Kweli Mungu ni muweza wa yote?



unajua kwenye maswala ya imani huwezi kumbadilisha mtu mwaweza hata pigana, mimi nina imani na imani yangu naona inanisaidia wewe kama huamini baki hivyo hivyo nchi huru hii ndio maana wengine huabudu miti, mizimu na wanaona kwao inatenda kazi. mimi huwa sipendi ubishi hasa kwenye maswala yanayohusisha uwezo na nguvu za Mungu naamini ninachokiamini basi, na wewe baki na imani yako ila usiingilie imani ya wengine wala kuwakwaza wale wanaoamini, usitumie nguvu kubwa ya ushawishi kuwa Mungu hayupo, wewe toa mawazo yako na imani yako ila usiende beyond.
labda kwako wewe unaona Mungu hajatenda kitu kwako una haki ya kuamini unachoamini, ila kwa amabe ameomba Mungu na jambo likatendeka mwache nae aamini kuna Mungu bila kumkwaza.
 
Mbona unaleta hadithi tu kama za zamani unaamamini zamani wanyawa walikuwa wanaonge? je kipindi kile akili bado changa ukiambiwa simba alimuambia swala kuwa leo nakutafuna si ulikuwa unaamini mpaka now kuna watu wanaamini kabisa kuna zombie na vampire kitu ambacho ni editing tyu Hata tusipopinga uwepo wa mungu yeye mwenyewe anajikinza kwann anashindana na shetani ikiwa yeye ni muweza wa yote?? kwann shetani ana mshinda na kuendesha kiumbe chake binadamu???
 
Mungu alimuumba binadamu kwa upendo na akamtofautisha na viumbe wengine wote kwa kumpatia AKILI, UFAHAMU kwa ajili ya kujitambua na kujitofautisha na viumbe wengine kama mijusi, mende na kereng'ende. Hivyo vitendo vya kuvaa mabomu na kujilipua ili kuua watu wengine au kuwafanyia watu wengine mamabo ya ajabu ni ROHO MBAYA NA MATUMIZI MABAYA YA AKILI & UFAHAMU. Hivyo Mungu yupo daima na kila binadamu anamshudia Mungu katika mazingira tofauti kadri anavyotumia akili & ufahamu wake katika maisha.
 
ni swala au suala?
 
Ngoja ni trace then ntakups aya clearly but unakumbuka rutu alikaa uchi mbele za watoto wake weupe walificha nyuso zao kutomuangalia pakikuwepo na mtoto mweusi ambae alitazama utupu wa babake na alilaaniwa (Hadithi hizi za vitabu vya mungu)

Sasa km Weusi ni kitu kibaya
Vipi usimlaumi Mungu kwa kuweka asilimia 70 ya World Minerals kwenye Ardhi za watu weusi?

Tumia akili kijana.
 
Ntarudi hapa ngoja nikusanye nguvu kidogo
 
shetan hamzidi mungu...ila wew ndio unazidiwa na shetana kwa kutokutaka kuwa karibu na mungu
Kwanini mungu asinisogeze kwake hali ya kuwa yeye ni muweza wa yote??
 
Mimi nasema kwa atheist wote kama hakuna mungu pale wakati wa kifo watumie sayansi yao kuzuia kifo ili wasife.

Pia watengeneze japo mende kwa ilimu zao na akili zao kama wao wasema hakuna mungu.

Pia usiku waufanye mchana kwa kutumia akili zao ili watuthibitishie kuwa hapana Mungu

Katika reply zenu sitaki habari za nature ambazo hazina maelezo ya kutosha.
Na km ataandika nature basi naomba nifafanuliwe neno nature km ifuatavyo.
Kwann nature iwe nature
Nature ilianza wapi
Hivi nature vipi inajipa amri wenyewe pasi na kuamrishwa
 
Mwenye upendo wote na uwezo wote anaweza kuachia anaowapenda wapatwe na mabaya?

Kwann asiwaachiye wapatwe na huo ubaya ilihali wao hawataki kupendwa?

Kwani wangapi walikuwa marafiki zako na kwa muda huu ni maadui zako? Jee huwapendi hao?

Baba anapokerwa na mtoto wake humuadhibu kwa kumpiga viboko kwa sababu hiyo utasema baba hampendi mwanawe?

Na ukisema baba hampendi mwanawe kwanini huchukia pindi mwanawe akipata adhabu kutoka kwa mengine?

Hivi mwanafunzi anapofeli katika masomo ya shule hufelishwa na mwalim?

Wakati mualimu anasahihishia daftari la mwanafunzi alikuwa hana uwezo wa kueka raiti hata kwenye makosa?

Jee kwa mwalim kutoweka raiti hatakuwa si muadilifu?

Basi jueni mola wangu ni mueza juu ya kila kitu.
Basi jueni mola wangu anawapenda waja wake na anawachukia sana wenye kukufuru

Basi jueni mola wangu anasikia nae anaona wala hakuna kitu chenye kufanana naye.

Basi jueni mola wangu amejiepusha mbali na kudhulumu na wala hawapendi madhalimu.

Kumbukeni watu wema ndio vipenzi vya mola wangu na watu wa wabaya ni vipenzi vya shetani.


Kumbukeni shetani anawaongoza katika giza na shida lakini mola anawaita kwenye uongofu na rehema

Muabuduni bwana wa mbingu na ardhi aliyefanya kuwa maji yenye kuchupa ndiyo chanzo chenu.

Muogopeni sana bwana wa viumbe vyote aliewapa neema ya kuona na kusikia.

Muogopeni yeye aliyetia huruma katika nyoyo za mama zenu kuwaleeni nyinyi mpaka mkawa watu wazima.

Mungu awaongoze na awasamehe madhambi yenu na anisamehe mimi kwa rehema zake pindi akitaka.

Enyi watu jisalimisheni kwa mola wangu na ndiye mola wenu huenda akawasamehe na akakufanyieni wepesi katika maisha yenu.

Mwiteni Allah au mwiteni Rahmani.vyovyote vile mutavo mwita basi yeye ana majina mazuri
 
Mungu yupo arawa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…