MNAODAI MUNGU HAYUPO. . .JIBUNI HAYA MASWALI
Ayubu 38
1 Ndipo Bwana akamjibu
Ayubu katika upepo wa
kisulisuli, na kusema,
2 Ni nani huyu atiaye
mashauri giza Kwa
maneno yasiyo na
maarifa?
3 Basi jifunge viuno
kama mwanamume,
Maana nitakuuliza neno,
nawe niambie.
4 Ulikuwa wapi
nilipoiweka misingi ya
nchi? Haya! Sema, kama
ukiwa na ufahamu.
5 Ni nani aliyeamrisha
vipimo vyake, kama
ukijua? Au ni nani
aliyenyosha kamba juu
yake?
6 Misingi yake ilikazwa
juu ya kitu gani? Au ni
nani aliyeliweka jiwe lake
la pembeni,
7 Hapo nyota za asubuhi
zilipoimba pamoja, Na
wana wote wa Mungu
walipopiga kelele kwa
furaha?
8 Au ni nani aliyeifunga
bahari kwa milango,
Hapo ilipofurika kana
kwamba imetoka
tumboni.
9 Nilipolifanya wingu
kuwa vazi lake, Na giza
zito kuwa nguo ya
kuifungia,
10 Nikaiagiza amri
yangu; Nikaiwekea
makomeo na milango,
11 Nikasema, Utafika
mpaka hapa, lakini
hutapita, Na hapa
mawimbi yako
yanyetayo yatazuiliwa?
12 Je! Umeiamuru
asubuhi tangu siku zako
zilipoanza? Umeyajulisha
mapambazuko mahali
pake?
13 Yapate kuishika
miisho ya nchi, Waovu
wakung'utwe wakawe
mbali nayo?
14 Hubadilika mfano wa
udongo chini ya muhuri,
Vitu vyote vinatokea
kama mavazi.
15 Na waovu nuru yao
huzuiliwa isiwafikie, Na
mkono ulioinuka
huvunjika.
16 Je! Umeziingia
chemchemi za bahari, Au
umetembea mahali pa
siri pa vilindi?
17 Je! Umefunuliwa
malango ya mauti, Au
umeyaona malango ya
kuzimu?
18 Umeyafahamu
mapana ya dunia? Haya!
Sema, ikiwa unayajua
hayo yote.
19 Iko wapi njia ya
kuyafikia makao ya nuru?
Na giza pia, mahali pake
ni wapi?
20 Upate kuipeleka hata
mpaka wake, Upate
kuelewa na mapito ya
kuiendea nyumba yake?