Amani iwe kwenu watumishi wa MUNGU katika kristo YESU
Tumsifu YESU KRISTO. AMINA
Tumshukuru MWENYEZI MUNGU kwa kila jambo hasa kwa kumtuma mwanae aje atukomboe . AMINA
PASAKA ni nini pasaka ni kuteseka/mateso/ kifo/kufa/na kufufuka kwa YESU KRISTO
PASAKA ilianzia misiri lakini badae wana wa Israel MWENYEZI MUNGU aliwaagiza waadhimishe pasaka kama kumbukumbu la kwamba wao walikuwa watumwa wa mateso huko misiri
Hivyo wakristo kwa sasa huadhimisha pasaka kama kumbukumbu la kwamba TULIKUWA WATUMWA/ WAFUNGWA WA MINYORORO YA SHETANI mpaka pale BWANA wetu YESU KRISTO alipokuja kutukomboa kwa mateso yake makali pale msalani
Je kwaresma ni nini, kwaresma ni ibada ni ibada ambayo husindikizwa na mfungo wa siku 46 kutoa Dominika 6 hivyo siku hubaki 40
Kufunga kwaresma ni kufanya nini, kufunga ni kuyakalibisha mateso ya YESU KRISTO ambaye ni mfufua wa ulimwengu wote
Hivyo wewe uliyefunga unapaswa kuwapikia wengine ambao hawajafunga na kutoa pesa yako iliyopaswa kula ili uwalishe ndugu na watu Baki
Lakin ndugu zangu kufunga bila sala huko ni kushinda NJAA kabisa
Kufunga bila kunuia jambo flani huko nako ni kushinda NJAA kabisa
Lakin pia kwaresma huanza na jumatano ya MAJIVU
MAJIVU ni nini, MAJIVU hutukumbusha kwamba sisi wanadamu ni mavumbi na mavumbini hakika tutarudi
Masomo husika yoel 2:12-18
Injili husika mathayo 6:1-6,16-18
Moderate tafdhari nawaomba uzi huu msiuunganishe maana uzi utakuwa wa milele kwa update za kila siku juu ya neno la MUNGU la kipindi cha kwaresma
Basi nawakaribisha tufunge na tumuombe MUNGU wetu aliye mwema sana
SAYUNI BOY