GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber amekabidhi kiasi cha Tsh Milioni 20 za rambirambi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwenda katika familia ya marehemu Sheikh Muhammad Idd.
Mufti Abubakar Zuber amekabidhi Milioni 20 kwa Mwakilishi wa familia Ustadh Abuu Ally huku Milioni 30 zilizobaki kutolewa kwa awamu na utaratibu uliopangwa ili kutimiza kiasi cha Tsh Milioni 50 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe Dkt. Samia kwa familia hiyo.
Sheikh Muhammad Iddi alizaliwa mwaka 1969 na kufariki dunia Januari 30,2025 katika hospitali ya Mloganzila alipokuwa akipatiwa matibabu huku enzi za uhai wake akihudumu kama Mshauri wa Mufti mambo ya jamii na Imamu mkuu wa msikiti wa Mwinyiamani Buguruni jijini Dar es salaam.
Chanzo: manaratv
Kumbe Tanzania hii hii kuna Watu wa kupewa Mamilioni ya Shilingi kama hivi na Mheshimiwa Rais na wengine hapana?