Kwaresma na Pasaka Special Thread

Ni kweli umekusudia kuandika "...........rosary takatifu ya mama wa FATMA?!"
" Au umekosea kuandika ?!
 
Amina mtumish utafunga naamini maana ushajikabizi mikononi mwa BWANA
Kufunga maana yake nini?! Na mtu anafungaje?!
Maana kuna kufunga milango, kufunga madirisha, kufunga tai, kufunga kamba za viatu, kufunga ndoa nk. Sasa nyinyi wakati wa kwaresma mnafunga nini?!
 
Sisi tunafunga ndugu yangu karbu tuungane kwa mfungo
Kufunga maana yake nini?! Na mtu anafungaje?!
Maana kuna kufunga milango, kufunga madirisha, kufunga tai, kufunga kamba za viatu, kufunga mkanda wa suruali, kufunga ndoa nk. Sasa nyinyi wakati wa kwaresma mnafunga nini?!
 
Yesu alifunga siku 40 usiku na mchana! Nyie hilo andiko linalowaruhusu kula usiku mmelitoa wapi?!
Sisi waislamu ibada zetu zinaendana na maandiko!
Kwahiyo ukisema KULA DAKU NI KUBADILI RATIBA YA KULA !
Ukiona ni hivyo basi ujue huko kubadili ratiba ya kula ni ibada na inampendeza Mungu kwa kuwa katuma mtume aje awafundishe watu kuwa katika mambo ambayo yanampendeza Mungu ni kubadili ratiba ya kula ( kulingana na mtazamo wenu ) katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kwahiyo sisi hatujali watu wajinga wanatuchukuliaje bali tunachojali ni kufuata maelekezo ya Mungu na mtume wake!
SASA NYINYI ANDIKO LA KULA USIKU MMETOA WAPI WAKATI YESU ALIFUNGA USIKU NA MCHANA KWA SIKU 40 ?!
 
Yesu alifunga siku 40 usiku na mchana! Nyie hilo andiko linalowaruhusu kufungua saa 12 jioni mumepata wapi?!
 
Ila kumbuka sisi wakristu hatuna kitu kinachoitwa futar sjui daku


Unapofunga asubuh hadi jioni kile ulichofunga wasaidie wahitaji

Nakutakia kwaresima njema tuwatendee vyema hasa maskini na wagonjwa na wazee
Yesu alifunga siku 40 usiku na mchana!
Kama nyie wakristo kweli fungeni kama alivyofunga kristo mwenyewe !
 

Mlango 58​


Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.
2 Walakini wanitafuta kila siku; hupenda kujua njia zangu; kama vile taifa waliotenda haki, wasioacha sheria ya Mungu wao, hutaka kwangu amri za haki; hufurahi kumkaribia Mungu.
3 Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.
4 Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu.
5 Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na Bwana?
6 Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
7 Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?
8 Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde.
9 Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;
10 na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri.
11 Naye Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.
12 Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejeza njia za kukalia.
 
Tumaini Letu.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Wale masikini ambao miezi yote wanakula ugali na maharage ikifika kwaresma wanakula nini au hawali kabisa ?!
Inategemea kama ataamua kufunga atafunga

Kwaresma si kipindi cha kutajilika na kuanza kula pirau hapana

Ni kipindi cha kujipatanisha na MUNGU haijalishi unakulaga maharage au dagaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…