Kweli binadamu ana 'roho'? Iko sehemu gani hasa mwilini?

Kweli binadamu ana 'roho'? Iko sehemu gani hasa mwilini?

Kiranga ninacho amini mimi kitakua tofauti na wewe, nafikiri itakua ngumu wewe kunikubalia mimi au mimi kukubalia wewe, kiukweli mambo ya Rohoni ni ya kiimani zaidi na sio physical, ukitaka niweke uthibitisho katika ulimwengu huu wa kawaida ni ngumu na haiwezekani, vya rohoni ni rohoni na vya mwili ni vya mwilini.

Naamini Biblia Takatifu, Naamini katika Mungu wa Bwana wangu Yesu Kristo.

Warumi 10 : 17 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.


Kipi si cha imani?
 
Last edited by a moderator:
.....kwa utafiti wangu roho ipo kwenye vitals organ, ambavyo ni ubongo,moyo,mapafu, ini na tumbo. Hivi vitu vimeshikilia roho.

Kimojawapo kisipofanya kazi hapo ndio mwisho wako umefika.
This is great info.
 
Wajuzi wa mambo haya mje hapa kunipa elimu juu ya hili. Je,iko kichwani,kifuani,moyoni,miguuni au mikononi? Mtu anapokufa,'roho' hufanyaje?

Wakuu Kiranga Shy land na Ishmael nawakaribisha pamoja na wengine kwa elimu.


Hebu tuzungumzie jinsi Biblia inavyotumia neno "roho." Watu fulani hufikiri kwamba "roho" ni neno lingine linalomaanisha "nafsi." Lakini, si kweli. Biblia inaonyesha wazi kwamba "roho" na "nafsi" ni vitu viwili tofauti. Vinatofautianaje?

Waandishi wa Biblia walitumia neno la Kiebrania ru′ach au neno la Kigiriki, pneu′ma waliporejelea "roho." Maandiko yenyewe yanaonyesha maana ya maneno hayo. Kwa mfano, andiko la Zaburi 104:29 linasema: "[Yehova] ukiiondoa roho [ru′ach] yao, wanakata pumzi, na kurudi katika mavumbi yao." Andiko la Yakobo 2:26 linasema kwamba "mwili bila roho [pneu′ma] umekufa." Katika andiko hilo "roho" inamaanisha kile ambacho huupa mwili uhai. Bila roho, mwili umekufa.

Kwa hiyo, katika Biblia neno ru′ach halitafsiriwi tu "roho" bali pia "nguvu" au kani ya uhai. Kwa mfano, Mungu alisema hivi kuhusu Mafuriko ya siku ya Noa: "Ninaleta gharika ya maji duniani ili kuharibu kutoka chini ya mbingu wote wenye mwili walio na nguvu [ru′ach] za uhai ndani yao." (Mwanzo 6:17; 7:15, 22) Hivyo, "roho" inarejelea nguvu isiyoonekana, inayotendesha viumbe vyote vilivyo hai.

Redio
Nafsi na roho hutofautiana. Mwili unahitaji roho kama vile redio inavyohitaji umeme ili kufanya kazi. Kwa mfano, unapotia betri katika redio na kuiwasha, nguvu zilizo katika betri huiwezesha redio kufanya kazi.

Hata hivyo, redio haiwezi kufanya kazi bila betri. Hali kadhalika, redio ambayo imeondolewa kwenye umeme haiwezi kufanya kazi. Vivyo hivyo, roho ni nguvu ambayo hutendesha mwili wetu. Kama umeme, roho haiwezi kuhisi wala kufikiri. Ni nguvu isiyo na utu. Lakini bila roho au kani ya uhai, "tunakata pumzi na kurudi kwenye udongo," kama mtunga-zaburi alivyosema.

Andiko la Mhubiri 12:7 linasema hivi linapozungumzia kifo cha mwanadamu: "Mavumbi [mwili wake] huirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho yenyewe humrudia Mungu wa kweli aliyeitoa." Roho au kani ya uhai inapoondoka mwilini, mwili hufa na kurudi ulipotoka, yaani, kwenye udongo. Vivyo hivyo, nguvu ya uhai hurudi ilipotoka, yaani, kwa Mungu. (Ayubu 34:14, 15; Zaburi 36:9) Hiyo haimaanishi kwamba nguvu ya uhai huenda mbinguni kihalisi.

Badala yake, inamaanisha kwamba mtu akifa, tumaini lolote la kuishi tena linamtegemea Yehova Mungu. Ni kana kwamba uhai wake uko mikononi mwa Mungu. Ni kupitia nguvu za Mungu tu ndipo roho au nguvu ya uhai inaweza kurudishwa ili mtu aweze kuishi tena.

Inafariji kama nini kujua kwamba hivyo ndivyo Mungu atakavyofanya kwa wote wanaopumzika ndani ya "makaburi ya ukumbusho!" (Yohana 5:28, 29) Wakati wa ufufuo, Yehova atamfanyizia mwili mpya yule anayelala katika kifo na kuuhuisha kwa kutia roho, au nguvu ya uhai ndani yake. Itakuwa siku ya shangwe sana.

Anyways, nilisha jibu hii kiundani sana kwenye mada moja iliyopo kwenye jukwaa lenu la dini.
 
Kinacho onekana kwa macho ya kawaida, kila mtu ana uwezo wa kukiona na kukishika.

Unajuaje kwamba unachofikiri unakiona kwa macho kipo kweli na si ndoto, mauzauza, maruweruwe, mirage, bending of light, sleigh of hand, kanyaboya, karata tatu au hata a prank straight out from the playbook of "Punk'd" ?

Unajuaje kwamba unapoona kitu hujakiona kwa apparent light tu na si real light?

Ona hapa ujue hata vinavyoonekana kwa macho havijapita realm ya imani.
 
Kiranga Najua kwasababu ya Imani nilyo nayo, iliyo jengeka katika msingi wa neno la Mungu wa Bwana wangu Yesu Kristo ninae amini neno lake na kuliishi.


Unajuaje kwamba unachofikiri unakiona kwa macho kipo kweli na si ndoto, mauzauza, maruweruwe, mirage, bending of light, sleigh of hand, kanyaboya, karata tatu au hata a prank straight out from the playbook of "Punk'd" ?
 
Last edited by a moderator:
Wajuzi wa mambo haya mje hapa kunipa elimu juu ya hili. Je,iko kichwani,kifuani,moyoni,miguuni au mikononi? Mtu anapokufa,'roho' hufanyaje?

Wakuu Kiranga Shy land na Ishmael nawakaribisha pamoja na wengine kwa elimu.

Now, let me answer regarding the location of your Spirit, where is the spirit/soul located in a human body?"

In the whole body. Without the spirit and soul your body could not/would not live. It is the essence and intellect of your being and can not be confined to one area.
 
Kiranga ! Najua kwasababu ya Imani nilyo nayo, iliyo jengeka katika msingi wa neno la Mungu wa Bwana wangu Yesu Kristo ninae amini neno lake na kuliishi.

Ukiwa na imani, hujui.
Ukijua, huamini.

The two are mutually exclusive.
 
Last edited by a moderator:
Wajuzi wa mambo haya mje hapa kunipa elimu juu ya hili. Je,iko kichwani,kifuani,moyoni,miguuni au mikononi? Mtu anapokufa,'roho' hufanyaje?

Wakuu Kiranga Shy land na Ishmael nawakaribisha pamoja na wengine kwa elimu.

Inawezekana kuna roho ndani ya miili yetu pindi ikiwa na uhai. Roho nahisi ipo kila sehemu ya mwili wa binadamu ila hakuna mtu aliewahi kuifafanua jinsi ilivyo. Tukifa na kufufuliwa (Yesu atakaporudi) tutaweza kujua ukweli wa roho.
 
Unawezaje kuthibitisha hili kwa ushahidi madhubuti ili tufahamu kwamba unachosema ndicho na si habari za mapokeo tu zisizo na ukweli?

Kiranga binadamu ana huruma, hasira,na hekima.
kama utakumbaliana na hivyo vitu kwamba binadamu anavyo.

uniambie huruma huwanga inakaa wapi? katika mwili wa binadamu.
 
Last edited by a moderator:

How would you know macroevolution is fact? Do the chemicals force that delusion?

As a non theist, how could you choose rationally to believe Darwinian dogma - apart from chemical delusions. What non-chemical part of you exists to choose apart from chemical delusion?

look at this fool??? ivi anajua swali la hii mada kweli au? MOD ni nani jaman watu wenye ugonjwa wa akili kama hawa wanatujazia server hapa!!!
 
Habari ya upepo tushaiongelea hapa kuanzia chanzo chake (mwendo wa hewa kutoka kwenye pressure kubwa kwenda kwenye ndogo) mpaka kifaa cha luupimia (anemometer).

Roho ni nini na tutajuaje kwamba ipo kweli na si hadithi ya kuungaunga tu?

sasa ndugu Kiranga, nini kinatufanya tuwe hai?
 
Mtoa mada ungejifunza kwanza roho ni nini ili uweze kujua kama inaweza kukaa sehemu au haiwezekani!
 
Mtoa mada ungejifunza kwanza roho ni nini ili uweze kujua kama inaweza kukaa sehemu au haiwezekani!

Akimaliza kujibu swali lako.
Ajiulize mawazo yanakaa sehemu gani katika mwili
 
Back
Top Bottom