Kwasasa nikiambiwa nichague kazi nitachagua kuwa askari wa barabarani (traffic)

Kwasasa nikiambiwa nichague kazi nitachagua kuwa askari wa barabarani (traffic)

Ile kazi naimiss sana kwasasa.

Ni kazi ambayo nikiambiwa nichague basi itakuwa first choice huku kazi za uhasibu na ugavi nikiziweka pembeni.

Nina hamu sana kuongoza magari barabarani.

Nyie mnaomiliki vyombo vya moto mngenipenda sana.
Unapenda kuongoza kipi sasa, magari au vyombo vya moto? Vyombo vya moto kawaida vinakuwa jiikoni kwenye mafiga, au mimi Kiswahili changu kina shida kidogo?
 
Kuna trafiki jana maeneo ya Kimara Korogwe alinifanyia kitu kibaya sana. Sijui tufanyaje tukomeshe rushwa nchini. Alinibambikia kosa halafu aka-force kunikatia risiti wakati kosa amenibambikia tu na alichukua leseni yangu. Kuna kitu kinatakiwa kifanyike TZ kunyoosha baadhi ya mambo. Taasisi kama PCCB zinatakiwa kufanya kazi kwa weledi kukomesha haya mambo. Au lah basi mishahara iongezwe ili watu waishi kwa kipato chao kuliko kumlipa mtu mshahara wa 500,000 halafu kwa week aingize milioni isiyo halali kutoka kwa watu. Inakuwa haina maana kumlipa kidogo huyo mtu

Jana nilichukia sana Mungu anisamehe tu
 
Back
Top Bottom