Kwanini wengi wanapenda kujifanya TISS wakati kazi hii ni kada ya ulinzi kundi moja na mgambo?

Kwanini wengi wanapenda kujifanya TISS wakati kazi hii ni kada ya ulinzi kundi moja na mgambo?

hawa tiss ambao hata hutambulika ni wale PSU makumbusho,kwao hata akiunguruma bar wala sio issue kabisa,na sio sehemu ya miiko yao kutambulika ndio maana wanakaa kwenye mageti ya viongozi au nyuma yao.

wana vitengo vingi,ila kile undercover ndio mnaweza mkamuua asiseme yeye ni nani,labda awe chini ya mikono salama kama polisi,au jeshini nk.
Nilikuwa sifahamu kumbe wale majamaa wanaolinda viongozi wote wanafahamika kwa majina na sura, na sheria zao haijali wao kufahamika kwa umma
 
Usalama wa Taifa ni kazi ya kila mmoja wetu, kila mmoja anawajibika kwa usalama wa Taifa letu. Tofauti ni kuwa kuna waliojariwa na wana mafunzo Fulani, wewe fanya kwa lile unaloliweza, Ni kama usafi tu, wapo walioajiriwa kufanya usafi lakini kwa ujumla wake ni jukumu letu sote.
 
Hawana lolote wa kawaida sana tunawajua na tunayaona maisha yao mtaani
 
Dah jamaa anataka kufananisha walinzi wa nchi TISS na Hawa jamaa wanaopola ubwabwa wa mama ntilie na kwenda kuula wao 🤣🤣🤣🤣
 
Peace upon ya'all,

Ebwana ni ajabu sana mtaani ukipita mtu anaesemekana ni TISS hutukuzwa na hata watu wengine wengi hujifanya TISS ili kuonekana maalumu na kutafuta maujiko

Hata hapa jf wengi hujifanya TISS ili kujipatia ujiko ajabu ni kwamba kama ilivyo nesi, daktari, mfamasia, dentist n.k wako katika kada ya afya (health sector) au walimu, wakufunzi wako kada ya elimu (education sector) au kama marubani, airhostess, astronuts n.k wako kada ya aviation ndivyo pia askari magereza, polisi, askari jeshi, mgambo na TISS wote ni kada ya ulinzi.

Kimsingi TISS ni kada ya ulinzi kundi moja, taaluma moja na mgambo wametofautiana juristiction chache ila wana mengi ya pamoja kuliko utofauti. Hata kimaslahi TISS ni wakawaida sana na wamepitwa na kada nyingi tu na hamna maajabu yoyote kwa hawa walinzi.

Kama reporting TISS officer analipwa 1,850,000 (1.8M) mbona ni kamshahara kadogo kuliko hata lecturer wa chuo cha umma achilia mbali daktari mwandamizi au hata tu mkandarasi wa electrical installation wa mradai wa pale Stigler anaelipwa zaidi ya 3M.

Ni ushamba tu wa Watanzania kuona ati walinzi hawa ni watu wa hadhi kubwaaaa, na ujinga huo ndio unawafanya watu kama Sabaya mwaka 2018 - 19 kujifanya TISS huku akisafiri bure, na kupata huduma katika mahotel makubwa bure akiwaonyesha kitambulisho tu.

Kitu ambacho hata angekua kweli ni TISS hakuna upendeleo wa kupata huduma bure hata sio invoice hapana anatakiwa kulipa labda vingvyo iwe argency ya serikali.
All in all status wanayo
 
We vaa tu sutiKaunda nyoa kipara nenda kaunta kunywa WINDOKU ukiwa umesimama kaunta...macho yako yanaangaza angaaza kila kona
Utaona Wabongo wananong'onezana wengine hata kukimbia kaunta.....

MAUJIKO ..teh teh teh....yani kutisha tu watu
Shemeji yangu aliolewa na bro akidhani jamaa ni afisa usalama kumbe jobless hana kitu. Yaani kuja kushtuka tayari harusi tumekula na ana watoto mapacha. Ikabidi tu shem akubaliane na ukweli kuhusu mumewe. Bro ana mwili mkubwa na alikuwa na hizo pigo za kuvaa kaunda suti
 
Shemeji yangu aliolewa na bro akidhani jamaa ni afisa usalama kumbe jobless hana kitu. Yaani kuja kushtuka tayari harusi tumekula na ana watoto mapacha. Ikabidi tu shem akubaliane na ukweli kuhusu mumewe. Bro ana mwili mkubwa na alikuwa na hizo pigo za kuvaa kaunda suti
Hahaha....
 
Sabaya ni TISS kweli Wala siyo kujifanya.

Tatizo kubwa mmejengwa vichwani kwenu TISS ni watu genius na akili kubwa sana na hivyo mtu Kama Sabaya hawezi kuwa na kiuhalisia ndio usalama wenu hao.

Kwa lugha rahisi Sabaya na yule aliyemtolea Nape bastola ni usalama na ni vichwa panzi tu.
yule aliyemtishia nape yupo kule kwa dangote anasubiri kitanzi.. kumbe lilikuwa ni lijambazi!!
 
Deep down kuna kitu kinakusumbua kuhusiana na hii kada. Tafakari utajua ni nini.
Kinachonisumbua ni kuona kwamba yale wanayojihusisha nayo siyo yale ambayo ni matarajio ya wananchi wengi wa nchi ya kulinda usalama wao. Badala ya ku-deal na watu ambao kwa hakika ni hatari kwa usalama na ustawi wa nvhi na wananchi wake, wao wanahangaika ktk kuwashughulikua watu ambao ni raia wema ktk jamii. Mifano hai ipo mingi sana kuhusiana na hoja hii, naamini hata wewe binafsi baadhi yake utakuwa unaifahamu. "Injustice somewhere is the threat to justice everywhere "( by Martin Luther King Jr).
Aidha, uovu haukubaliki mahali popote pale, aidha iwe duniani au mbinguni. Uovu unakubalika na wale wenyewe watenda maovu tu lakini siyo kwa mtu mwingine yoyote yule ambaye ni raia mwema.
Hivi unataka kuniambia watu ambao wamekuwa wakijihusisha na matendo kama haya ya huyu kwenye video hapa chini ndio "wana status nzuri" ktk jamii?? Seriously??
Jaribu kutafakari kidogo tu kwamba, matendo mabaya kama haya ameweza kuyatenda hadharani kabisa mbele ya umati wa watu, Je, hayo matendo ambayo wamekuwa wakiyatenda mafichoni tena kwa Siri kubwa ni mabaya kiasi gani???????
Je, hivi ni kweli kwamba sisi Watanzania tunahitaji taasisi ya Usalama wa taifa inayofanya kazi kwa mtindo wa namna hii??Kweli??

Kuna msemo mtaani kwamba, "Chura anapenda maji, lakini siyo maji ya Moto."
 

Attachments

  • 5117362-148efa178040dfcd6b51b581965e1bf3.mp4
    25.4 MB
Shemeji yangu aliolewa na bro akidhani jamaa ni afisa usalama kumbe jobless hana kitu. Yaani kuja kushtuka tayari harusi tumekula na ana watoto mapacha. Ikabidi tu shem akubaliane na ukweli kuhusu mumewe. Bro ana mwili mkubwa na alikuwa na hizo pigo za kuvaa kaunda suti
Duh

Ova
 
Usalama wa taifa ni Askari wa intelijensia, idara chini ya ofisi ya Rais.

Lakini Askari kanzu ni Polisi wa upelelezi asiyevaa Uniform.
Nilipokuwa mdogo nilikuwa najua Askari kanzu ni Polisi ila huwa anavaa Kanzu 😆😆😆😂😂😂🤣🤣🤣🚬🚬🚬🏃🏾‍♂️🏃🏾‍♂️🏃🏾‍♂️
 
Back
Top Bottom