Kweli Mungu ni muweza wa yote?

NileSat

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2015
Posts
340
Reaction score
179
Kuna hili swala la kusema Mungu kashatupangia kesho yetu ipoje pia anajua wewe utafanya nini kesho kwa mantiki hiyo, Mungu ni muweza wa yote hata sisi atheist kashapanga tusikubali uwepo wake kama hajapanga na hivi tunafanyavyo tunajiamulia, basi tumtoe katika kundi la mpangaji wa yote. Hii ina maana hajui kesho yangu.

Naeleweka hivi! Hoja ya uwepo wa mungu inatafisiriwa kama moja ya harakati za mwanadamu aliyekataa tamaa ambae anajipa matumaini kwa nadharia hii kuwa itamsaidia...Mungu mwenye upendo iweje aruhusu watu sio na hatia kuuwawa mungu mwenye upendo anawambia viumbe wake wawaue wengine ili waione pepo?? Mapungufu ya science kueleza asili yetu wala hayamuumbi mungu au kumfanya awepo
 
Mungu ni muweza wa yote ndiyo ila siyo kwenye Dunia hii. Kwenye Dunia hii muweza wa yote ni Shetani Ibilisi na kipindi chake alichopewa kuitawala hii Dunia ni kifupi.
 
Mungu ni muweza wa yote ndiyo ila siyo kwenye Dunia hii. Kwenye Dunia hii muweza wa yote ni Shetani Ibilisi na kipindi chake alichopewa kuitawala hii Dunia ni kifupi.

Shetani katengenezwa na nani na kwa manufaa yapi labda?
 
Mungu ni muweza wa yote yalioko duniani,mbinguni na akhera na kokote kule unakokujua wewe.

Kwanini shetani anamzidi nguvu katika kikiendesha kiumbe chake alichokiambua (mwanadamu)
 
A rather exposing question.

Bertrand Russel, mwanahisabati na msoni wa mantiki wa kutoka Uingereza alishawahi kusema kwamba akifa na kukuta kuna mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na mwenye upendo wote, na akihukumiwa kwa kutoamini mungu, atamhoji mungu huyo kwa nini hajumpa akili za kumjua.
 

hueleweki
 
asante jirani ila huko nyumba ya pili sitii maguu kamwe...mana hata akili ya kawaida tu ya uwezo wa chini ya kufikiri haikubali kumkataa mungu..huu ulimwengu jinsi ulivoumbwa complex hivi burebure tu..mambo mengi ya ajabu na maarifa ya hali ya juu yamepangiliwa kiufundi hayawezekaniki kukosa aliyeumba na kuyaratibu.nikienda chumbani kwangu nikakuta kuna gunia la mkaa kitandani lazima nishtuke kuwa kuna aliyeliweka..akitokea mtu akasema hakika hilo gunia limetokea tu from nature nitamwona punguani...hvyo hvyo kwa ulimwengu na vilivyomo kuna muumbaji lazima.naamini nina moyo na unasukuma damu japo sijawahi kuuona,naamini dunia ni umbo kama la tufe na inalizunguka jua japo sijafanya safari ya kwenda nje ya dunia kushuhudia hayo.daktari akiniambia nina vidudu vya maleria kaona yeye kwenye darubini yake naamini kabisaa na ananipa dawa napona..sasa kwa mambo madogo hivi nayaamini kwa nini la mungu nilikatae eti kwa kuwa simuoni?? ethiests mna tumia akil ndogo sana kumkana Mungu..jirani toka huko uliopo njoo uishi upande huu
Doyi karibu katika uhuru jikomboe na utumwa wa kidini ambao una hasara zaidi kuliko faida....Jinasueeee
 
Last edited by a moderator:
Kazi kweli kweli
Nikuwaga nasimuliwa kuna watu hawaamini uwepo wa Mungu... lakini sasa najionea mwenyewe.
Believing God's existance is also a grace
 
Hapa sijui unajaribu kumchambua Mungu yupi...

Mungu nimjuaye mimi ambaye ni Muumba wa vitu vyote viijazavyo nchi anajua jana, leo na kesho ya mtu...

Wakati huo huo kila mwanadamu yu na nafasi ya kuamua hatma ya mambo yake...

Ubaya au wema unaoufanya umefanywa kutokana na utashi na maamuzi yako binafsi baada ya kuwaza na kuwazua katika fahamu zako...

 
Haya bhana......
Imani ni kitu hatari kuliko vyote. Nsijejilipua kwa mabomu mie
 
Yeye nae katokea wapi...who created God if the universe Doesn't create itself?
 

Complexity ni lazima iwe imeumbwa by design?
 
Kazi kweli kweli
Nikuwaga nasimuliwa kuna watu hawaamini uwepo wa Mungu... lakini sasa najionea mwenyewe.
Believing God's existance is also a grace

Mungu gani unayeamini kwamba yupo?

Kuamini unaruhusiwa kuamini chochote. Kina mikataba ya kimataifa kutetea imani yako. Lakini je, unajua kwamba mungu yupo?

Unaelewa tofauti ya kuamini na kujua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…