Kwaresma na Pasaka Special Thread

Kwaresma na Pasaka Special Thread

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2016
Posts
19,976
Reaction score
32,195
Amani iwe kwenu watumishi wa MUNGU katika kristo YESU

Tumsifu YESU KRISTO. AMINA

Tumshukuru MWENYEZI MUNGU kwa kila jambo hasa kwa kumtuma mwanae aje atukomboe . AMINA

PASAKA ni nini pasaka ni kuteseka/mateso/ kifo/kufa/na kufufuka kwa YESU KRISTO

PASAKA ilianzia misiri lakini badae wana wa Israel MWENYEZI MUNGU aliwaagiza waadhimishe pasaka kama kumbukumbu la kwamba wao walikuwa watumwa wa mateso huko misiri

Hivyo wakristo kwa sasa huadhimisha pasaka kama kumbukumbu la kwamba TULIKUWA WATUMWA/ WAFUNGWA WA MINYORORO YA SHETANI mpaka pale BWANA wetu YESU KRISTO alipokuja kutukomboa kwa mateso yake makali pale msalani

Je kwaresma ni nini, kwaresma ni ibada ni ibada ambayo husindikizwa na mfungo wa siku 46 kutoa Dominika 6 hivyo siku hubaki 40

Kufunga kwaresma ni kufanya nini, kufunga ni kuyakalibisha mateso ya YESU KRISTO ambaye ni mfufua wa ulimwengu wote

Hivyo wewe uliyefunga unapaswa kuwapikia wengine ambao hawajafunga na kutoa pesa yako iliyopaswa kula ili uwalishe ndugu na watu Baki

Lakin ndugu zangu kufunga bila sala huko ni kushinda NJAA kabisa
Kufunga bila kunuia jambo flani huko nako ni kushinda NJAA kabisa

Lakin pia kwaresma huanza na jumatano ya MAJIVU

MAJIVU ni nini, MAJIVU hutukumbusha kwamba sisi wanadamu ni mavumbi na mavumbini hakika tutarudi

Masomo husika yoel 2:12-18
Injili husika mathayo 6:1-6,16-18

Moderate tafdhari nawaomba uzi huu msiuunganishe maana uzi utakuwa wa milele kwa update za kila siku juu ya neno la MUNGU la kipindi cha kwaresma

Basi nawakaribisha tufunge na tumuombe MUNGU wetu aliye mwema sana

SAYUNI BOY
 
Ujumbe wa kwaresma nitauweka hapa maaskofu bado hawajautoa

Je kwanini tunasali njia ya msalaba?

Njia ya msalaba ni ibada ya kupita kwenye njia na mateso aliyopita YESU
Hivyo kwa kuwa sisi hatuna uwezo wa kwenda Israel kupita njia ile bas huwa tunatumia huu utaratibu wa kusali njia ya msalaba

Asante sana
 
Back
Top Bottom