Jiulize na hili, yesu alikufa kwa, siku tatu, na tunaambiwa Yesu ni Mungu, swali kwa siku alizokuwa amekufa, na ni alikuwa Mungu wa dunia/ulimwengu? Au, dunia kwa muda huo ilikosa Mungu!
Yesu alikuwepo kabla ya kuumbwa ulimwengu.
Yesu alikuja duniani kwa kutumia mwili wa binadamu kupitia Mariamu.
Yesu hafi, ni ule mwili aliokuja nao ndio uliteswa, ulikufa na ukafufuka na kupaa Mbingu.
Sisi Wakristo tunamwangalia Yesu kiujumla wake na sio yule mtoto wa Mariamu.
Isaya 9:6
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto mwanamume;
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa ajabu,
Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele,
Mfalme wa amani.
Isaya 7:14
Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara.
Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.
Mathayo 1: 23
Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, (maana yake ni) Mungu pamoja nasi.
Yohana 10:17 Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena.
18 Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.
Yaa ladhiina amanu.
Hakuna Binadamu anayeweza kumwua Yesu.
Yesu mwenye uweza wa kuzifufua maiti za binadamu.
Pale alikuwa hafufui bali alikuwa anaumba upya kama alivyo muumba Adam . (maiti imeoza siku nne anaiumba upya na kuipa uhai)
Yesu alikuja dunia katika umbo la mwili. Kama alivyomtembelea Nabii Ibrahimu katika kitabu cha Mwanzo 18:1....
Mwanzo 18:1
Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari.
2 Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi,
3 akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako.
Yohana (Joh) 8:56 Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.
Yohana 8:57
Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu?
Yohana (Joh) 8:58
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.
Kwa akili yenu Amanu, hapo mtauliza.
Hivi alipo mtembelea Nabii Iburahimu kule Mbinguni alimwacha nani ?
Inamaana sisi wa huku Mbagala Mungu hakuwepo huku kwetu ?
Mungu tunayemjua ni Omnipresence, yupo kote wakati wote.
Mbona hamu ulizi, Mungu alipomtokea Nabii Musa kwenye Bonde la Tua akiwa kama kijinga cha moto unaowaka, kama Qurani inavyosema, kule Mbinguni alimwacha nani ?
Mungu yupo pote na muda wote, zile zilizowatokea Musa na Ibrahimu ni dalili tu au ishara, na sio kwamba Mungu yote yupo pale mahali.
Binadamu hawezi kuishi kama atatokewa na utukufu wa Mungu, atakufa, hata jua litakufa na dunia kuyeyuka kabisa.
Maswali yenu ni ya kitoto sana sana.
Na tatizo mnamlinganisha Mungu wa kwenye Biblia na Mungu wa kwenye Qurani.
Yesu hajawahi kuzaliwa wala kufa.
Yesu yupo tangu enzi na enzi na atakuja kuwahukumu walimwengu siku ya mwisho.
Mlicho ona nyinyi ni umbo la mwili, mwili kama ule alio uona Nabii Ibrahimu.
Na mtamuuliza Ibrahimu.
Mungu anakula? inayumnikanaje amchinjie ndama ili kumwandalia chakula ?
Kwani chakula alikitengeneza nani? 🤣🤣🤣🤣
Mungu akiwa katika ishara au dalili ya umbo la mwili wa Binadamu, basi anaweza kufanya mambo yote mema ya Kibinadamu.
Akili zenu zinaishia hapo kwenye uwezo wa kuona kwa macho ya nyama.
Ndio maana maswali yenu yapo kimwili mwili tu.
You are out of holy spiritual reams.
Utawasikia
Inayumnikanaje Mungu ana Mwana ilhali hajaoa mke? (hana mke)
Yaani huwa nacheka hadi najikojolea maji.