Kweli kweli wameiba! Je, tupo tayari kwa vikwazo (Sanctions)? Nani ataathirika: Mimi na Wewe au Mwanasiasa?

Kweli kweli wameiba! Je, tupo tayari kwa vikwazo (Sanctions)? Nani ataathirika: Mimi na Wewe au Mwanasiasa?

Usiweweseke jomba..usidhani wazungu hawana akili au wajinga kiasi hicho...kwanza wamsikilize na kumuamini lisssu kama Nani..Lissu hana ushahidi wa lolote ni Mambo ya hisia tu...Sasa Nani anayeweza fanyia kazi hisia...
Waangalizi wa ndani, wa kimataifa woote wale hawana akili, ripoti zao zoote in maana Ni utumbo tu..acheni kuweweseka..Lissu Hana lolote...
Kwa tàarifa yako mataifa makubwa haya hayategemei taarifa za Lisu au waangalizi bali wanategemea taarifa za inteligensia zao tu. Wanajua hata ikulu kuna nini kwenye mvungu wa kitanda. Ukweli wa yaliyotokea uchaguzi huu hayajifichi kwani tayari mitaani yanatrend. Vituo vingi hawakuhesabu kura vituoni kwani masanduku yalibebwa na vijana wa jkt kabla ya kuhesabiwa na kuna baadhi ya vituo hata wahudumu waliachwa wakapanda boda boda. Tunaelewa sasa kuwa karatasi za matokeo sehemu kubwa zilishajazwa hata kabla ya upigaji wa kura kuisha na wasimamizi wakalazimisha kuyasoma, kama yule wa Arusha aliyesema nanukuu ' Nasoma kama yalivyoandikwa' .
Kwa haya yote yaliyotokea sielewi hata hao washindi wanapata wapi ujasiri wa kupita kwa wapiga kura na kudai wao ndio washindi. Kibaya zaidi hata wasimamao madhahuni wanathubutu kumdanganya Mungu kuwa waneshinda na sijui wanaweza kufanya maombi ya shukurani nafsi zao zisiwasute.
 
Mbona unatumia nguvu nyingi sana kupingana na ukweli? Hata kama mfumo unakufaidisha ni bora ungekaa kimya kwa madudu tuliyofanya uchaguzi huu. Ni aibu kwa mtu yeyote mwenye utu wake.
Halafu asivyo kuwa na aibu, eti asilimia 80 wamemkubali JPM. Huko ni zaidi ya kujitoa ufahamu!
 
Afu wazee mbona twitter yangu tangu jana haifunguki nikaifuta nikadownload upya bado tu hata kulog in inasumbua .Kuna mwingine ana shida hii?
 
Siku mbili kabla ya uchaguzi Lissu alituambia wameweka mawakala nchi nzima zaidi ya 80,000.
Na kwataarifa ya tume nchi nzima kulikuwa na vituo 82,000.
Leo upinzani wanadai wameibiwa kura, serious?
Hao mawakala walikuwa wapi? Kwanini wasituwekee hapa form za mawakala ambazo zipo tofauti na matokeo ya tume iliyoyatangaza ili sisi kina Tomaso tuamini?
Ugumu upo wapi kwenye hilo?
Malalamiko mengi ya kuibiwa naona yapo kihisia tu.
Ukweli utatuweka huru. WaTZ wamewakataa wapinzani. Kauli za mgombea Lissu ktk kuomba kura hazikuwa za kiungwana na ndie aliyewanyima viti vya ubunge wapinzani.
Asitafutwe mchawi!
1.Kwanini mlizuia matokeo ya urais kubandikwa vituoni?
2.Kwanini mlizima mitandao?
3.Kwanini tallying centre mmekamata watu wakijumlisha matokea mmewabambikizia kesi ya kukutwa na mabomu na mpaka sasa mmemficha Mazrui?
 
Raisi uliyepo madarakani unaibiwaje kura?
Kwa hiyo na Marekani watawekewa nikwazo na dunia au siyo jomba...si Trump anahisi na anasema ameibiwa kura..kaenda mahakamani..Joe Biden atawekewa vikwazo sijui na nchi gani Sasa...hahahaha
 
Atakaye dai haki Ni Nani Sasa hapa..ikiwa asilimia zaidi ya 80 ya wananchi wanamuunga mkono JPM na serikali yake. Au unadhan JPM kajipigia kura mwenyewe nchi nzima...hahahah..msiwachukulie poa wananchi wa Tanzania ..upinzani una Nini huu..hakuna lolote...na nasema watanzania wataendelea kuwanyima kura Kama mtaendelea nanupinzani usiokuwa na tija
Mbona kama umepanic?
 
Bora tuteseke kwa muda ,hamna mtu mwenye mamlaka na hii nchi
 
Umesema kwa upole na weledi, umemuelimisha taratibu kwa kiswahili rahisi kabisa.
Kama hajaelewa tena tumuache tukanunie cement 35,000
Mkuu unahitaji mabadiliko ya mifumo huru huku ukiwa unagonga kashata na kahawa umerelax? vikwazo vitawatumia ujumbe watawala kuwa dunia inaona hivyo wajirekebishe na watende haki kwa wananchi, pia wananchi waoga wakichapika kisawasawa na maisha siku nyingine wakiambia daini haki yenu hakuna ataebaki ndani, kwa ujumla unafiki wa kutukuza watawala dhalimu utaisha. Hizo ndizo gharama za kudai haki.
 
Usiweweseke jomba..usidhani wazungu hawana akili au wajinga kiasi hicho...kwanza wamsikilize na kumuamini lisssu kama Nani..Lissu hana ushahidi wa lolote ni Mambo ya hisia tu...Sasa Nani anayeweza fanyia kazi hisia...

Waangalizi wa ndani, wa kimataifa woote wale hawana akili, ripoti zao zoote in maana Ni utumbo tu..acheni kuweweseka..Lissu Hana lolote...
Wakati Makonda anawekewa vikwazo uliwekwa ushahidi gani?
Mabalozi wa nchi tatu kumsindikiza mtu mmoja bado unajiaminisha ya kuwa mtu huyu ni mkulima wa viazi wa Lushoto?

Kama Taifa kuna mahali tumeteleza inabidi tuache kujidanganya.
Diplomasia yetu imepinduka kidogo katika miaka hii mitano ni lazima tukae vizuri na tujirekebishe ila bahati mbaya unafiki umetujaa na hakuna wa kuwaambia viongozi wetu kuwa suruali imetoboka mahali.Kikwete anajua dhahiri repercussion ya mrengo tunaochukua.
 
1.Kwanini mlizuia matokeo ya urais kubandikwa vituoni?
2.Kwanini mlizima mitandao?
3.Kwanini tallying centre mmekamata watu wakijumlisha matokea mmewabambikizia kesi ya kukutwa na mabomu na mpaka sasa mmemficha Mazrui?
Kwakawaida mawakala wanakuwa na form wanazo sign baada ya kuhesabu kura.
tuonesheni hizo tofauti Kati ya mawakala wenu na tume hata kwa matokeo ya ubunge na udiwani itapendeza.
Hizo zingine ni blah blah tu
 
Kwakawaida mawakala wanakuwa na form wanazo sign baada ya kuhesabu kura.
tuonesheni hizo tofauti Kati ya mawakala wenu na tume hata kwa matokeo ya ubunge na udiwani itapendeza.
Hizo zingine ni blah blah tu
Kuna uzi hapa wa ushuhuda,unaweza kuutafuta!
 
Yaani wazungu watuwekee vikwazo mwaka 2020 duu, kweli alili ni mali, kwamba wao peke yao ndo wanaendesha dunia au? Tena wakijadai kuweka vikwazo tunaenda na nchi za Asia, CHINA, INDIA, n.k

China alikuwa rafiki mkubwa wa Zimbabwe wakati wa vikwazo, kaangalie hali ya Zimbabwe ndio ujue wazungu ndio wenye hii dunia.
 
Mkuu unahitaji mabadiliko ya mifumo huru huku ukiwa unagonga kashata na kahawa umerelax? vikwazo vitawatumia ujumbe watawala kuwa dunia inaona hivyo wajirekebishe na watende haki kwa wananchi, pia wananchi waoga wakichapika kisawasawa na maisha siku nyingine wakiambia daini haki yenu hakuna ataebaki ndani, kwa ujumla unafiki wa kutukuza watawala dhalimu utaisha. Hizo ndizo gharama za kudai haki.
Kwani kudai haki Ni kuwachagua cdm? Vipi kwa wale ambao waliichagua ccm hawana haki hiyo?
 
Sidhani vikwazo vitafua dafu sisi ni donor country.tuna Kila kitu wawaulize kenya,
 
Nadhani lengo kuu la vikwazo ni kuwashinikiza wananchi waichukie serikali iliyopo madarakani na kisha waikatae kwa vitendo.Maana wao wakija directly kuitoa tutawajibu "sisi ni nchi huru" hivyo vikwazo ni indirect way ya kutimiza lengo lao la msingi(kuing'oa serikali ilyopo madarakani).Tanzania ni yetu sote.
Kwahiyo tukiwekewa vikwazo ni kipi ambacho tutafanya wananchi ili kuikataa serikali kivitendo?
 
Sasa unataka Lissu afanye nini? Lissu hawezi kuandamana mwenyewe barabarani. Hiyo ndio option iliyobaki. Lissu hawezi kwenda msituni. Ngoja tu tubinywe labda tutapata akili.
Mnakumbuka yaliyoendelea Zimbabwe au Somalia au Iran.
Ni ukweli Haya majamaa yameiba kura yameua watu Zanzibar, lakini je hatua anazochukua Lisu na wapinzani za kutusema kule duniani je mnadhani madhara ni kwa nani? Kwa jiwe au mm na wewe?

Mshahara WA jiwe Kwa mujibu WA scale za serikali Ni million 32 Kwa mwezi na hiyo kabla ya marupurupu.. mshahara WA mbunge Ni million 8 kabla ya marupurupu..

Lisu anadai alishinda na kaibiwa Kura ok let say Kweli ndiyo kaibiwa na Sisi tunaamini hivyo. Mimi na wewe hatukatai kuwa uchaguzi ulikuwa Ni uchafuzi TU.
Mwaka 2015 uchaguzi haukuwa huru na haki; ndiyo hili tunakubali. Mwaka huu haukuwa uchaguzi Bali uchafuzi TU..

Wasiwasi Wangu je hizi hatua za kutusema duniani ambazo Lisu atazianza soon zitakuwa na faida Gani Kwa Sisi wanyonge.? Unadhan vikwazo ailivyopigwa Zimbabwe je zilimuathiri Mugabe na watoto wake au Morgan tshangarai..au watu wanyonge km mm na wewe.

Aisee asikudanganye mtu hakuna USA , sijui UN au Europe watakaokuja kumtoa kwa nguvu magufuli.. wazungu watakachofanya ni kutupiga vikwazo (sanctions) vya kufa MTU.

Twende kwenye vikwazo unadhan nani ataarithika..Lisu atakuwa zake Brussels- Belgium akila mvinyo au akigonga Budweiser.

Magu atakuwa ikulu akila samaki WA kuchoma na bia pendwa ya Kilimanjaro na akisisitiza tumuombee..na wakina gwajima watakuwa busy kutuaminisha tumuombee wakina Diamond wakirunga nyimbo za kumsifu.

Mimi na wewe wanyonge Sisi tutakuwa tunalala njaa.. sanctions hatutoruhusiwa tena kununua au kuuza vitu nje ya Nchi.

Lisu Pole sana brother..lakini hatua unazochokua zitatuumiza Mimi na wanyonge, wewe na magu hamtoathirika.

Uzuri Ni kuwa CCM na chadema wote tutaisoma namba TU Kwa sanctions.. Vikwazo visikie Kwa jirani.

SEMA mjomba Magu punguza basi Mzee..
kuzima mitandao..ubabe siyo mpango., unatumia rungu kuua sisimizi...Sisi wanyoyonge mtuhurimie. Lol
 
Back
Top Bottom