Nilijua tu yatakushinda sababu siku zote njia ya muongo ni fupi,sasa hivi ndiyo unajua alichokiuliza mtoa mada, ila wakati tunajadili kuhusu imani hukujua mtoa mada anauliza nini hadi ulipoona umekwama ndiyo unakumbuka mada inasema nini.
Tatizo bado liko palepale, ni kwamba wewe kushindwa kuelewa au kutaka kupotosha neno imani nililotumia kuelezea roho. Kwahiyo huwezi kuniambia sijajibu nilichoulizwa kama itakuwa neno imani halijaeleweka.
Nikikwambia unitajie rangi ya sauti yako halafu wewe ukasema kuwa sauti haina rangi. Je,itakuwa ndiyo hujajibu swali langu? kwa sababu mie nimeuliza rangi ya sauti we unaniambia sauti haina rangi.