May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Nimekuwa napata ukakasi sana kuhusu matumizi ya haya maneno kwani ni dhahiri kuwa Matatizo pia yaweza kuwa yanaanzia hapa.
Kwanza sitaki kuamini ya kwamba hilo eneo ni la/au ni kwa ajili ya Jamii ya Kimasai pekee, na pia siamini kama waishio huko ni hao Wamasai pekee.
Pia kwa kutumia na kusisitiza kunasibisha eneo hili na Wamasai pekee ni kama ndio kunawapa kiburi cha kuamini hayo ni maeneo yao, kana kwamba Mungu aliwakabidhi wao tu...tofauti na ninavyofahamu mimi kwamba ardhi hii ni mali ya kila Mtanzania, na Raisi ndio Msimamizi kwa niaba ya Watanzania wote.
Ndio maana hata Viwanja tukimilikishwa tunapewa muda maalumu wa kumiliki, kwamba mkataba ukiisha Mamlaka kwa niaba ya Wananchi Wenzako wote wanaweza kukwambia hatukuongezei tena muda wa kukaa eneo hili hivyo tafuta sehemu nyingine.
Hali inapaswa kuwa hivyo hivyo kwa kila Mwananchi bila upendeleo wala umaalumu wa Jamii moja kutoka nyingine.
Kama Mndengereko wa Mtwara atatakiwa ahame Kijiji tupitishe bomba la Gesi kwa manufaa ya Wananchi wote wakiwepo wale waishio Kigoma, basi hili laweza kumkuta pia Muha aishiye Kigoma, Mhehe aishiye Iringa, Mmasai aishiye Oldonyosambu n.k.
Na mbona Wamasai hao hao kama tu Jamii nyingine wamekuwa wakihama kutoka eneo moja hadi lingine tangu kale?.. Wangoni walitokea Kusini mwa Afrika, Wa iraq wametokea Kaskazini wa Africa...vipi leo waone ugumu wakiambiwa tunataka muhamie kati kati ya Nchi?.
Sitounga mkono iwapo hili litafanywa kwa manufaa ya Wachache lakini nitaunga mkono kama litafanywa kwa manufaa ya wengi, na kwa bahati mbaya au nzuri mpaka sasa sijaona sababu za kuniridhisha kuwa kinachofanywa ni uonevu na si kwa manufaa ya Uma wote wa Tanzania.
Mimi ni muumini wa mazingira na huwa natamani kuona lililo na nia njema linafanikiwa haswa kama ni kwa manufaa ya mazingira.
Kwa ujinga ambao Binaadamu tumekwishaufanya kwa Mazingira mpaka sasa naamini hata Mungu angetamani sisi Binaadamu wote tuangamie Wabaki Wanyama, Wadudu, Miti ,Milima, Mabonde n.k. isiyolipiza ubaya na ukatili wa sisi Viumbe Mwenzao Binaadamu.