Kwanini wenye nyumba wanalazimisha wapangaji walipe Kodi kwanzia miezi 6?

Mwezi mmoja atafanyia nayo maendeleo gani? Kuna watu wanalipa ada kwa hiyo kodi sasa ukimpa mwezi mmoja lazima atakwama.

Ukijenga nyumba ya biashara utakuwa unachukua mwezi mmoja mmoja?
 
Mkuu mimi nina kwangu nimejenga,nilichokiandika hapo ni maisha ya marafiki,ndugu na jamaa zangu wanachopitia,na ukiacha hivyo hata mimi nimewahi kuwa mpangaji hivyo yote yapo kama yalivyo!
Screenshot comment yangu uwatumie hao ndugu na jamaa zako, wasikae kizembe. Namna umewawakilisha, pia na ujumbe wangu wafikishie.
 
Kwa sababu mnasumbua sana , wabongo mnasumbua sana
 
Ungekuwa mmiliki wa nyumba au unaendesha hiyo biashara ungeelewa ni kwanini wanachukua kodi ya kuanzia miezi sita na si vinginevyo
 
si wote ni baadhi ya wenye nyumba tu.
Hata na hivyo kama umeridhia sharti hilo kulingana na mkataba huna sababu kulalamika lipa huku ukikaza msuli kujenga yako 🐒
 
K
ila kila mwezi anachukua Kodi bei gani
 
Una uhakika una huo weledi wa kulipa kodi kila mwezi bila longolongo na usumbufu kwa kwenye nyumba za " Nivumilie nimekwama / kuna mchongo nausikilizia" ?
Wapangaji wa bongo ni kero sana , mi Niko kwenye hii sekta na ninaongea kwa uzoefu , ninasimamia real estate properties tano za mzazi lakini usumbufu na kero za wapangaji wa kibongo kama huna roho ngumu aisee
Ngoja niishie hapa
 
Kama hutaki sheria kajenge uishi kwako....
 
Hawaelewi hawa , hii biashara wapangaji ni pasua kichwa nakwambia , wao hawapigii hesabu uharibifu tena mara nyingi wa makusudi kabisa wanaofanya kwenye miundombinu ya nyumba + longolongo za kodi ,kusumbua kwenye malipo .
 
Hawaelewi hawa , hii biashara wapangaji ni pasua kichwa nakwambia , wao hawapigii hesabu uharibifu tena mara nyingi wa makusudi kabisa wanaofanya kwenye miundombinu ya nyumba + longolongo za kodi ,kusumbua kwenye malipo .
Mtu anatoka unatumia kodi yote ya miezi sita kurekebisha ili mtu aingie! Mpangaji anaekaa zaidi ya mwaka anakupumzisha hata vitu vingine anarelebisha mwenyewe.
 
Nakumbuka enzi hizo Zambia,yani Kodi unalipa kwa mwezi mmojammoja,ukitaka kulipa ya miezi mingi mwenye jengo anakataa anadai asijetumia zote akakosa Hela muda mrefu,bongo nyoso
Una weledi wa kulipa hiyo kodi ya mwezi after mwezi bila kuleta longolongo kwa mwenye nyumba ,au unajitoa ufahamu jinsi watz walivyo kero na wasumbufu kwenye malipo ?
 
Ndio ambacho hawaelewi hicho
 
Una weledi wa kulipa hiyo kodi ya mwezi after mwezi bila kuleta longolongo kwa mwenye nyumba ,au unajitoa ufahamu jinsi watz walivyo kero na wasumbufu kwenye malipo ?
Mkuu swala la kutoheshim mkataba ni swala binafsi la mtu sio taifa,maana hata hiyo Kodi ya mwezi mmoja mmoja Bado watu walikuwa wanapenda kinyume,lakini Kuna watu wanalipa hiyo miezi6 bila usumbufu wowote
 
Hapo kwenye madalali umegusa penyewe, wanakeraa balaa
Uzuri sijawahi kukutana na utapeli wao. Mfyuuuuh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…