Sun Zu
JF-Expert Member
- Mar 16, 2022
- 636
- 1,819
Sina chuki na Huyu Bwana Diamond, huwa napenda sana nyimbo zake, ni burudani tosha.
Ni takribani mwezi sasa toka huyu Bwana na bint Zuchu watoe wimbo wao walioupa jina 'Mtasubiri sana'. Ni wimbo mzuri katika muktadha wa burudani.
Ukakasi unakuja katika video ya wimbo huu. Kile kinachoonekana katika sekunde za mwanzo za wimbo huu ni dharau na kejeli kwa ukristo, na zaidi kwa kwaya ya Mt. Kizito Makuburi.
Uongozi wa Kwaya ya Mt. Kizito, Mwenyekiti, chukueni hatua za kisheria dhidi ya hawa watu, hatuwezi kuruhusu wimbo wetu wa YESU NI MWEMA kutumika kuinajisi imani, na katika hili hakuna kumuachia MUNGU. Chukueni hatua, shitakini huyu mtu kwa kutumia maudhui ya wimbo bila ridhaa ya kwaya, shitakini huyu mtu kwa kukashifu imani ya wengine.
Dharau dhidi ya imani nyingine sio mara ya kwanza kufanywa na huyu Bwana. Miaka kadhaa nyuma alishawahi kutoa wimbo kwa jina 'Hallelujah' huku wimbo huo ukisifia mambo ya kiasherati.
Kwa kuwa hawa wawili, Diamond na Zuchu wote ni waislamu, na kwa kuwa misikiti ipo mingi tu, kiliwashinda nini kuigiza Zuchu yupo msikitini anaimba Qaswida na diamond yupo club anampigia Zuchu simu kisha huyu bint anaacha Qaswida na kumfata Diamond waanze kutongozana?
Hizi ni dharau na dhihaka kwa wakristo! Kwamba bint mcha Mungu anathamini zaidi uasherati, anaacha kuimba kwaya anakimbilia uhuni, stupid!
Kumnyamazia kimya sio sahihi, he needs to be taught a lesson, mbona nyimbo zake ni nzuri tu bila kuingiza vikorombwezo vya dharau na dhihaka dhidi ya imani nyingine?
Haya anayoyafanya kwa imani ya kikristo anaweza kuthubutu kuifanyia imani yake islam?
#AchaDharau