May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
- Thread starter
- #41
Kati ya Wanyama na Binaadamu nani kamkuta Mwenzake?.Kama wewe ni mwanamazingira kweli ungeanza na hao wanyama. Kwamba ikiwa nafasi haitoshi ku-coexist wao na binadamu nani ahame?
Kwamfano vyura wa project ya hydropower Kihansi (kama rare and endegered species) si baadhi yao walihamishiwa USA ili wasitoweke?
Kwahiyo punguzeni wanyama Ngorongoro (kama nao ni rare and endegered species) kutokana na idadi ya binadamu (Wamaasai) kuongezeka; basi hao wanyama waende Mikumi Ruaha au Chato nk.
Vinginevyo kuna jamii ya Watanzania ambayo hawaongezeki? Wanyakyusa Wandamba, Waluguru, nk wakiongezeka mtawahamishia wapi?
"Overriding interest" ya Serikali katika suala la ecosystem ya Ngorongoro lazima iwe uhai na ustawi wa binadamu! Sio wanyama au watalii au mapato ya nchi kama kodi, tozo, nk.
Na je unajua kuwa sababu ya kuwahamisha Vyura ni kwa sababu ya kuharibu Mazingira hivyo yale Mazingira asili ya kuwafanya Vyura waishi yalianza kutoweka?...na nani alisababisha kama sio Binaadamu sisi tusio na vision?.