Mnakumbuka yaliyoendelea Zimbabwe au Somalia au Iran.
Ni ukweli Haya majamaa yameiba kura yameua watu Zanzibar, lakini je hatua anazochukua Lisu na wapinzani za kutusema kule duniani je mnadhani madhara ni kwa nani? Kwa jiwe au mm na wewe?
Mshahara WA jiwe Kwa mujibu WA scale za serikali Ni million 32 Kwa mwezi na hiyo kabla ya marupurupu.. mshahara WA mbunge Ni million 8 kabla ya marupurupu..
Lisu anadai alishinda na kaibiwa Kura ok let say Kweli ndiyo kaibiwa na Sisi tunaamini hivyo. Mimi na wewe hatukatai kuwa uchaguzi ulikuwa Ni uchafuzi TU.
Mwaka 2015 uchaguzi haukuwa huru na haki; ndiyo hili tunakubali. Mwaka huu haukuwa uchaguzi Bali uchafuzi TU..
Wasiwasi Wangu je hizi hatua za kutusema duniani ambazo Lisu atazianza soon zitakuwa na faida Gani Kwa Sisi wanyonge.? Unadhan vikwazo ailivyopigwa Zimbabwe je zilimuathiri Mugabe na watoto wake au Morgan tshangarai..au watu wanyonge km mm na wewe.
Aisee asikudanganye mtu hakuna USA , sijui UN au Europe watakaokuja kumtoa kwa nguvu magufuli.. wazungu watakachofanya ni kutupiga vikwazo (sanctions) vya kufa MTU.
Twende kwenye vikwazo unadhan nani ataarithika..Lisu atakuwa zake Brussels- Belgium akila mvinyo au akigonga Budweiser.
Magu atakuwa ikulu akila samaki WA kuchoma na bia pendwa ya Kilimanjaro na akisisitiza tumuombee..na wakina gwajima watakuwa busy kutuaminisha tumuombee wakina Diamond wakirunga nyimbo za kumsifu.
Mimi na wewe wanyonge Sisi tutakuwa tunalala njaa.. sanctions hatutoruhusiwa tena kununua au kuuza vitu nje ya Nchi.
Lisu Pole sana brother..lakini hatua unazochokua zitatuumiza Mimi na wanyonge, wewe na magu hamtoathirika.
Uzuri Ni kuwa CCM na chadema wote tutaisoma namba TU Kwa sanctions.. Vikwazo visikie Kwa jirani.
SEMA mjomba Magu punguza basi Mzee..
kuzima mitandao..ubabe siyo mpango., unatumia rungu kuua sisimizi...Sisi wanyoyonge mtuhurimie. Lol