Kweli Mungu ni muweza wa yote?

Mungu ndiye aliyeumba Mbingu na nchi na kila kilichomo

Sasa kwa nini kaumba dunia inayoweza kuwa na matetemeko ya ardhi yanayoua watoto wasio na hatia wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao hauna matetemeko hayo?
 
Sasa kwa nini kaumba dunia inayoweza kuwa na matetemeko ya ardhi yanayoua watoto wasio na hatia wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao hauna matetemeko hayo?

Wewe huwezi jua mwenye hatia na asiye na hatia Yeye ndo anajua kama wana hatia ama hawana, pia ikumbukwe kuwa dhambi za wanadamu ndo chanzo cha haya yote maana hata maandiko yanasema mshahara wa dhambi ni mauti. Kama wapo wema waliokufa basi Mungu kaona ni wakati muafaka wa kuwachukua maana wakiendelea kukaa duniani wanaweza kuja kughafilika.
 

Hujaelewa swali.

Dhambi nayo ni kitu kibaya. Mungu alikuwa na uwezo wa muumba ulimwengu ambao dhambi haiwezekani.

Kwa nini hakuumba ulimwengu huo?

Na kwa nini mungu wa haki aachie majambazi mengine yalioua watu na Hitler yaishi mpaka miaka 90 wakati watoto wengine wanakufa bila hata kufikisha miaka mitano? Haki ikonwaoi hapo?
 

Sio kama sikuelewa swali ila ugumu wa jibu langu ndo limekufanya ushindwe kuoanisha na swali lako. Ikumbukwe kuwa wote ambao hawatendi mapenzi ya Mungu ni wana wa ibilisi ingawa aliyewaumba ni Mungu hivyo shetani nae huwatunuku walio wake kwa kuwapa vitu wanavyohitaji na Mungu huwa hazuii maana siku ya hukumu yaja na atakuhukumu kwa haki.
Najua utauliza kwanini Mungu akuachie utende maovu kumbuka kuwa shetani yupo kazini kwa lengo la kuwashawishi watu na kuwadanganya. Sasa ili na wewe uweze kutunukiwa taji lazima ufanye kazi ukiwa apa duniani na kazi yenyewe ni kutenda yale yanayompendeza Mungu.
 

Uko low sana mkuu!,umeulizwa mtoto mdogo anayekufa ana hatia gani?,we unajibu et huwez jua mwenye hatia!,poor!

Eti mungu kaona ni wakati muafaka kuwchukua!,aisee!,wewe bado kabisa ndugu
 
Kama ninavoamini jf kuna ma GT kama GT unatakiwa uwe open minded kuangalia vitu kwa undani zaidi bila uoga ili kuupata ukweli we should first question religion, question existance una like kutrace source ya life/existance kwenye holy books wanasemaje? Na evolution(science) inasemaje? Unapata majibu unaangalia which 1 is relevant even though inaeza raise doubts lisikutatize keep on digging for the facts based on vivid proof ondoa uoga then u might come up with jaw breaking answers na ukaanza kuiona dunia in a very new meaning....
 
Mungu anaweza yote ila anaheshimu maamuzi unayoyachagua.
 
Uko low sana mkuu!,umeulizwa mtoto mdogo anayekufa ana hatia gani?,we unajibu et huwez jua mwenye hatia!,poor!

Eti mungu kaona ni wakati muafaka kuwchukua!,aisee!,wewe bado kabisa ndugu

Ukirejea maelezo yangu ya nyuma hili swala nimelijibu vizuri. Nilisema kuwa mtu anapokufa inategemea Mungu alivyomuandikia bila kujali ni mkubwa ama mtoto.... Mungu anatufahamu kabla hatujazaliwa hivyo kuna wengine amewapangia wataishi duniani siku moja wengine wiki na kadhalika si kwa kuwa hawapendi hao wanaokufa wakiwa na siku moja hapana bali Mungu kwa kuona maisha yao yattakavyokuwa baadae kaamua kuwachukua mapema wakapunzike, pamoja na hilo ila tukumbuke kuwa vifo vingine vinasababishwa na shetani kwa namna tofauti tofauti. Najua utauliza kwa nini Mungu asizuie shetani asiwaue na kwanini hawa wanaokufa mapema kwa mapenzi yake kwa nini asiwaache wakue ila cha msingi elewa kuwa unapokufa Mungu tunasema Mungu kakupenda zaidi na sio kama anakuchukia ndo maana ukafa.
 

Pokea "like" yangu ya kutoka moyoni. Watu wanajiaminisha kwamba kusema hakuna Mungu na kuondoa habari ya creation ndiko kutamfanya binadam awe na uwezo huru wa kujiuliza maswali na kutafuta majibu kuhusu Asili,maana na madhumuni ya maisha au uhai katika dunia hii na ulimwengu kwa ujumla. Hapo Mimi naona imani isiyo na mashiko (blind faith ya Atheist)
Kosa kubwa la kimantiki linalowakabili Atheist ni kujidanganya na kidanganya kwamba ukiwa Atheist wewe automatically unakuwa na authority kiasi cha kuchanganya kauli zao kuwa kauli za kisayansi.
Atheist wanafikiri Binadam anatakiwa achague Kati ya Sayansi na Mungu, wakijidanganya kuwa haiwezekani ukawa unaamini Mungu na kuwa Mwanasayansi.
Huo ni moja ya mambo ya kilimbukeni mnooo, historia haijapungukiwa na watu ambao walikuwa ni wacha Mungu wazuri na wakati huo huo sayansi ya kisasa imesimama katika misingi ya sayansi na ugunfuzi wa kisayansi. Mfano mzuri wa Great brain ambazo zilikuwa zinajinasibu na Mungu na kutenda makuu ya sayansi ni pamoja na Newton, Galileo na keppler.
Busara ya binadamu wa kawaida akiamua kutafuta ukweli kuhusu chanzo cha uhai kwa sasa hivi Creation / God world view ndiyo yenye mashiko.
Vingine ni viroja tu. Evolution inszungumzia Mechanism na sio chanzo. Big bang nayo inahangaika humo humo. Lakini ukirudi kwenye neno;
In the beginning God created...
Unapata mashiko,
Moja imeanza na kuonyesha kwamba kulikuwa na mwanzo...

Hongera Sana Mkuu. Umeweka hoja itayowasaidia wengi hata wale ambao wamekaririshwa hakuna Mungu kwa imani tu huku wakijifanya hakuna Mungu yao ni sayantific

They believe in the belief that God does not exists, but they hate to be told that they are believers too.
 

Haujajibu swali...maelezo yako kuhusu kutambua jambo ovu nimekubaliananayo bila tabu kwa sababu umetaja kama makundi matatu ambayo twaweza kujua uovu kupitia makundi hayo,na moja wapo ktk hayo makundi ni kundi la "Imani" hili kundi linabeba hizi dini na imani mbalimbali.

Hivyo mie nimekuelewa vizuri hivyo naomba unijibu swali nililokuuliza.
 

Hizo ni sababu za kupinga uwepo wa mungu wa Mungu ila si ushahidi wa kuthibitisha kutokuwepo kwa Mungu. Unaweza hata ukampinga baba yako mzazi kwa kusema si baba yako mzazi na ukawa na sababu za kusema hivyo ila ukakosa ushahidi(sijui kama umenielewa).

Sasa labda nikuulize unataka ushahidi wa uwepo wa Mungu au unataka majibu ya hizo unazoita contradiction?
 
Hili swali utaliuiza mara ngapi na unataka nikujibu mara ngapi?

Nataka uniambie namba ya mara unazotaka nilijibu ili nilimalize hapahapa.

Halafu, baada ya kulijibu, nikuulize, linahusika vipi na kithibitisha mungu yupo.

Haujajibu hili swali kama lilivyo na kuhusu kuthibitisha uwepo wa mungu,nyie ndiyo wa kuulizwa masuala ya uovu kwa sababu nyie ndiyo mliyoyaleta hapa.
 

Rudia kusoma tena,mie nimerudia kusoma nilichokiandika na naona nilichoandika kinaeleweka kabisa.
 

Hilo tendo la kutoa ushahidi linaitwaje mkuu?
 
Sasa kwa nini kaumba dunia inayoweza kuwa na matetemeko ya ardhi yanayoua watoto wasio na hatia wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao hauna matetemeko hayo?

Mkuu wewe, swali la kitoto namna hii linatolewa na GT tena ajiitae mwanasayansi ?
Kuwepo kwa tetemeko na Umuhimu wake ni vitu ambavyo badala ya kuita Uovu unatakiwa ufanyie utafiti, mimi nafahamu kuna faida za kielolojia za kuwepo kwa tetemeko.
Habari ya watoto kufa kwenye tetemeko sio KOSA LA TETEMEKO, ni uzembe wako wewe ambaye umepeleka watoto wasio na hatia kwenda kufanya makazi kwenye ukanda ambao kuna uwezekano wa kuwepo kwa matetemeko.

Mwanasayansi kweli unaweza kujenga hoja zilizokufa kwa kiwango hiki kweli ?
Hujui kuwa tetemeko linajulikana kuhusiana na mwenendo wa miamba (Plate tectonics) wewe unahusisha na kuita ni EVIL ?
 
Wanaosema mungu yupo hawajathibitisha kwamba yupo.

Na hawajaondoa contradiction ya "the problem of evil".

Umetaja vitu viwili hapo "kuthibitisha mungu na kuondoa contradiction"

Sasa ni wapi wewe umetowa uthibitisho au ushahidi kuwa mungu hakuna ukiacha kueleza hizo unazoita contradiction?
Au kwamba kungekuwa hakuna hizo unazoita contradiction ungekuwa hauna budi kukubali kuwa mungu yupo?
 
Sasa kwa nini kaumba dunia inayoweza kuwa na matetemeko ya ardhi yanayoua watoto wasio na hatia wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao hauna matetemeko hayo?

Unakubali kuwa ni kweli mungu ndiye aliyeumba?
 
Uko low sana mkuu!,umeulizwa mtoto mdogo anayekufa ana hatia gani?,we unajibu et huwez jua mwenye hatia!,poor!

Eti mungu kaona ni wakati muafaka kuwchukua!,aisee!,wewe bado kabisa ndugu

Yapi yalikufanya uache imani yako na kuamua kuwa atheist?
 

Binafsi naamini Mungu yupo na anaweza na kujua yote. Ila pia naamini sio kila kitu kinachotokea kwa binadamu anapanga yeye. Ndio maana huwa siamini kwenye kitu wanaita "fate". Having a will power, kila binadamu anauwezo wa kutengeneza his or her own destiny ingawa kwa namna moja au nyingine, binadamu pia anaweza ku affect destiny ya binadamu mwenzake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…