Kweli Mungu ni muweza wa yote?

Kweli Mungu ni muweza wa yote?

Mkuu kuamini mungu yupo hakungarimu chochote usipomkuta?? Je huo muda unaopoteza kumuabudu je hizo pesa unaowapa Hao servant wake Je hio akili yako unavyoilaza kwa kila jambo ukitegemea support from him? Mangapi umeshindwa kupambanua na ukamuachia mungu ambae haja leta positive effect kwa hilo jambo ulilomuachia Yani unataka tu useme kuabudu hakugharimu kitu khaa really u kidding me kwa taarifa yako unaona somalia ilivyo poor sasa wale wanamjua mungu hewa haswaa ndo mana bongo zao zimelala kila jambo ni kumuachia tu mtu ambae hae exist physically


unajua kwenye maswala ya imani huwezi kumbadilisha mtu mwaweza hata pigana, mimi nina imani na imani yangu naona inanisaidia wewe kama huamini baki hivyo hivyo nchi huru hii ndio maana wengine huabudu miti, mizimu na wanaona kwao inatenda kazi. mimi huwa sipendi ubishi hasa kwenye maswala yanayohusisha uwezo na nguvu za Mungu naamini ninachokiamini basi, na wewe baki na imani yako ila usiingilie imani ya wengine wala kuwakwaza wale wanaoamini, usitumie nguvu kubwa ya ushawishi kuwa Mungu hayupo, wewe toa mawazo yako na imani yako ila usiende beyond.
labda kwako wewe unaona Mungu hajatenda kitu kwako una haki ya kuamini unachoamini, ila kwa amabe ameomba Mungu na jambo likatendeka mwache nae aamini kuna Mungu bila kumkwaza.
 
kuna viumbe wa ajabu sana, yaani kwa nguvu zako zote umeshupaza shingo kuwa Mungu Hayupo! Kisa? you believe in science and the scientists! you are betting the only life you have, kwa mtu mwenye hekima mada kama hizi ni bora ukae kimya, kuliko kujifanya wewe sijui ni adheist and you don't believe in the existence of your creator, ndio hapo na amini kwamba shetani hufanya kazi kwa kupitia watu kama ambavyo mungu pia hufanya, so nimegundua kwamba unaweza kubishana na kiumbe humu mpaka siku inaisha kang'ang'ania tuu Mungu hayupoo, Kumbe the devil himself is at work, you guys you are possessed with demons and before you know it you will find yourself spending eternity in hell.. sishangai kuona wapinga kristo maana kuna ma-agenti wa kuzimu kila mahali, hata humu jf wamejaa na elimu zao za giza.. anaanza na elimu ya kujitambua anakupeleka kwenye the so called 'meditation' atarukia kweye kuongea na roho za wafu, na kufanya Astro Projection Mpaka Unakua Mchawi Huru and trust kuna stage utafika hutatamani kuacha
Mbona unaleta hadithi tu kama za zamani unaamamini zamani wanyawa walikuwa wanaonge? je kipindi kile akili bado changa ukiambiwa simba alimuambia swala kuwa leo nakutafuna si ulikuwa unaamini mpaka now kuna watu wanaamini kabisa kuna zombie na vampire kitu ambacho ni editing tyu Hata tusipopinga uwepo wa mungu yeye mwenyewe anajikinza kwann anashindana na shetani ikiwa yeye ni muweza wa yote?? kwann shetani ana mshinda na kuendesha kiumbe chake binadamu???
 
Kuna hili swala la kusema Mungu kashatupangia kesho yetu ipoje pia anajua wewe utafanya nini kesho kwa mantiki hiyo, Mungu ni muweza wa yote hata sisi atheist kashapanga tusikubali uwepo wake kama hajapanga na hivi tunafanyavyo tunajiamulia, basi tumtoe katika kundi la mpangaji wa yote. Hii ina maana hajui kesho yangu.Naeleweka hivi! Hoja ya uwepo wa mungu inatafisiriwa kama moja ya harakati za mwanadamu aliyekataa tamaa ambae anajipa matumaini kwa nadharia hii kuwa itamsaidia...Mungu mwenye upendo iweje aruhusu watu sio na hatia kuuwawa mungu mwenye upendo anawambia viumbe wake wawaue wengine ili waione pepo?? Mapungufu ya science kueleza asili yetu wala hayamuumbi mungu au kumfanya awepo
Mungu alimuumba binadamu kwa upendo na akamtofautisha na viumbe wengine wote kwa kumpatia AKILI, UFAHAMU kwa ajili ya kujitambua na kujitofautisha na viumbe wengine kama mijusi, mende na kereng'ende. Hivyo vitendo vya kuvaa mabomu na kujilipua ili kuua watu wengine au kuwafanyia watu wengine mamabo ya ajabu ni ROHO MBAYA NA MATUMIZI MABAYA YA AKILI & UFAHAMU. Hivyo Mungu yupo daima na kila binadamu anamshudia Mungu katika mazingira tofauti kadri anavyotumia akili & ufahamu wake katika maisha.
 
Kuna hili swala la kusema Mungu kashatupangia kesho yetu ipoje pia anajua wewe utafanya nini kesho kwa mantiki hiyo, Mungu ni muweza wa yote hata sisi atheist kashapanga tusikubali uwepo wake kama hajapanga na hivi tunafanyavyo tunajiamulia, basi tumtoe katika kundi la mpangaji wa yote. Hii ina maana hajui kesho yangu.

Naeleweka hivi! Hoja ya uwepo wa mungu inatafisiriwa kama moja ya harakati za mwanadamu aliyekataa tamaa ambae anajipa matumaini kwa nadharia hii kuwa itamsaidia...Mungu mwenye upendo iweje aruhusu watu sio na hatia kuuwawa mungu mwenye upendo anawambia viumbe wake wawaue wengine ili waione pepo?? Mapungufu ya science kueleza asili yetu wala hayamuumbi mungu au kumfanya awepo
ni swala au suala?
 
Ngoja ni trace then ntakups aya clearly but unakumbuka rutu alikaa uchi mbele za watoto wake weupe walificha nyuso zao kutomuangalia pakikuwepo na mtoto mweusi ambae alitazama utupu wa babake na alilaaniwa (Hadithi hizi za vitabu vya mungu)

Sasa km Weusi ni kitu kibaya
Vipi usimlaumi Mungu kwa kuweka asilimia 70 ya World Minerals kwenye Ardhi za watu weusi?

Tumia akili kijana.
 
shetan hamzidi mungu...ila wew ndio unazidiwa na shetana kwa kutokutaka kuwa karibu na mungu
Kwanini mungu asinisogeze kwake hali ya kuwa yeye ni muweza wa yote??
 
Mimi nasema kwa atheist wote kama hakuna mungu pale wakati wa kifo watumie sayansi yao kuzuia kifo ili wasife.

Pia watengeneze japo mende kwa ilimu zao na akili zao kama wao wasema hakuna mungu.

Pia usiku waufanye mchana kwa kutumia akili zao ili watuthibitishie kuwa hapana Mungu

Katika reply zenu sitaki habari za nature ambazo hazina maelezo ya kutosha.
Na km ataandika nature basi naomba nifafanuliwe neno nature km ifuatavyo.
Kwann nature iwe nature
Nature ilianza wapi
Hivi nature vipi inajipa amri wenyewe pasi na kuamrishwa
 
Mwenye upendo wote na uwezo wote anaweza kuachia anaowapenda wapatwe na mabaya?

Kwann asiwaachiye wapatwe na huo ubaya ilihali wao hawataki kupendwa?

Kwani wangapi walikuwa marafiki zako na kwa muda huu ni maadui zako? Jee huwapendi hao?

Baba anapokerwa na mtoto wake humuadhibu kwa kumpiga viboko kwa sababu hiyo utasema baba hampendi mwanawe?

Na ukisema baba hampendi mwanawe kwanini huchukia pindi mwanawe akipata adhabu kutoka kwa mengine?

Hivi mwanafunzi anapofeli katika masomo ya shule hufelishwa na mwalim?

Wakati mualimu anasahihishia daftari la mwanafunzi alikuwa hana uwezo wa kueka raiti hata kwenye makosa?

Jee kwa mwalim kutoweka raiti hatakuwa si muadilifu?

Basi jueni mola wangu ni mueza juu ya kila kitu.
Basi jueni mola wangu anawapenda waja wake na anawachukia sana wenye kukufuru

Basi jueni mola wangu anasikia nae anaona wala hakuna kitu chenye kufanana naye.

Basi jueni mola wangu amejiepusha mbali na kudhulumu na wala hawapendi madhalimu.

Kumbukeni watu wema ndio vipenzi vya mola wangu na watu wa wabaya ni vipenzi vya shetani.


Kumbukeni shetani anawaongoza katika giza na shida lakini mola anawaita kwenye uongofu na rehema

Muabuduni bwana wa mbingu na ardhi aliyefanya kuwa maji yenye kuchupa ndiyo chanzo chenu.

Muogopeni sana bwana wa viumbe vyote aliewapa neema ya kuona na kusikia.

Muogopeni yeye aliyetia huruma katika nyoyo za mama zenu kuwaleeni nyinyi mpaka mkawa watu wazima.

Mungu awaongoze na awasamehe madhambi yenu na anisamehe mimi kwa rehema zake pindi akitaka.

Enyi watu jisalimisheni kwa mola wangu na ndiye mola wenu huenda akawasamehe na akakufanyieni wepesi katika maisha yenu.

Mwiteni Allah au mwiteni Rahmani.vyovyote vile mutavo mwita basi yeye ana majina mazuri
 
Kuna hili swala la kusema Mungu kashatupangia kesho yetu ipoje pia anajua wewe utafanya nini kesho kwa mantiki hiyo, Mungu ni muweza wa yote hata sisi atheist kashapanga tusikubali uwepo wake kama hajapanga na hivi tunafanyavyo tunajiamulia, basi tumtoe katika kundi la mpangaji wa yote. Hii ina maana hajui kesho yangu.

Naeleweka hivi! Hoja ya uwepo wa mungu inatafisiriwa kama moja ya harakati za mwanadamu aliyekataa tamaa ambae anajipa matumaini kwa nadharia hii kuwa itamsaidia...Mungu mwenye upendo iweje aruhusu watu sio na hatia kuuwawa mungu mwenye upendo anawambia viumbe wake wawaue wengine ili waione pepo?? Mapungufu ya science kueleza asili yetu wala hayamuumbi mungu au kumfanya awepo
Mungu yupo arawa!!
 
Back
Top Bottom