Kwanza mwanafunzi asichapwe, pili akipata mimba arudi shuleni, tatu kama ana utovu wa nidhamu pia arudi shuleni. Waoneeni huruma walimu

Wewe bana,hapa Tz mtoto atakula fimbo hutaki shika bango,mama samia akipita andamana.au anzisha shule yako.walimu wasiache kutumia fimbo

Tz mtoto analelewa kimaadili ya kitanzania.
Wewe piga fimbo kwani umekatzwa, tumeona wanao piga watoto wengine watoto walikuwa sugu na jeuri zaidi. Hayo ni machaguzo yako
 
Nakwambia wewe mjuzi fanya hivo kwako! Lakini kwangu hapana!
 
Kwani wapi nimelazimisha uamini ninacho amini? Alafu kwanza wewe ndio wa kwanza kuni quote
 
Tatizo sio kama unavyotafasiri hapo , tatizo kubwa kwenye issue ya maadili ni pale inapoleta picha akilini mwa watu kuwa zile kamba za maadili sasa zimelegezwa , picha hiyo inafanya kazi na kuleta madhara automatically kwenye maadili yote kwa ujumla, hilo la kwanza
La pili , ni kwamba ukichunguza hao wanaoua albino, wezi, vibaka n.k ni wale walioshindikana hata shuleni wakivuta bangi, je tunataka kundi lote liwe kama hao? Shuleni ndio mahala pekee panaposaidiana na dini kutunza maadili katika vijana wanaokaribia kuacha familia zao na kuingia mtaani, je ndio waandaliwe kwa style kama hizo , wajifunze kuwa huko kwenye jamii ni ovyo tu hakuna morals/ maadili hayazingatiwi? Unategemea nguvu waliyonayo kama itaachwa bila maadili vijana wanaweza kutenda matendo gani kwenye jamii?
" BADO JAMII HAIJAFIKIRI VIZURI JUU YA HILI"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…