuwa watu wa kusaka taarifa,ndio utakuta wauza mkaa,mama ntilie,n.k

Hawa usalama tunaowaona wakiwa kwenye misafara nyuma ya raisi hawa sio wale undercover ni wale wa kawaida tu.

hata ukienda polisi hizo vitengo vipo vya intelinsia,hao ni undercover huwezi wajua,kuna mwaka alikufa mwandishi wa habari wa kike polisi wakadai maiti yao,watu wakapiga kelele sana ikauwaje polisi anakuwa mwandishi je analipwa mishahara miwili ? Habari ndo hiyo.

unaweza kushangaa hawa viongozi wa kisiasa wengine ni undercover wa jeshi fulani au idara fulani.
 
Unadanganya umma mkuu😀😀.

Watu wanakuchora tu unavyoyakuza mambo kimchongomchongo.

Hakuna kazi ambayo lengo lake ni kutisha watu.

Hakuna kazi ambayo lengo lake ionekane ipo juu zaidi ya nyingine.

Kazi zote unazoziona lengo kuu ni ulinzi na maendeleo ya nchi.

Unapoanza kusema kazi fulani sijui iko hivi na vile basi ujue unaenda nje ya malengo ya kazi hiyo.

Hakuna kazi ambayo iko juu yawenzake,jsio polis,sio jeshi,sio usalama wala uhamiaji wala madaktari.

Mnachokifanya hapa ni kujipotosha wenyewe tu na stori za vijiwe ambazo hazina uhalisia wowote.
 
Tiss hata hawana maisha ya ajabu mno. Pia hawaishi kwa kujiachia ,wanachunga midomo yao wanachoongea Mana anaweza akaropoka yasiyotakiwa kuongelewa public. They're just as if they're Living but in reality they're aren't
hujawahi kukutana nao wakilewa wewe....🤣🤣🤣🤣🤣
 
Japo kauzi kanafatiliwa vizuri na wazee

Kunasiku tulikua tunazurula na Toyo mtaani,tukakutana na wajeda walikua na ruti zao za kikaz wapo na misafara ya iveco,gari zote zilitakiwa zipaki pembeni,ilikua raundi abauti Moja ivi kunagari ikajichanganya haikufata mashart ya masoja,masoja wakastopisha safari zao wakashuka ma MP wamechafukwa balaa wakaifata Ile gari na AK-47,kunanini sijui kilioneshwa ndani ya sekunde 5 ma MP waliludi wanalalamika" MAMBO GANI AYA"

Tuliokua tumegandishwa kwenye msafara tulicheka sana,yaani ma MP wamesanda kwa dogo janja wa miaka 25,tulitegemea dogo aibebe crown yake aluke nayo kichura wiki nzima,mbaya zaid ilikua na brigade office.

Tulijiuliza sana uyu dogo ni nani wajeda wamkatae,maana dogo hakuongea chochote alitoka kwenye gari sekunde 2 akalud kwenye gari akapotea,dogo mwenyewe ni bishoo tu,kala kiduku kikali ila wajeda walisanda

Tuliokua pale tukajua dogo ni usalama,sio rahisi wapenda sifa wakuache kirahisi

Mtoa mada unapo wa underrate oa wajomba wakati wajeda wenyewe wanawagwaya nakushangaa sana
Tuwagwaye kwa kazi yao waliyochagua wenyewe
Sisi haituhusu

Ova
 
Kwanini umelishwa upepo kwamba hawaachi/hawaachishwi kazi?

Hakuna kada dunia hii isiyokuwa na haki ya kuacha/kuachishwa kazi kutegemea na kanuni,taratibu na sheria walizojiwekea.

Kama top boss wao anatimuliwa kazi kwa kushindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo vipi kuhusu hao wadogo wadogo wasiokuwa na taarifa zozote nyeti za kuathiri utendaji kazi kiujumla?
Mtu asipo elewa ulivyoelezea hakuna maneno atakaye pewa tena ili aelewe.
Simple logic umetumia lakini kuna watakaokaza fuvu.
 
Sabaya hakua TISS wadau mbona mnafeli kuelewa mambo madogo tu​
baada ya kuwa MKUU wa wilaya TISS ya wilayani kwake ilikuwa chini yake hivyo kama kipindi hiko hakuwa....hivi sasa yumo....mind you kuna baadhi ya nyazifa hapa nchini huwezi kupewa kama wewe sio EAGLES...

Siajabu hata huo uwaziri ndio maana MAWAZIRI waliotoka upinzani wameishia kuwa manaibu waziri...!​
 
Huo ni uongo.

Polisi, Magereza na JWTZ Wana vitengo vyao vya intelligence na ni askari wenzao ambao hawahusiani ja TISS.

Ni sawa tu, na MP (Military Police) wa JWTZ huwezi kusema MP ni police.

Kwanza TISS mafunzo yao ni mepesi na ya kawaida tu, ndio maana wanaitwa Jeshi Usu Kama ilivyo mgambo, polisi, Magereza, Uhamiaji. Wanaojifunza silaha nzito ni JWTZ pekee
Labda ni kwa Tz, lakini kwenye baadhi ya nchi zingine Idara za usalama wa umma/nchi ni Majeshi kamili kabisa ktk nchi yenye mafunzo kamili sawa na majeshi mengine ya ulinzi. Wengine idara hizo wanaziita "Jeshi la Upelelezi na Hujuma."
 
Kwanini umelishwa upepo kwamba hawaachi/hawaachishwi kazi?

Hakuna kada dunia hii isiyokuwa na haki ya kuacha/kuachishwa kazi kutegemea na kanuni,taratibu na sheria walizojiwekea.

Kama top boss wao anatimuliwa kazi kwa kushindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo vipi kuhusu hao wadogo wadogo wasiokuwa na taarifa zozote nyeti za kuathiri utendaji kazi kiujumla?
once the one always the one....utakacho kuwa huru ni kufanya shughuri zako huru ila bado utashiriki kazi za hapa na pale kama informa....

nadanganya bwana​
 
Japo kauzi kanafatiliwa vizuri na wazee

Kunasiku tulikua tunazurula na Toyo mtaani,tukakutana na wajeda walikua na ruti zao za kikaz wapo na misafara ya iveco,gari zote zilitakiwa zipaki pembeni,ilikua raundi abauti Moja ivi kunagari ikajichanganya haikufata mashart ya masoja,masoja wakastopisha safari zao wakashuka ma MP wamechafukwa balaa wakaifata Ile gari na AK-47,kunanini sijui kilioneshwa ndani ya sekunde 5 ma MP waliludi wanalalamika" MAMBO GANI AYA"

Tuliokua tumegandishwa kwenye msafara tulicheka sana,yaani ma MP wamesanda kwa dogo janja wa miaka 25,tulitegemea dogo aibebe crown yake aluke nayo kichura wiki nzima,mbaya zaid ilikua na brigade office.

Tulijiuliza sana uyu dogo ni nani wajeda wamkatae,maana dogo hakuongea chochote alitoka kwenye gari sekunde 2 akalud kwenye gari akapotea,dogo mwenyewe ni bishoo tu,kala kiduku kikali ila wajeda walisanda

Tuliokua pale tukajua dogo ni usalama,sio rahisi wapenda sifa wakuache kirahisi

Mtoa mada unapo wa underrate ao wajomba wakati wajeda wenyewe wanawagwaya nakushangaa sana
Hakuna lolote na wala si chochote! Once a devil always a devil, kwa nini basi mtu ajivunie au kuona ufahari juu ya hilo?
 
Back
Top Bottom