Uoga wako tu. Wewe unadhani kumomonyoka maadili ni watu kujamiana tu? Iwe jamii tofauti au jamii moja. Hauoni dhulma, ubakaji wa watu wazima na watoto, uuaji wa vikongwe, uuaji wa albino, unyang'aji, uvunjaji wa nyumba ( grili zinathibitisha hiyo), ufisadi, ubamizaji wa kutisha wa wake zetu na watoto wetu, rushwa iliyokithiri.
Kutiwa ndani kwa kuonewa, kupigwa na kuwekwa ndani kwa sababu una jog asubuhi au umevaa fulana fulani, kufa kwa sababu huna hela ya kuhonga, kufa kwa sababu hamna dawa hospitali, kufa kwa sababu umeshindwa kufika hospitali, kufa kwa sababu hospitali haina vifaa, baada ya kufa maiti yako kuzuiwa kwa sababu huna pesa, watu kuvunjiwa vibiashara vyao bila compesation na kadhalika na kadhalika. Watu mnatembea na vibameidi na mabinti wa kazi wenye miaka 13 na mnajiona mashujaa!
Wewe unaona tatizo kubwa ni binti kuruhusiwa kuendelea na masomo baada ya kupata mimba kutokana na kubakwa! Au watu wazima wa jinsia moja kujamiana kwa hiari yao? Kitu ambacho kipo miaka yote, hata kabla hao mabeberu kuanza kututembelea. Mnafik mkubwa wewe.
Amandla....