ndio maana soko huria hawawezi na wanaliogopa kuliko TBC wanavyoogopa media huru:Hasa kwenye *pricing policy*, mfano ATCL from Mwanza to Dsm kama ukitaka kusafiri January unatakiwa ulipe 180000 lakini mshindani wake mkuu ni 120000, so automatically hapo kwa mtu asiye wa serikali ambaye anajilipia sio kulipiwa na serikali lazima atachoose low cost.....So yanaweza jirudia yaleyale na ndoto ya JPM ikashindwa kukamilika kwa kulipia ticket sh 70000....
Ndio maana mkuu NOD RwandAir mpaka sasa ndege zake zooote za Bombardier zipo chini ya Ethiopia kuanzia Marubani mpaka wahandisi,na wameingia mkataba wa miaka saba wa kuhudumiwa na Ethiopia kwenye wahandisi na marubani.Sasa kwa maana ya kubana matumizi kama sera ya JPM ilivyo,na sisi tukiingia kwenye mfumo huu kwenye dreamliner,ina maana dhana hiyo inakuwa haifanyi kazi.
Ethiopia wana Bombadia na Boeing tu za kawaida,kwa maana ya B737,B738,B767,B757 na B777...,hii Dreamliner ni ETOPS,ndio maana hata wao wana uhaba wa mainjinia na marubani licha ya utabe wao ktk soko la usafiri wa anga.Sisi tungeweza kuanza na B737,B738 kabla ya kufika kwenye Dreamliner.Kumbuka rating ya dremliner sio ya kitoto mkuu
Note:Namuunga mkono JPM na suala lake la kuifufua ATCL,mjadala huu si nia ya kuikatisha tamaa ATCL,ni mawazo tu ktk kuchangia mjadala juu ya ufufuaji wa ATCL...
Mkuu,nami nina wasiwawi huu,kama kweli ufufuaji wa ATCL ni kwa ajili ya kuinua uchumi ama ni kwa ajili ya sifa ya kwamba nasi tuna shirika la umma lenye ndege nyingi!?Tunanunua ndege hizi kwa sababu analysis zote zinaonesha zitakuza uchumi wetu au ni prestige tu ya kusema na sisi tuna ndege? Inapendeza kuwa na shirika la ndege lakini sishawishiki kabisa kuwa hizi ndege zitatuongezea uwezo wetu wa kiuchumi, zaidi ninachoamini zitaendelea kula kidogo tulicho nacho.
Siamini kama ndege hizi zitaongeza utalii maana sijaona ni kwa namna gani.
Rwanda walishakwama kitambo. Ni ujeuri tu wa rais wao.Watabiri wamerudi tena!!!
Awamu hii Ni mwendo wa kutabiri kushindwa tu!!!
Lkn mtoa mada umejaribu kujenga hoja lkn haijitoshelezi!!! Hizo sio sababu kweli Za kuifanya ATCL ikwame Na hata ilipo kwama hapo nyuma kabla ya JPM sio kwa sababu hizo!!
RwandaAir wanazo Dreamliner na bombardier, Hao Ethiopia Airline nao hadi Leo hii wanazo Na hawajakwama, sisi ndio tumeanza naamini Na sisi hatutakwama!!!
Watanzania wanaaminika. Serikali ya CCMScrow ndo haiaminiki kufanya biashara hiyo ya ndege.Tatizo lako unaangalizia mpaka mwandiko.
Hivi unaelewa strategy za competition, hahaha kujipambanua kuwa tofauti na wengine ni advantages.
Siamini kama hoja elementary kama hazikufikiriwa mapema. Prof Mbarawa ni Engineer tena aliyebobea toka Majini mpaka Angani.
Hebu pia cambia za kuwa na dreamliner straight kutoka Detroit to Dar vs Boeing.
Tufike mahali tuwaamini watanzania wenzetu wafanye kazi tumeona nia yao.ni.nzuri.na kweli.wamekusudia kuinyanyua hii.nchi kiuchumi
... mbona kikwete kwa miaka10 hata Q400 ilimshinda?
Alishaletaga hizo vitu humi kitambo. Nadhani hujamfuatilia barafu sana. Huyo jamaa ni sapota mkubwa sana wa ATCL na hizo Dear Bomba zao. Labda ni agent wa Dear Bomba ([emoji41] [emoji41] ) anataka waendelee kupata soko la Tz.Hakuna utaalamu hapo.ila.ni kupotezeana muda.
Utalaamu angeingia deep atuletee fuel consumption per given united, maintenance cost per given operation hours/age, Speed and comfortability, na analysis He wamarekani wanapenda nini.kati ata Dreamliner na Boeing hasa watalii.
Alivoviweka ni vitu vya kawaida sana hata mnunuzi wa daladala huwa anavifanya
Eti? Tupia kapicha jamaaHuu upuuzi wao unakera, iweje ndege mpya kila kukicha ni hitilaf tuuu
Leo tena imefia arusha!!
Utaishia kuyauza kama Princess Muro wakati wenzie Dar Express na Kilimanjaro wanayaongeza ya platform moja. Marcopolo.Hivi jamani kwani kuna ubaya gani kuwa na Yutong,Scania,Higer na Zongthong Bus kwenye kampuni moja?
Sipati mantiki kabisa
Walikurupuka kwenye sukari kwahiyo kila wanachofanya kinahojika. Usiwe mwepesi kuamini serikali inajua kila kitu. Walau sio hii ya CCMScrow.Mkuu naomba muiamini selikari yenu. Selikarini kuna wataalamu zaidi ya huyu mleta maada. Kwa kawaida kila mtu na mawazo yake na siwezi kuyapinga ya mleta maada maana ni mawazo yake. Wahusika hawakukurupuka na naomba tusiwakatishe tamaa. Wanafahamu wanafanya nini. Mkuu keshasema wanataka ndwge ya masafa marefu ili watalii waje moja kwa moja anamaanisha na yuko sahihi sana. Seatback and relax waacheni waturekebishie nchi.
Tusichotaka wengi wetu ni serikali kuendesha biashara ya ndege. Hizo pesa kununua hiyo midudu kwa taslimu zikaboreshe huduma za jamii. Elimi. Afya. Maji. N.k.Hivi waTanzania tufanyiwe nini?
tukigeuka huku watu wanalia uchumi hoi...tukigeuka kule....ufisadi umetamalaki...Bwana Yule ndo anajitahidi angalau aweke mambo mstarini..kila mwananchi anakuja na yake. Sasa afanye nini? Ukitokea ukaona jema la Bwana Yule utaambiwa wewe ni sehemu ya CCM au unataka cheo.
Ila nilichogundua waTanzania wengi tumezoea na tunapenda siasa za kudanganyana (no wonder watu wanamkumbuka Kikwete humu). Tunapenda michakato kwa sababu ndo inatupa nafasi za kupiga hela. Ni mara ngapi bajeti zimepangwa na hela imeliwa? leo Magufuli anahukumiwa eti ananunua ndege bila bajeti ya Bunge! Wonders shall never cease!
Au atukusanye waTanzania wote pale uwanja wa taifa tujadili vipaumbele vya taifa kwa kunyoosha mikono?
wewe jamaa nimekufuatilia saana inaonekana unaiwaza ccm kila wakati...unaponda uku unabwabwaja tu...utake husitake magu kashaifufua ATCL....ukiona inakuuma hamia SYRIA_ALEPOAlishaletaga hizo vitu humi kitambo. Nadhani hujamfuatilia barafu sana. Huyo jamaa ni sapota mkubwa sana wa ATCL na hizo Dear Bomba zao. Labda ni agent wa Dear Bomba ([emoji41] [emoji41] ) anataka waendelee kupata soko la Tz.
Umeliweka vizuri. Hawa CCMScrow wananunuaga vitu ndo wanafanya study kwa roho za watu.Kawaida ya tz. Study haifaywi kabla ya uamuzi. Ona mifano. ndege ya rais, meli ya Bagamoyo, mabehewa rada na madudu mengine ambayo hayasemwi
Unaiwaza ccm tu...kunyaaa basi kila unapoiona bombardierUmeliweka vizuri. Hawa CCMScrow wananunuaga vitu ndo wanafanya study kwa roho za watu.
Mfano walidai Dear Bomba inatua viwanja vya ndani hadi vya changarawe. Matokeo yake juzi tu imekwama Arusha ambacho zaidi ya muongo mmoja ndege style yake zinatua hapo.
Huyo barafu kwa wanaomjua ni rahisi kumbaini humu maana ana shida sana ya ala (R) na ero (L).Tamko langu: Barafu huu ni ushauri wa msomi, ingawaje bro wakosea ukiandika 'ghalama' badala ya gharama. Ni kweli, katika hali ya kawaida Tanzania ingefaidika sana kwa kufuata ushauri wako. Ila kwa hali ya uozo ilipofikia Tanzania, naona tukimbie wakati wengine wakitembea. 'Baptism by fire" ndiyo inayotakikana hivi sasa. Kwa hiyo, ukiangalia kwa ncha hiyo, MAGU anafanya vizuri. Maana ukitaka kwenda mwendo wa kawaida utaanza kwa kusika wapi? Kwa mwendo wa kawaida tungeanza kwa kutengeneza viwanja vyetu kwanza, ili tuwe na usafiri imara wa ndani hata kabla ya wa nje. Usafiri wa ndani unegtuingizia fedha nyingi sana ambazo zinegetumika kusimika viwanda vidogo vidogo vinavyoendana na mahitajio ya ndege, kama vya kukaangia korosho na vya kutengeza wrapping yake n.k.
Utasubiri sana ifufuke. We ndo mbwabwajaji humu. Mi msimamo wangu uleule. ATCL haitofufuka asilani na serikali haina haja kufanya biashara ya ndege.wewe jamaa nimekufuatilia saana inaonekana unaiwaza ccm kila wakati...unaponda uku unabwabwaja tu...utake husitake magu kashaifufua ATCL....ukiona inakuuma hamia SYRIA_ALEPO
Pilau bila kachumbali haijanogaUmeandika vizuri sana..lakini tununue ndege Kwanza... Tuwe nazo km kumi na tano. Kachumbali ni nzuri pia