Kweli kua uyaone! Natamani nirudishe siku nyuma nirekebishe nilipokosea ila siwezi

Kweli kua uyaone! Natamani nirudishe siku nyuma nirekebishe nilipokosea ila siwezi

Jackson amoss

Member
Joined
Nov 8, 2023
Posts
10
Reaction score
58
Nilipo angalia majibu yangu ya kidato cha nne nililia sana nilipoona nimepata 4 kumbe kilio kile niliona mbali sana wakuu.

Maisha yananichapa vibaya sana kulala njaa kwangu imekuwa jambo la kawaida. Inafika hatua naeanda kwenye mihangaiko wiki nzima siambulii chochote daah 😠.

Natamani nirudishe siku nyuma nirekebishe nilipo kosea ila siwezi. Inafika hatua natamani nisingezaliwa sio kwa msoto huu. Usingizi hata hauji mawazo masaa 24 kichwa kinawaza tuu.
 
Nilipo angalia majibu yangu ya kidato cha nne nilia sana nilipoona nimepata 4 kumbe kilio kile niliona mbali sana wakuu...
Usichokijua ni kwamba Kuna wenzako Wana degree mpaka 3 na bado maisha yanawapiga na hapo hapo wapo kama ww mtaani na wanaishi fresh tu usikariri kutoboa maisha sio lazima uwe umesoma tu.

Dedication: Yatapita by Chibu Dangote.
 
Ubaya kwenye maisha hakuna kushikiana, kwamba aahh, bwana makaveli nishikie maisha yangu haya kwa muda nipumzike nitakuja kuchukua.

Mzee kwakiwa upo hai, una nguvu hakuna kukata tamaa japo kuwa inaumiza na kukatisha tamaa, usikate tamaa pambana kadri uwezavyo. Maisha yana siri nyingi nzito
 
Wew unawaza kuishia form 4 ndo ulipokosea wengine wanawaza bora wangefeli wafaye ishu nyingine na sio kusoma.

Na kingine nilichokijua sasa hivi ni kua vijana tunakosa fursa kwasababu hatuna taarifa sahihi. Sababu ni eidha watu tunaoongea nao au story zetu kwao. Taarifa sahihi zina nguvu sana, taarifa za kazi, watu wa kutoa michongo, michongo ya watu na hustle zao nk.

Umemaliza hiyo form 4 mwaka gani na una umri gani?
 
Homeboy! Homeboy! Sijui hupo mkoa gani kama hupo dar es salaam nataka nikuelekeze uwende ukafanye kazi hapo unaenda na barua yako ya serikali ya mtaa unaoishi

kama unapajua sehemu mmoja pakuitwa vingungut kwenye kiwanda cha Pepsi ukifika hapo getin utaona watu wanasotea kazi waulize eti hapa kiwanda cha chuma kipo wapi watakuonesha ukifika hapo

kiwandani ulizia neno SHANANGA HARD WARE ni wapi watakuonesha ni geti lile pale ukifika muone mlinzi muelezee shida zako atakupa muongozo na siku hiyo hiyo unapata kazi hapo kwa siku 15 hadi 20 au zaidi ni wewe juhud yako machaka yapo mengi hayo mengine kipato kidogo utateseka ukishaingia humo utapata information nyingi tu
 
Kiwanda cha chuma show zao sio za kitoto mkuu
 
Homeboy! Homeboy! Sijui hupo mkoa gani kama hupo dar es salaam hasa hasa mbagala nataka nikuelekeze uwende ukafanye kazi hapo unaenda na barua yako ya serikali ya mtaa unaoishi na copy ya kitambulisho cha mpiga kula au NiDa

kama unapajua sehemu mmoja pakuitwa mbagala rangitatu kwenye kiwanda cha Rasta (Darlin) ukifika hapo getin utaona watu wanasotea kazi. Waulize "vipi naweza unganishwa na mimi nikaanza kazi ""

Au muone mlinzi muelezee shida zako atakupa muongozo na siku hiyo hiyo unapata kazi hapo kwa siku 7k hadi 10k
Narudia tena hom boy homboy hii ni kama kule kwenye ishu heavy ya chuma ikiwa imekushinda maana kazi za viwandani hasa upande wa hardware wee pasikie tuu.
 
Back
Top Bottom