Kwaresma na Pasaka Special Thread

Ij
Kuna mtu kaniambia hapa kuwa unakunywa maji na unakula kidogo ila usishibe hii ni kweli?
 
Asanten sana jamani

Nimeona vijana wengi wa kiluther kkkt wamepaka majivu
 


IFANYE KWARESMA 2025 KUWA YA TOFAUTI KIROHO

πŸŸͺπŸŸͺ Kwaresma ni kipindi maalum sana kiroho, ni safari ya kwenda nyikani na Bwana Yesu kwa muda siku 40.

πŸŸͺπŸŸͺ Kipokee kipindi hiki kama fursa ya Kiroho kwani ni kipindi cha kufunga, Kusali, Kutubu, na Kufanya matendo ya Huruma kwa wahitaji.

πŸŸͺπŸŸͺ Jiandae kiroho kwa kufanya toba halisi.

πŸŸͺπŸŸͺ Usiingie kwenye mfungo huu maalum ukiwa moyo wako una makwazo ama manung'uniko yeyote achilia kila jambo lililo gumu na ubaki huru.

πŸŸͺπŸŸͺ Weka nia maalum ya mfungo kwa kutenga na kumwambia Mungu akupe msaada hasa changamoto nzito na ngumu ambazo kwa upande wako unaziona huziwezi.

πŸŸͺπŸŸͺ Kama huna changamoto yeyote ya kiafya mfano kama si mjamzito ama husumbuliwi na ugonjwa wowote tafadhari jinyime kwa kutokula chakula.

πŸŸͺπŸŸͺ Usifunge kwa kujionyesha kwa watu kwamba na wewe umefunga, funga kwa kusudi ama nia uliyoikusudia ili Mungu akupe msaada wake.

πŸŸͺπŸŸͺ Kumbuka kipindi hiki hutokea mara moja tuu kwa mwaka hivyo ifanye kama fursa ya kiroho ambayo mara tuu baada ya kumaliza mfungo utavuna na kujiwekea akiba kubwa ya kiroho.

πŸŸͺπŸŸͺ Uwapo kwenye mfungo waombee na watu wengine kwani ukifanya hivyo Mungu atapokea maombi yako haraka na kwa urahisi.

πŸŸͺπŸŸͺ Saidia wahitaji hasa kwenye kipindi hiki cha Kwaresma, watu wote Mungu amewaumba kwa mfano wake hivyo unavyowasaidia tambua kwamba unagusa mboni yake.

πŸŸͺπŸŸͺ Omba kwa imani na Mungu ataisikia sauti yako

πŸŸͺπŸŸͺ Omba kwa kumaanisha na Mungu ataenda kukutendea sawa sawa na mapenzi yake

πŸŸͺπŸŸͺ Safari hii ya siku 40 itakuwa ni historia kwenye maisha yako kwani ukifunga na kuomba kwa imani Mungu ataenda kuruhusu mambo makuu mnoo yatendeke maishani mwako.

πŸŸͺπŸŸͺ Nakutakia Mfungo mwema wa Kwaresma na Mungu akubariki sana πŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…