Kwanza mwanafunzi asichapwe, pili akipata mimba arudi shuleni, tatu kama ana utovu wa nidhamu pia arudi shuleni. Waoneeni huruma walimu

Waalimu kinawauma nini mtoto mwenye mimba akirudi shule? Kuna sehemu inawawasha? Piganieni maslahi yenu, acheni akili za kikoloni.
 
Usipende kutajiwa ulie zoea school feeding.
kaangalie states za Marekani ngapi zinaruhusu fimbo.
Zitaje tu. Mimi sizijui. Usisahau kutaja na za ulaya. Usisahau na zinazofukuza shule wanafunzi wanaopata uja uzito. Muongo njia yake fupi.

Amandla....
 
Nadhani HURUMA si kwa walimu pekee, ila kwa familia na jamii yote ya watanzania!

Sent from my TECNO LA6 using JamiiForums mobile app
 
Nitajie nchi moja Ulaya au Marekani au Australia au Canada ambako mwanafunzi anachapwa, anapimwa mimba na akipata mimba anafukuzwa shule. Nitajie hata nusu nchi. Hata robo nchi.

Amandla....
Marekani wana pregnat test kwa wanafunzi na canada pia sina hakika Australia huko sijui
Tuwaonee huruma walimu????? Watoto wengi hupewa mimba na walimu
Inawezekana
 
Nitajie nchi moja Ulaya au Marekani au Australia au Canada ambako mwanafunzi anachapwa, anapimwa mimba na akipata mimba anafukuzwa shule. Nitajie hata nusu nchi. Hata robo nchi.

Amandla....
Ngawethu
 
Jiulize ni nchi yako tu yenye walimu?!
Walimu wa nchi zingine wanafanyaje?! Au watoto wa huko kote hawana nidhamu ila wetu tu?!
Mfano: Japan labda…
Unapo onesha ujinga zaid ni pale unapo fananisha mwanafunzi wa nchi za dunia ya kwanza na mwanafunzi wa dunia tatu huko anaye enda shule na kidumu cha maji na ufagio hana hata viatu
 
Niwe muwazi tu kwamimi itakuwa ngumu hata kumnunulia sare itakayo mtosha na Hilo zigo lake la baba nanihii
 
Uko sahihi [emoji817]
 
Kuchapa viboko sio njia sahihi ya kumjenga mtoto, mtoto ajengwi kwa adhabu hata kidogo.. Wale walio kulia kwenye misingi hiyo ndio hao mnawaona madarakani
Kama wewe ni mkristo na unaamini biblia kama kitabu kitakatifu toka kwa mungu basi rejea tena maandiko.

Kuna wakati kiboko lazima kitumike na hiyo ipo kote dumiani nimeishi na wajeruman wanawachapa watoto fimbo pia , hata japani wanaachapa watoto pia wanapo kosea sasa we mwenzangu nakushangaa unapo sema fimbo sio njia ya kumfundisha mtoto

Elewa yapo mzingira yatakulazimu utumie fimbo labda kama mwenzangu hujawahi kuwa na watoto.
 
Marekani wana pregnat test kwa wanafunzi na canada pia sina hakika Australia huko sijui

Inawezekana
Wanawafukuza watoto wakigundulika na mimba? Na ni States zipi zina compulsory pregnancy tests katika public schools?

Amandla...
 
Biblia imeongea kwa picha nyingi sana, na sio kila andiko ni lako na si kila andiko lipo kwa ajiri ya sehemu flani. Neno linabaki kuwa hai
 
Hivi watu wanasema watoto wakipata mimba wasirudi shuleni mlitaka waende wapi? Kuolewa utotoni? Mama ntilie? Mlitaka waishi vipi bila elimu?
Lakini mimba ni watu wawili mbona tunaongea mimba kama tatizo ni watoto wa kike pekee? Je wangapi wamebakwa? Wangapi wametembea na watu wazima?
Hivyo inabidi vitu vyote vizingatiwe
 
Huyo mwache hao ndo wanajidai wazungu lakini usishangae kuna uwezekano ni mgogo wa mpwapwa! Hajui kuwa sio kila anachofanya mzungu ni kitu bora mengine ni matango pori tu! Yaani biblia itaje na wewe uje na digrii yako ya kibongo hapa ujidai umeelimika kuliko Biblia neno la Mungu! Mungu atusamehe sana ndo maana Biblia inasema Hekima ya mwanadamu machoni pa Mungu ni Upumbavu!
 
Biblia imeongea kwa picha nyingi sana, na sio kila andiko ni lako na si kila andiko lipo kwa ajiri ya sehemu flani. Neno linabaki kuwa hai
Wewe hata Biblia husomagi ni mvywa K vanti tu unatusumbua humu! Hujui lugha ya picha ni kukuonesha uhalisia wa vitu! Ukumbuke pia Biblia haisomwi kama gazeti la Mwananchi! Lazima uombe Mungu akupe macho ya kiroho!
 
Zitaje tu. Mimi sizijui. Usisahau kutaja na za ulaya. Usisahau na zinazofukuza shule wanafunzi wanaopata uja uzito. Muongo njia yake fupi.

Amandla....
Kwa hiyo kisa ni ulaya hata wakifanya ujinga tuwafate? Mbona mnaishi maisha ya kijima sana nyie wabongo!? Kwa hiyo huko wakioana wanaume na sie turuhusu waoane kisa wamefanya ulaya? Best sio kila tajiri anaakili ni Mungu tu aliamua kuwapa mali ndo maana mazezeta kama wewe unaaabudu!
 
Marekani wana pregnat test kwa wanafunzi na canada pia sina hakika Australia huko sijui

Inawezekana
Nchi zote mbili ulizozitaja hazina compulsory pregnancy tests kwa sababu itakuwa ni kuingilia faragha ( privacy) ya binti. Kinachofanyika ni kuwa nesi wa shule au mwalimu akihisi kuwa mtoto ni mja mzito na anajua mazingira ya nyumbani kwake ni hatarishi basi nesi anaweza mshauri kupima mimba kama binti atamwambia kuwa amebakwa. Nesi atawajibika kutoa taarifa kwenye mamlaka husika.
Mazingira mengine ni kama binti anacheza michezo hapo shuleni ambayo inaweza kuwa hatarishi kwa mtu mwenye uja uzito na kichanga kilichokuwa tumboni. Hapo tena anawajibika kumshauri binti apime mimba ili kuepuka majanga hapo baadae. Binti akikataa basi anaweza kumsimamisha kuendelea na hiyo michezo mpaka uhakika wa hali yake utakapopatikana. Ila mtoto anaweza kumshtaki mwalimu au nesi au shule kwa kuzuia haki yake ya kushiriki kwenye michezo.
Cha kuzingatia ni kuwa binti hawezi kulazimishwa kupima mimba. Na matokeo ya upimaji huo hayawezi kutolewa kwa mtu mwingine bila ridhaa yake.
Hapa nyumbani binti hana mamlaka yeyote kuhusu upimaji wa mimba. Wanabebwa tu mzobe mzobe ( mara nyingi kwa kustukiza) kwenda kupimwa uja uzito. Na atakayejulikana positive ndio bai bai. Huo ni unyama na ukatili mkubwa kwa mabinti zetu.

Amandla...
 
Wewe hata Biblia husomagi ni mvywa K vanti tu unatusumbua humu! Hujui lugha ya picha ni kukuonesha uhalisia wa vitu! Ukumbuke pia Biblia haisomwi kama gazeti la Mwananchi! Lazima uombe Mungu akupe macho ya kiroho!
Ulie na macho ya rohoni unaona nini ? mfyuuuuu... najua Biblia kuliko wewe mala elfu kama huamini omba ruhusa nikufundishe hapa ndio utajua mie ni mwalimu wako..

Methali 23:13-14 BHN​

Usiache kumrudi mtoto; ukimchapa kiboko hatakufa. Ukimtandika kiboko, utayaokoa maisha yake na kuzimu.

Ukimchapa kiboko kwa akili zako umemeza mjeledi eeh ... kasome vision na lugha mbali mbali ndio utaelewa, sio kila neno ni lako katika biblia
 
Hayo mawazo ya ccm Tukidai katiba mpya mnasema eti MAGAIDI kweli inchi hiii inayajua MAGAIDI?
 
Nitajie nchi moja Ulaya au Marekani au Australia au Canada ambako mwanafunzi anachapwa, anapimwa mimba na akipata mimba anafukuzwa shule. Nitajie hata nusu nchi. Hata robo nchi.

Amandla....
Kaaah mkuuu umetia aibu sana
Kweli kumbe tunafanya haya yote kisa ulaya hawafanyi hivyo mkuuu amka ulipo lala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…