Kituo cha redio cha EFM na watangazaji wake wameacha taaluma yao na kuleta ushabiki wao na fitina binafsi juu ya clab yetu ya yanga na viongozi wetu Yanga tunapenda kukosolewa lakini Media ya EFM imezidi kutukera, kututusu na kuidhalilisha team yetu.
Assume mwandishi wa habari aliyesoma chuo anaita club ya Young Africans eti Gongo wazi mara Utopolo haipendezi. Waandishi wa EFM wamezusha mengi kukatisha tamaa, kubeza timu yetu jambo ambayo sio jambo zuri.
Leo wanazusha ati mashabaki wa Yanga waliripua fataki na kung'oa viti na wanashiniza Yanga wapewe adhabu, jambo ambalo sio kweli na video zinadhihirisha hivo. Tukumbuke walivoshinikiza Mchezaji wetu Aucho afungiwe.
Na tuhuma nyingine za uongo ati Yanga tunanunua mechi ambao wote ni uongo na ni habari ambazo hawawezi kuthibisha lakini wakiacha doa kwenye team yetu. Nawasihi viongozi wa Yanga piga marufuku habari za timu yetu kuongelewa Efm. Yanga ni timu kubwa na habari zetu zinauza ndo zinawapa umaarufu huku wakiinajisi timu yetu.
Asanteni