Kweli kweli wameiba! Je, tupo tayari kwa vikwazo (Sanctions)? Nani ataathirika: Mimi na Wewe au Mwanasiasa?

Tutaendelea kuathirika kama tunavyoathiriwa na CCM.
 
Ndio maana mabalozi walimsindikiza hawana akili wale
 
Kwa hiyo na Marekani watawekewa nikwazo na dunia au siyo jomba...si Trump anahisi na anasema ameibiwa kura..kaenda mahakamani..Joe Biden atawekewa vikwazo sijui na nchi gani Sasa...hahahaha
Karuhusiwa kwenda mahkamani huku kwetu hata vituo havikubandika matokeo vikachora
 
Hivi miaka mitano iliyopita Magufuli, hajatuwekea vikwazo vya uchumi wananchi wake? Mbona uligwaya kulalamikia vyuma kukaza? Mbona hukulalamika kuwaondoa watu kazini kwa uonevu? Mbona hukulalamika watu kukosa ajira? Mbona hukulalamika Watu biashara zao zimefilisiwa? Mbona hukulalamika Sekita binafsi imevurugwa? Mbona hukulalamika watu kutekwa na kupotezwa Jumla? Ukweli ni kwamba vikwazo vya uchumi vilishaanzishwa tayari na Magufuli!!!
 
Musiogope kuwekewa vikwazo na mabeberu.
 
Yaani wazungu watuwekee vikwazo mwaka 2020 duu, kweli alili ni mali, kwamba wao peke yao ndo wanaendesha dunia au? Tena wakijadai kuweka vikwazo tunaenda na nchi za Asia, CHINA, INDIA, n.k
Huyo mchina bila ya kuwa unatumia $ dola kwenye biashara na wewe hakutaki nenda na pesa yako ya madafu
 
Onesha kituo kilichobandika matokeo
 
Umewahi kumwambia JIWE na jamaa yake Mahela hizi hatari?
 
Yaani wazungu watuwekee vikwazo mwaka 2020 duu, kweli alili ni mali, kwamba wao peke yao ndo wanaendesha dunia au? Tena wakijadai kuweka vikwazo tunaenda na nchi za Asia, CHINA, INDIA, n.k
Zimbabwe ya Mugabe walikuwa na majibu ya hii umeandika leo kawaulize maisha yao
 
Kwa hiyo na Marekani watawekewa nikwazo na dunia au siyo jomba...si Trump anahisi na anasema ameibiwa kura..kaenda mahakamani..Joe Biden atawekewa vikwazo sijui na nchi gani Sasa...hahahaha
Joe atawekewa vikwazo na Tanzania..
 
Kifupi kukitokea vikwazo Lisu asije kanyaga Tanzania na ndio mwisho wa Chadema na upinzani Tanzania watachukiwa kupita maelezo .Tutarudi mfumo wa chama kimoja Kama China
Kihalisia mpaka sasa tuko chini ya mfumo wa chama kimoja,mengine ni zuga ya kuwazuga mabeberu watuone kuwa tuko kwenye mfumo wa vyama vingi.
 
Ukishakuwa mnufaika wa huu utawala lazima akili zikutoke,mbuzi wewe.
 
Zimbabwe ya Mugabe walikuwa na majibu ya hii umeandika leo kawaulize maisha yao
Kesi ya Zimbabwe Ni tofauti kule wanasiasa walipora mashamba ya wazungu na kujigawia wao na familia zao
 
Duh!? Waafrika chini ya jangwa la Sahara tunaitwa kila majina, mara manyani, mara akili zetu ndogo,mara ni binaadamu lakini hatujatimia,sub human being

Lakini wewe umemzidi,wewe ni mfano mzuri wa Mwafrika chini ya Jangwa la Sahara

Mkuu,weka hisia zako pembeni angalia uhalisia wa ule Uchaguzi,je ule ulikuwa Uchaguzi au ubaguzi?
 
Wewe una uhakika gani kwamba alipigiwa kura halali? Wewe unajua mchezo uliokuwa unafanyika kwenye vituo vya kupigia kura?, Kwenye kituo unakuta kapata kura 37 alafu inaongezwa sifuri moja na kuwa 370 huku Lissu akiandikiwa chache zaidi ya alizopata, mawakala wanafukuzwa kwenye vituo?
 
Kuna comment pale juu mdau katoa kumuhusu Samson that's real instance.

Pamoja na kuwepo binadamu wanaopinga maandiko
(live) lakini inapaswa ieleweke wazi kwenye kutafuta haki na amani lazima wengine wafe ili walio nyuma waishi kutokana na imani ya waliokufa.

Issue ya kupigwa pin na mabeberu as Zimbabwe ndiyo itakuwa funzo kwa watakaobaki, kumbuka; huwezi kudai haki ukiwa unakunywa juice na mdai wako mezani!.
 
.....kuna neno linatumikaga vibaya sana "MSIONE WATANZANIA WAJINGA" nikilionaga ua nacheka sana,ofcourse CCM wanawafanya Watanzania ni WAJINGA ndo maana yote haya yanatokea,kwa mgongo wa AMANI.

Sent from my SM-A9000 using JamiiForums mobile app
 
neno mabwana zao.unalotumia linakutoa kwenye HOJA husika....kwa nn waitwe mabwana? je na wakitoa msaada kwa magufuli nao watabakia.na.jina hilohilo au wataitwa wadau wa maendeleo? kimsingi LISSU ana hoja ya msingi....na yupo sahihi kutafuta msaada nje kadri atavyoona inafaaa maaana hamna sehemu.nyingine yakumshitaki mtesei wako zaidi ya huko.

Sent from my SM-A9000 using JamiiForums mobile app
 
Nadhani lengo kuu la vikwazo ni kuwashinikiza wananchi waichukie serikali iliyopo madarakani na kisha waikatae kwa vitendo.Maana wao wakija directly kuitoa tutawajibu "sisi ni nchi huru" hivyo vikwazo ni indirect way ya kutimiza lengo lao la msingi(kuing'oa serikali ilyopo madarakani).Tanzania ni yetu sote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…