Maziku-Winston Smith
JF-Expert Member
- May 17, 2015
- 296
- 168
Umenena vyema, maana hata mimi nilikuwaga mkristo. kutokana na haya maswali nikaona kama sisi Ndio tuliomuumba Mungu kwenye akili zetu.
Hebu jiulize kama shetani yupo atakuwa na dhambi gani wakati Mungu anamuumba alijua kabisa ikifika tarehe fulani atamuasi.
Lakini akamuumba tu! Na kadhalika sisi vivyohivyo kabla ya kuzaliwa anajua kuwa mimi nitampinga. Je? Huyu Mungu burudani yake ni mateso yetu au.
Mungu anaweza yote ila anaheshimu maamuzi unayoyachagua.
Ushahidi wenye kuthibitisha kuwa kweli hakuna Mungu hadi sasa hakuna,mmebaki tu mara mungu hana upendo mara hana uwezo wote sijui kwanini kaumba ulimwengu una maovu? Lakini hamtoi ushahidi wa kutokuwepo kwa Mungu.
Yapi yaliyokuwa yanakufanya useme mungu yupo kabla haujawa atheist?
Halafu cha kushangaza sasa ilikuwa kila nikihoji hivyo wazazi wakawa wananiambia siwezi kuhoji mambo ya Mungu wakati tayari uwezo wa kuhoji ametupa.
huna sababu ya kutetea uwepo wa Mungu kwa kuuponda Ukristo, unaonyesha jinsi ulivyo mbumbumbu wa kujenga hoja.
Wakristo hawaabudu Mungu.
Bali wanaabudu picha ya Mzungu na sanamu yake.
Zaburi 14:1 mpumbavu amesema moyoni mwake hakuna mungu. .
Wakristo hawaabudu Mungu.
Bali wanaabudu picha ya Mzungu na sanamu yake.
Mwanao tu nyumbani akikosea huwa unaheshimu maamuzi yake au unamrekebisha kabla hajaharibikiwa?
anatumia njia nyingi sana kuwaonka watu wasipotee. afurahii mtu mbaya asipotee katika ubaya.
tofauti na wanyama, ametuumba na uhuru wa kuchagua. ukikomaa sana ukaacha mahusia yake hawezi kukuforce kama robot mkuu.
Anasema! Kabla ya kuzaliwa nalikujua, na nilujua njia zako zote.
Hapo anamaanisha kwamba kabla ya kukomaa hadi uache mahusia yake alijua hata kabla hujazaliwa.
Je? UPENDO WAKE MKUU uko wapi??. Maana hapo inaonekana yeye ndio anatuumbia huo ukomavu, kiburi, na machukizo mengine yote alafu akatuadhibu eti!
Huyu Mungu yupo au ni hadithi tu za wanadamu?.
Kwani hiyo zaburi siiliandikwa na mtu kama mimi na wewe? Kwa taarifa yako wewe ndio MPUMBAVU kwa kuamini tu pasipokuuliza.
Ndio maana wengine wamelawitiwa kwa kufata mkumbo kama wewe, kisa tu maandiko yamewaathiri kisaikolojia hata kujijua hamtaki.
Mungu yupo, ila sisi ndi hatumuelewi na opportunist wanatumia hiyo gap kuingiza mafundisho hayo ya kutokuwapo kwa Mungu.
Ulipaswa kujiuliza mswali zaidi ya hapo,
Kwa nini aumbe dunia akijua ataichoma moto?
Kwa nini amauche shetani aje atudanganye asingemuua mojakwa moja na maraika zake?
kwa nini aruhsu watu kama wewe muendelee kuongezeka?
kwa nini aruhusu vita majanga na matatizo?
Mungu hawezi kuacha kufanya chochote eti kwa sababu kitakuja kuwa na madhara. Ni kweli anajua mwanzo na mwisho, Alipojua mwanadamu ataanguka katika dhami aliandaa mpango wa wokovu kabla hata ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu.
Mungu yupo kaka. Na anatupenda wote ha wewe pia. ila kuwa makini moyo wako usije ukashupaa na kukakamaa ukashindwa kuamini ukapotea kabisa. Hata kama watu watachomwa moto hatawasahau.
GOD EXISTS
Nashukuru kwa mchango wako kaka, ila unanipeleka kiimani zaidi. Swali ni je? Kwanini afanye ivo wakati ana upendo wote na uwezo wote?
Kuna maswali mengine Binaadamu hawezi kuyajibu hata awe na elimu namna gani.
Kabla ya kuuliza kazi za Mungu na maamuzi yake hebu jiulize swali ambalo liko karibu yako.
Jiulize KIFO ni NINI?
Kwanini kila kiumbe kilicho hai LAZIMA KIFE?
Au iulize hio Sayansi KIFO ni KITU GANI HASA?
Ukiweza kupata jibu hili Tutaendelea na Darasa.
Hao wanasayansi mnaotegemea watatoa majibu kwa kila kitu wamejaribu Kutafsiri Maana ya kifo zaidi ya Tafsiri 200! Na hakuna mmoja akakubaliana na mwenzake kwa tafsiri hizo.
Sasa huwezi kujaribu kutafuta majibu yanayo mhusu MUNGU asie Onekana Wakati kuna mambo MENGI mno unayo yaona lkn MAJIBU huna.
Nasubiri jibu niendelee na Darasa.
Ahsanta.