Kweli tunapiga vita ugaidi au ni vita dhidi ya uislam?

Kweli tunapiga vita ugaidi au ni vita dhidi ya uislam?

Status
Not open for further replies.
vile vichanga vinavyouliwa na drone huvionagi ila vichanga vya westgate!!

Kwani mimi nimekuambia naunga Mkono mauaji ya Drones? tatizo lenu sijui humo Miswikitini mnamezeshwa sumu gani, mimi siungi mkono mauaji ya Drones ila nimejikita kwenye huuu ushenzi wa Mauaji yanayofanywa na washenzi fulani waliodanganywa kwamba wafanye hivyo maana Mnyaazi Mungu atawabariki. Na kuna kitu nimeki-notes kwa watu wenye vichwa vya panzi kwamba marekani wakifanya kitu fulani basi hiyo inamaanisha wakristo ndo wapo nyuma ya pazia, na ili ku-revenge mtu anaenda kulipua ubarozi wa Marekani ili waliomo ndani wafe bila kujari wame-play role gani katika madai yao hayo
.
 
Mimi ni Muislam na nipo Kilindi kulikotokea hayo yanayosemwa. Kiukweli walioshambuliwa na polisi SI WAISLAM kwa matendo yao. KUFUNDISHA WATOTO KUUA, KUCHUKIA MAKUNDI FULANI YA JAMII, KUNYANG'ANYA ARDHI WATU, KUUA WATU HADHARANI KAMA KULE LULAGO, KUKATA WATU MIKONO, KUENDESHA MAFUNZO YA KIJESHI, KUJITENGA MBALI NA JAMII, KUTOTII VIONGOZI WA SERIKALI ZA VIJIJI, KATA HADI TAIFA, KUINGIZA WAGENI TOKA NCHI ZA NJE BILA UTARATIBU, KUFUNDISHA CHUKI KWA WASIO WAAMINI. Nk Huo sio uislam kwani hayo si msfundisho ya dini yetu. Dini yetu inatufundisha UPENDO NA AMANI. KUTAMBUA NA KUHESHIMU WASIO WAISLAM Nk.
mmh?!mmeanza kuja kwa mbinu ingine,kwani hapa ni mahakamani jama,naona mmeshupaa hadi mmeanza kutengeeza username special kwa hii thread,kha!.

Haya unadai uko kilindi,ulikuwa wapi kuclarify mambo karibu miezi mitatu hili swala liko hapa?.
Weka picha tuone kama kweli uko kilindi?
 
Mimi ni Muislam na nipo Kilindi kulikotokea hayo yanayosemwa. Kiukweli walioshambuliwa na polisi SI WAISLAM kwa matendo yao. KUFUNDISHA WATOTO KUUA, KUCHUKIA MAKUNDI FULANI YA JAMII, KUNYANG'ANYA ARDHI WATU, KUUA WATU HADHARANI KAMA KULE LULAGO, KUKATA WATU MIKONO, KUENDESHA MAFUNZO YA KIJESHI, KUJITENGA MBALI NA JAMII, KUTOTII VIONGOZI WA SERIKALI ZA VIJIJI, KATA HADI TAIFA, KUINGIZA WAGENI TOKA NCHI ZA NJE BILA UTARATIBU, KUFUNDISHA CHUKI KWA WASIO WAAMINI. Nk Huo sio uislam kwani hayo si msfundisho ya dini yetu. Dini yetu inatufundisha UPENDO NA AMANI. KUTAMBUA NA KUHESHIMU WASIO WAISLAM Nk.

Umechomekea upande gani ama pana mtu kakutuma maana?

Samahani kama nimetumia maneno machafu maana sijakuona tangu mwanzoni mwa uzi au nipe muda nipitie Post moja baada ya nyengine ili nione mchango wako, au nisaidie wewe mwenye je, wakati unaingia katika uzi huu umepitia kila post na ndo ukaamua kutoa ulicho nacho?

Na mwisho kama hivyo ndivyo na watakakutuaminisha hayo uloyaandika hapo, kama kweli uu-mungwana ilipendeza ututhibitishie hata kwa majina ya kuwa mimi XXX.... bin YYY.... bin ZZZ....... mkazi au mwenyeji wa pahala hapo japo sipo kwa sasa hayo yaloletwa na mleta UZI ni uzushi mtupu maana uhalisia wa mambo ni ..........

Hata kwa jina moja tu ingelitutosha kuliko porojo kama hizo

Ni ushauri tu najaribu kukugeiya,
Waezababaika na ukataka tena anza malumbano yasofaida nami wala jukwaa, kuwa ati MBONA WEWE mwenyewe hujataja lako jina?!

Nami ntakujibu .........kama itahitajika kukugeiya hayo majibu.

Ahsanta.
 
Kwani mimi nimekuambia naunga Mkono mauaji ya Drones? tatizo lenu sijui humo Miswikitini mnamezeshwa sumu gani, mimi siungi mkono mauaji ya Drones ila nimejikita kwenye huuu ushenzi wa Mauaji yanayofanywa na washenzi fulani waliodanganywa kwamba wafanye hivyo maana Mnyaazi Mungu atawabariki. Na kuna kitu nimeki-notes kwa watu wenye vichwa vya panzi kwamba marekani wakifanya kitu fulani basi hiyo inamaanisha wakristo ndo wapo nyuma ya pazia, na ili ku-revenge mtu anaenda kulipua ubarozi wa Marekani ili waliomo ndani wafe bila kujari wame-play role gani katika madai yao hayo
.
yataka uwe na ushahidi kuwa wale jamaa wameua kwa kuwa wamefundishwa na nani sijui.

Reliable source iliyopo hapa ni gazeti inayosema kuwa ushuru ndo chanzo...wewe unasema wamefundishwa.
Weka ushahidi.
 
Kwani mimi nimekuambia naunga Mkono mauaji ya Drones? tatizo lenu sijui humo Miswikitini mnamezeshwa sumu gani, mimi siungi mkono mauaji ya Drones ila nimejikita kwenye huuu ushenzi wa Mauaji yanayofanywa na washenzi fulani waliodanganywa kwamba wafanye hivyo maana Mnyaazi Mungu atawabariki. Na kuna kitu nimeki-notes kwa watu wenye vichwa vya panzi kwamba marekani wakifanya kitu fulani basi hiyo inamaanisha wakristo ndo wapo nyuma ya pazia, na ili ku-revenge mtu anaenda kulipua ubarozi wa Marekani ili waliomo ndani wafe bila kujari wame-play role gani katika madai yao hayo
.

Ni kweli maana wapo wengine wana vichwa vya nzi huamini kuwa waarabu wakifanya mauaji yyte ni waislamu,na wanaamini waarabu wote ni waislamu,au huko iraq,somali,afghanistani na pakistani pakitokea mauaji mbio mnaanza ujinga eti waislam hao,someni kitabu chao Qur an kisha mtajua kinasemaje khs wauaji au wanaodhulumu ,sio kuropokwa km umemeza cf,sijui huko makanisani mnamezeshwa sumu gani,west gate walishasema wenyewe kuwa wamefanya mauaji kwa sababu wakenya walipeleka MAJESHI YAO SOMALIA NA KUWAUA NDUGU ZAO HUKO,na ndio maana wameamua kulipiza,sasa wewe nani alikwambia kwamba walipoenda kuua west gate wameambiwa mnaazi mungu atawabariki??ulikuwa nao wakati wanapanga mikakati ya uvamizi??ndio sumu mnazolishwa makanisani ndugu yangu,west gate haihusiani kabisa na masuala ya dini na tayari wenyewe wakenya walishajua hilo,wewe bado una mfumo kristo kwenye kichwa chako,wacha fitna na unafiki,
 
Ok labda hapo nimechemsha, ehee unajua Alishabab ni waislam? unajua kwamba pale Westgate kwa mtu aliyehojiwa vizuri nakuonekana ni Muislam alinusurika? Hivi unaweza kunikumbusha ni nini maana ya neno Alshabab?
 
Duh! Mada imepamba moto!

Huku majibu ya msingi hayajibiwi!
 
Hakukua na mda wa kuhojiwa vizuri,ni maneno tu,ukumbuke kuna waislam pia wamekufa westgate.
Tena ukumbuke kwamba mwenye jengo la westgate na yule mwenye jengo la worldtrade centre lilogongwa ndege wote ni wayahudi.
Mbaya zaidi wote wawili ni business partiner.
So ule ni uvumi tu kwamba watu walikua wanahojiwa dini.
 
HABRUHI YA NIPASHE KUTOKA KWA MAJERUHI NA MASHUHUDA ILIKUA KAMA IFIATAVO...

25th October 13
Wananchi waasi

Lulu George
Askari mgambo wa kijiji cha Lwande Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, Salum Mgonje, ameuawa kwa kucharangwa mapanga na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha wilayani hapa, Inspekta Lusekelo Edward, kujeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi baada ya kuibuka vurugu kubwa kijijini hapo.

Vurugu hizo zinadaiwa kusababishwa na kundi la watu ambao walikuwa wakipinga kitendo cha mwenzao kulipishwa ushuru wa ununuzi wa hiliki na serikali ya kijiji.
Kufuatia vurugu hizo, askari kadhaa wakiongozwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kilindi, Inspekta Edward, walikwenda katika kijiji hicho kwa lengo la kuwakamata watu waliohusika na mauaji ya askari mgambo, na ndipo alipopigwa risasi tumboni na mkononi.

Inspekta Edward akizungumza na NIPASHE jana katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo, alikolazwa kwa matibabu, alisema alipigwa risasi alipofika katika Msikiti wa Answaar Suna uliopo kwenye eneo la Kibirashi wilayani Kilindi muda mfupi baada ya kuwatangazia watu hao ambao baadhi yao wanadaiwa kuwa waumini wa msikiti huo kuwa wako chini ya ulinzi.

Alisema chanzo cha tukio hilo ni kutokana na vurugu zilizotokea Oktoba 22, mwaka huu saa 6:00 mchana, baada ya waumini hao kutakiwa kulipa ushuru wa mazao waliyonunua, lakini waligoma na kusema kuwa ni kinyume cha sheria za dini yao.

Alisema kutokana na hali hiyo, watu hao walianzisha vurugu na kusababisha kifo cha mgambo huyo kwa kumshambulia kwa mapanga.
Hali hiyo iliwalazimisha polisi kuwakamata viongozi wao wawili na kusababisha wengine kuandamana kupinga hatua hiyo.

“Baada ya vurugu hizo ambazo zilisababisha kifo cha mgambo, ndipo tulipoamua kuwafuata waumini hawa kwenye msikiti wao, tulipofika pale walikuwa wakitoka na ndipo tulipowatangazia kuwa wapo chini ya ulinzi. Cha kushangaza walirudi na bunduki mkononi na kuanza kuwafyatulia askari risasi ovyo,” alisema Edward.

Alisema pamoja na kushambuliwa na waumini hao, hadi kufikia juzi watu watatu walikuwa wamekamatwa na kwamba msako unaendelea.

Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Selemani Liwowa, alisema chanzo cha mapigano hayo ni mfanyabiashara mmoja ambaye jina lake halijafahamika, mkazi wa kijiji cha Lulago, Kata ya Lwande alipokwenda kijiji cha Lwande kununua hiliki na kukaidi kulipa ushuru wa mazao.

Alifafanua kuwa mfanyabiashara huyo baada ya kukataa kulipa ushuru huo, ndipo askari mgambo (marehemu), alipokwenda kumtia msukosuko ili alipe kama taratibu na sheria za kijiji zinavyoelekeza.

Liwowa alisema baada ya kutokea mabishano makubwa baina ya mgambo na wafanyabiashara, ndipo wenzake walipoingilia suala hilo kwa kuanza kumshambulia kwa mapanga mgambo huyo hadi kusababisha kifo chake.

Aliongeza kuwa taarifa za mauaji ya mgambo zilipofika kituo cha polisi, ilimlazimu Mkuu wa Kituo kuongoza kikosi cha askari kilichokwenda kijiji cha Lwande kwa ajili ya kuwasaka waliohusika na mauaji hayo na ndipo lilipojitokeza kundi la watu wenye silaha na kuanzisha mapigano dhidi ya askari hao.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Juma Ndaki, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa polisi inaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo halisi cha vurugu hizo.

Kamanda Ndaki alisema kundi hilo lilianzisha vurugu baada ya kuona wenzao wamekamatwa na kukimbilia msituni na kwamba msako mkali unaendelea ili kuwatia nguvuni.

“Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constatine Massawe, yupo eneo la tukio kwa ajili ya kuona hali halisi ilivyo na operesheni maalum ya kuwasaka watu hao imeanza kutekelezwa,” alisema Kamanda Ndaki.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo, Dk. Jumanne Karia, alisema majeruhi huyo, Mkuu wa Kituo cha Polisi alipokelewa hospitalini hapo juzi saa 10:30 usiku akitokea wilayani Kilindi.

Dk. Kariya alisema hali yake kwa sasa inaanza kuimarika na kwamba utaratibu wa kumwondoa risasi moja iliyopo tumboni unaendelea.

Tukio hilo limetokea Kilindi wakati kukiwa na taarifa za tukio linalofanana na hilo kutokea katika Wilaya ya Lushoto ambako Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wilayani humo (OCCID), Ufoo Maanga, alicharangwa mapanga na wananchi baada ya askari kwenda kumkamata mtuhumiwa wa mgogoro wa ardhi katika kijiji cha Viti, Kata ya Shume wilayani Lushoto.

NIPASHE

Utaona vurugu hizi ni kama ilivo tajwa katika habari hiii. LAKINI pia usome habari kama ilivomkariri juu polisi majeruhi ni kuwa baada ya vurugu zile za wafanya biashara walikwenda msikitini !!!!! kuwataka waumini wajisaliimishe...
tuseme ukweli polisi walivurunda na kukitia adabu kijiji kizima na wanawake na watoto ...na ili kuficha ouvu wao basi wakatangaza wanapambana na magaidi wapo msikitini na lashabaab.....
waislam ndio wamekua punching bag na kichaka cha uovu

lakini kuna masuala tujiulize kuhusu hili:

  • kwanini polisi walizuia waandishi kufika kule kujua kinachoendelea?
  • masheikh wa mJINI Tanga walipopata taarifa hizi walikutana na kutaka kwenda kujua kina cho jiri lakini hawakukubaliwa
  • sheikh chambuso na wenzake wanao kaa mjini Tanga walifika kuwaona majeruhi hospital kwa nini wakamatwe na kusingiziwa?
  • kwa nini waislam wa Tanga mjini kwa muda wa wiki mbili walikua wakizingirwa siku za ijumaa misikitini?
  • polisi walikua wanaficha nini?
kuna haja ya kuunda tume huru kulifanyia uchunguzi jambo hili....

Jamani tusitoke nje ya mada mbali ya bandiko la Mohamed Said, tutumie rejea na hii hapa kuitafuta haki na dhuluma!
 
Ok labda hapo nimechemsha, ehee unajua Alishabab ni waislam? unajua kwamba pale Westgate kwa mtu aliyehojiwa vizuri nakuonekana ni Muislam alinusurika? Hivi unaweza kunikumbusha ni nini maana ya neno Alshabab?

Skia ndugu yangu,inamana mkiristo akilawiti na kujisifia hadharani ndio mafunzo ya dini yake kulawitiana??
Sasa nataka nikujibu,tatizo lenu wengi sana mkiona neno lolote la kiarabu mnajua la kiislamu,bila kutambua kuwa kiarabu ni lugha wapo waislam na wakiristo na wasio na dini pia,nadhanibpia biblia hd leo ingekuwa haijabadilishwa imeachwa kwa lugha ileile ya kiebrania ambayo baadhi ya lafudhi zao ni za kiarabu msingeiamini.
Sasa nakujibu maana ya ALSHABAAB, hili ni neno la kiarabu lenye maana ya KIJANA MSHUPAVU,MWENYE NGUVU,NA ANAEJIAMINI ASIEOGOPA.ni sawa na neno jengine la kiarabu lijulikanalo kwa jina la RIJALI,hili maana yake ni mwanamme mwenye nguvu za kiume,na laiti neno hili pia lingetumiwa na vikundi hv watu wangeanza ooh waislam bila kujua maana yake,sawa na wewe kuongea kitu kwa kiluga,haihusiani na dini wala dini haiathiriki kwa lugha ya mtu,pia kuna kikundi chengine sisi tunakitambua kwa jina la bokoharamu,lakini uhalisia wake ni BOOK HARAM,wakimaanisha kuwa mtoto wa kike hatakiwi kusoma,ni haramu kwake kutafuta elimu,lkn je uislam unasemaje khs kusoma kwa wanawake?? Qur an inasema KUTAFUTA ELIMU NI LAZIMA KWA WAISLAM WANAUME NA WANAWAKE,sasa jiulize hao bokoharamu wanafuata dini gani?? Au matakwa tu ya makabila yao nchini mwao??km yalivyo baadhi ya makabila hapa nchini kuwaweka wanawake ni watu duni wasiostahiki baadhi ya mambo,lkn sivyo dini inavyosema,je hayo ni waislam pia??
Sasa hapo uislamu uko wapi? Kuhusu suala la westgate kunusurika wamenusurika hata wakiristo,maana yupo yule mdada aliesindikizwa na gaidi alieshika silaha hd mlangoni na akatoka hakuwa muislam na anaitwa pascalia michael,sasa msiwe mnaropokwa msiyoyajua ila ulizeni kwanza,tatizo kubwa lilojitokeza ni kwamba asilimia 100% ya wasomalia ni waislam,jiulize pia wasomali wenyewe kwa wenyewe wanapigana na kuuana hd leo je wanaowaua ni wakiristo??wakati somali waislam watupu,kwa hiyo hv vikundi vinapigana wana mambo yao binafsi lkn sio dini eti imewatuma,vilianza vikundi baada ya kuuawa rais wao Siad Baree ndipo mapigano na uhalifu ukaanza km walivyopigana watusi na wahutu.
Qur an imekataza kuua nafsi isiyokuwa na hatia,naomba muisome hii qur an km waislam wanavyoisoma biblia,msikubali kuambiwa makanisani kuwa aya za shetani,hebu fungukeni muiangalie hasa ipi aya ya shetani??kuambiwa usiibe,usiue na usidhulumu,usizini na usiutoe uhai wa mwenzio ndio aya za shetani??someni muone sio kusema msiyoyajua hapana hata sehemu moja ktk qur an inayoamrisha shari au mauaji.
 
Usinishawishi nirudi kwenye Topic wakati wewe upo nje ya Topic ndiyo haya haya nimetoka kuyaandika mda si mrefu kwamba unafundisha hiki Mswikitin alafu wewe huonyeshi kwa vitendo, unafundisha vijana wajitoe mhanga wakati wewe unajiwekea mipango yako ya maisha ya baadaye na familia yako, hebu niambie Umedai Wachungwaji wanadai sadaka then wanawaambia waumini wao wamesamahewa Dhambi zao... Sasa nakuhoji je hili swala limewahi kusababisha mauaji ya watu wakiwemo watoto na vikongwe? nashangaa sana mimi nimejikita katika kuzishambulia hizi Imani za kishenzi kwa kusababisha uharifu wa mauaji na ndiyo maana zinahusishwa na Magaidi duniani kama wanavyo kiri Alshabab, Alqaeda na makundi zaidi ya 200 ya kigaidi yote yanasema yanapigania dini ya Mnyaaazi Mungu, haya tuanmini kweli huyo Mnyaaz Mungu anapiganiwa, je vitoto vichanga vilivyokufa Westgeti na kwingineko vimemkosea nini Mnyaaaz Mungu? Kama siyo ushetani ni nini?

Kafiri ukitaka kumuelekeza.mpaka aelewe sharti moja muhimu ni.lazima akaoge kwanza!

Sasa mkuu hebu fanya hivyo mi nakisubiri.

La sivyo hapa tutakesha! Kunielewa huwezi.

Fanya fasta mara moja kabla uzi haujachafuka!
 
Na fursa pekee ya kueleweshwa ni hii hapa Jamvini ili kama unanipotosha kila mtu aone na aku-challenge nijuavyo mimi watu wengi wamekuwa wanapotoshwa kwenye vinyumba uchwara vya ibada ibada za kishetani mpaka inafika mahala vijana wanaamini na wanafikia hatua ya kujitoa Mhanga kupigania hizi imani potofu kabisa, haiwezekani unamshawishi mtoto wa mwenzio akajiue kwa ajiri ya Imani eti mwisho wa siku ataenda peponi as if hao viongozi wa hizo Imani hawataki kwenda peponi kwanini wasijitoe wao, wanawapotosha watoto wa watu wanakufa huku wao wakiendelea kutwanga Mvinyo na nguruwe rost duniani, Ninaamini kabisa hapa duniani kusingekuwa na Imani za kishenzi kama hizi, dunia ingekuwa salama sana

Maneno ya Hekima sana haya.
 
Mimi ni Muislam na nipo Kilindi kulikotokea hayo yanayosemwa. Kiukweli walioshambuliwa na polisi SI WAISLAM kwa matendo yao. KUFUNDISHA WATOTO KUUA, KUCHUKIA MAKUNDI FULANI YA JAMII, KUNYANG'ANYA ARDHI WATU, KUUA WATU HADHARANI KAMA KULE LULAGO, KUKATA WATU MIKONO, KUENDESHA MAFUNZO YA KIJESHI, KUJITENGA MBALI NA JAMII, KUTOTII VIONGOZI WA SERIKALI ZA VIJIJI, KATA HADI TAIFA, KUINGIZA WAGENI TOKA NCHI ZA NJE BILA UTARATIBU, KUFUNDISHA CHUKI KWA WASIO WAAMINI. Nk Huo sio uislam kwani hayo si msfundisho ya dini yetu. Dini yetu inatufundisha UPENDO NA AMANI. KUTAMBUA NA KUHESHIMU WASIO WAISLAM Nk.

Nimependa sana maelezo yako.Waislamu wote wangekuwa kama wewe tungeungana kutambua changamoto zinazotukabili kama Taifa.
 
Skia ndugu yangu,inamana mkiristo akilawiti na kujisifia hadharani ndio mafunzo ya dini yake kulawitiana??
Sasa nataka nikujibu,tatizo lenu wengi sana mkiona neno lolote la kiarabu mnajua la kiislamu,bila kutambua kuwa kiarabu ni lugha wapo waislam na wakiristo na wasio na dini pia,nadhanibpia biblia hd leo ingekuwa haijabadilishwa imeachwa kwa lugha ileile ya kiebrania ambayo baadhi ya lafudhi zao ni za kiarabu msingeiamini.
Sasa nakujibu maana ya ALSHABAAB, hili ni neno la kiarabu lenye maana ya KIJANA MSHUPAVU,MWENYE NGUVU,NA ANAEJIAMINI ASIEOGOPA.ni sawa na neno jengine la kiarabu lijulikanalo kwa jina la RIJALI,hili maana yake ni mwanamme mwenye nguvu za kiume,na laiti neno hili pia lingetumiwa na vikundi hv watu wangeanza ooh waislam bila kujua maana yake,sawa na wewe kuongea kitu kwa kiluga,haihusiani na dini wala dini haiathiriki kwa lugha ya mtu,pia kuna kikundi chengine sisi tunakitambua kwa jina la bokoharamu,lakini uhalisia wake ni BOOK HARAM,wakimaanisha kuwa mtoto wa kike hatakiwi kusoma,ni haramu kwake kutafuta elimu,lkn je uislam unasemaje khs kusoma kwa wanawake?? Qur an inasema KUTAFUTA ELIMU NI LAZIMA KWA WAISLAM WANAUME NA WANAWAKE,sasa jiulize hao bokoharamu wanafuata dini gani?? Au matakwa tu ya makabila yao nchini mwao??km yalivyo baadhi ya makabila hapa nchini kuwaweka wanawake ni watu duni wasiostahiki baadhi ya mambo,lkn sivyo dini inavyosema,je hayo ni waislam pia??
Sasa hapo uislamu uko wapi? Kuhusu suala la westgate kunusurika wamenusurika hata wakiristo,maana yupo yule mdada aliesindikizwa na gaidi alieshika silaha hd mlangoni na akatoka hakuwa muislam na anaitwa pascalia michael,sasa msiwe mnaropokwa msiyoyajua ila ulizeni kwanza,tatizo kubwa lilojitokeza ni kwamba asilimia 100% ya wasomalia ni waislam,jiulize pia wasomali wenyewe kwa wenyewe wanapigana na kuuana hd leo je wanaowaua ni wakiristo??wakati somali waislam watupu,kwa hiyo hv vikundi vinapigana wana mambo yao binafsi lkn sio dini eti imewatuma,vilianza vikundi baada ya kuuawa rais wao Siad Baree ndipo mapigano na uhalifu ukaanza km walivyopigana watusi na wahutu.
Qur an imekataza kuua nafsi isiyokuwa na hatia,naomba muisome hii qur an km waislam wanavyoisoma biblia,msikubali kuambiwa makanisani kuwa aya za shetani,hebu fungukeni muiangalie hasa ipi aya ya shetani??kuambiwa usiibe,usiue na usidhulumu,usizini na usiutoe uhai wa mwenzio ndio aya za shetani??someni muone sio kusema msiyoyajua hapana hata sehemu moja ktk qur an inayoamrisha shari au mauaji.

Mkuu kuna maswali niliwauliza ndugu zangu Bilal bin Rabah na ndugu CHAMVIGA! Na Wote wakasema Hicho unacho kataa Kua kipo!

Na pia ndugu Bilal bin Rabah akasema anaitaji muda kidogo ili aje kutoa majibu Au maelezo vizuri Zaidi! Nami niko na subira nikimsubiri!

Labda wewe ungenisaidia ili iwe hatia ndio uweze kuuwawa Kwa mujibu Wa maandiko yako inakuaje hasa? Hasa tukianza lilefundisho linalosema ni kupambana mpk kuua kuhakikisha FITNA Hakuna? Au kupambana Kwa namna yeyote Ile kutetea haki?

Nisaidie Kwa ili! Maana huenda kuna Watu wanasoma Quraan na wanakuta vitu km hivi ndio maana wanaweza wakasema mafundisho yanafundisha kuua!
Jaribu kuweka elimu ktk Hili ili hili andiko lisitumike vibaya!

Na pia kuna swala la kodi nalo pia nime muuliza ndugu Crabat lkn mpk Saizi hajatoa majibu! Nalo pia Unaweza ukatusaidia!

Asante!
 
hata mie naungana na wewe bwana Ntuzu katika kuamini hivyo kwamba ni kweli kuna kiapo kama walivyosema CHAMVIGA na BILAL BIN RABAH kwani kuna link moja nimepewa na bwana AYER inayoeleza hadith za maswahiba wa mtume.Kama ijulikanavyo hadith ni mojawapo ya nguzo kuu sana katika mafundisho ya uislam kama unataka kuuelewa uzuri.Hadith zinaelezea matendo ya mtume Muhammad S.A.W na hivyo ni elimu nzuri ya kujifunza uislam kivitendo yaani "sunna".Kwa mujibu wa mwandishi Ibn Ishaq wa kitabu cha Sirat Rasul Allah(Maisha ya mtume wa Mwenyezi Mungu),kuna hadithi mle inamuelezea mtume wakati akiwa Medina,akimtuma mmojawapo wa wafuasi wake kwenda kumuua myahudi mmoja akiitwa Abu Afak ambaye alikuwa akifanya kampeni kuwaambia watu wampuuze Muhammad na dini yake ya uislam wasijiunge nayo na yule mfuasi akafanya kama alivyoagizwa na kumvizia Abu Afak akiwa amelala akamsokomeza jambia kwenye ini hadi ncha ikagota kitandani.Akarudi na kumweleza mtume,mtume akamwambia umemsaidia Allah na mtume wake.Kwa mujibu wa hadith hii nashawishika kuamini maneno ya akina CHAMVIGA kwamba yapo mazingira na kiapo mtu anaruhusiwa kuua katika uislam.Nadhani tuendelee kusubiri ufafanuzi wao kwa yale maswali yako bwana Ntuzu lakini pia na mie nakumbushia swali langu,kwamba waislam wanafanya juhudi gani kuutangaza uislam sahihi kama ilivyo kwenye vitabu vyao ili kuionyesha dunia uislam wa kweli tofauti na ule wa kupakaziwa?ni kweli walimwengu wanawaita magaidi,je nyinyi mnafanya nini kujisafisha na tuhuma hizi ukizingatia wapo watu wanatumia uislam kufanya ugaidi na wenyewe baadhi yenu mmekiri hapa?ni muhimu kwa waislam wachanga na tusio waislam tuelimishwe na kuonyeshwa ili tujuwe uislam ni upi na uhuni ni upi ili tuwe na perception sahihi kwa uislam wa kweli ili kama jamii moja tupate washughulikia hawa wahuni ndani ya dini zetu wanaoziponza dini zetu zionekane tofauti na zilivyopaswa kuwa.
 
Juve2012.
Kwanza kabisa nataka nikujulishe uislamu unapingana na UGAIDI usione hivi vikundi vinavyo jilipua kwa mwamvuli wa kutumia uislamu ukawahukumu waislamu wote.

Ukitaka kujadiliana siku zote mambo ya imani jadiliana kwa kupitia vitabu sahihi vya huyo unaejadiliana nae sio kukurupuka na kuingia kwenye mtandao na kucopy and paste kama wakristo wengi wanavyo fanya huku kwenye mitandao ya kijamii.

Utakuta mtu amechukua hadithi ya mtume Muhamad (S.A.W)na kuileta huku bila hata kujua wanachuoni/maulamaa wa kiislamu wanaizungumziaje hiyo hadithi ni sahihi au dhaifu.

Na katika uislamu kuna somo linaitwa "mustalawal hadithi" ni lazima ujue haya mambo ndio uweze kuelezea mambo ya hadithi na ujue pia kitu kinaitwa "ilmu rijal" ndio utajua mpokeaji wa hadithi hii ni mkweli au muongo na mengineyo.....

Kwahiyo muislamu haruhusiwi kumuua mkristo hata kama anaishi nchi iliyo chini ya dola ya kiislamu, mkristo anahaki ya kuishi pale bila kubughudhiwa ilimradi atii sheria zilizoko pale na yeye atafanya ibada zake huko aliko bila ya kudhuriwa.

Kwahiyo haya yaliyotokea Kilindi mimi nilishangaa sana kwataarifa nilizo nazo nasikia ulikuwa ukionekana suruali yako ni fupi na unandevu nyingi unakamatwa unaonekana wewe ni GAIDI.

Napenda kuwafahamisha mtu kufuga ndevu au kukata suruwali sio GAIDI kwasababu haya ni mambo ya kiimani wala hayahusiani na UGAIDI na wakristo wengi wanapenda kuwashutumu watu wenye kukata suruali na kufuga ndevu na kuwaita AL QAIDA hicho kitendo sio kizuri na hakitupendezi sisi ni hayo tu.

Ahsanta.

Maalim Bilal bin Rabah. Amani iwe nawe Mkuu!

Mkuu utaniona msumbufu sn, lkn yote haya ni kutaka kupata Elimu!

Umezungumzia kitu kiitwacho HADITHI za mtume! Niliwahi kumuuliza ndugu Yangu mmoja juu ya hizi HADITHI kua zina maana gani! Akaniambia kua ni fafanuzi ya Qu'ran ndani ya uislam!

Historia inaonesha Mtume Mohamadi (saw) alipata hizi HADITHI wakati akiwa Madina na akarudi nazo Mecca. Na kule Mecca inasemakana hizi HADITHI walizikataa! Na inasemakana mpaka Leo kuna baadhi ya Waislam hizi HADITHI hawazitaki na wengine wanazitumia! Hili swala unalionaje wewe ndugu Yangu? Lina ukweli wowote? Maana hao wanaozikataa wanadai ziko na shida kidogo!

Hebu nisaidie Mkuu huku nikiona maelezo yako hapo juu ukizungumzia watu kutumia HADITHI bila kujua kua ni dhaifu au laa na pia kuna somo kwa ajili ya HADITHI! Nisaidie Mkuu kunielewesha!

Wabeja sn
 
hiki kitabu Sirat Rasul Allah ni kitabu ambacho kimekuwa quoted na wanazuoni wengi sana wa kiislam na ndio maana nimeibeba hiyo hadith baada ya kuona imekuwa quoted toka humo.Lakini mie si muislam.Nijipe uwanja wa kujifunza.Kama hiki nacho ni cha kizushi,basi tupewe list ya vitabu vyenye hadith sahihi na maelezo ya kutosha jinsi ya kuvitumia kama Bin Rabah alivyosema ili tufuatilie wenyewe.Sie wengine hupenda kuifuata source wenyewe badala ya kusimuliwa tu na masheikh kwani wao ni binadamu kama sisi wanaoweza kuwa na motives zao katika kutafsiri vitabu wakataka watu waelewe vile wanavyotaka wao.Kwa maelezo yoyote nitakayopewa hapa yakielezea tafsiri ya vitabu hasa quran na hadith,nahitaji tafsiri hizo ziwe na authority ambayo ni quran na hadith zenyewe.Nimewahi kusikia kwamba kuna matatizo kwenye hadith za mtume,kwamba waandishi wengine wanapotosha tafsiri ndio maana nataka source kama mie mwenyewe nilivyoweka source hapo juu ili wale wanazuoni wetu humu waje kunieleza kama hiyo source nao wanaitambua kama authority halali au la na kama sio basi watupe source zao na maelezo yao na sie tukajifunze kama wao walivyojifunza maana sote tu binadamu wenye akili sawa tumeumbwa na Mungu mmoja na dini yake inapaswa kujulikana na kila mwanadamu bila ubaguzi.
 
Maalim Bilal bin Rabah. Amani iwe nawe Mkuu!

Mkuu utaniona msumbufu sn, lkn yote haya ni kutaka kupata Elimu!

Umezungumzia kitu kiitwacho HADITHI za mtume! Niliwahi kumuuliza ndugu Yangu mmoja juu ya hizi HADITHI kua zina maana gani! Akaniambia kua ni fafanuzi ya Qu'ran ndani ya uislam!

Historia inaonesha Mtume Mohamadi (saw) alipata hizi HADITHI wakati akiwa Madina na akarudi nazo Mecca. Na kule Mecca inasemakana hizi HADITHI walizikataa! Na inasemakana mpaka Leo kuna baadhi ya Waislam hizi HADITHI hawazitaki na wengine wanazitumia! Hili swala unalionaje wewe ndugu Yangu? Lina ukweli wowote? Maana hao wanaozikataa wanadai ziko na shida kidogo!

Hebu nisaidie Mkuu huku nikiona maelezo yako hapo juu ukizungumzia watu kutumia HADITHI bila kujua kua ni dhaifu au laa na pia kuna somo kwa ajili ya HADITHI! Nisaidie Mkuu kunielewesha!

Wabeja sn

Mkuu Ntuzu

Ole mholla bagesha!
Kujaribu kujibu maswali yako hapo juu,
Kwanza nakuomba tu tusiende mbali saana na kutoka kabisa ktk huu uzi.
Manake hio haitokuwa haki mwa muanzilishi wa huu uzi.
Kwanza kabisa HADITH ZA MTUME (saw) KAZI YAKE SIO KUTAFSIRI QURAAN.! Bali ni mafundisho ya mtume s.a.w.
Na hadith zimeongekea All aspects of life!
Quraan ni kitabu kilichokamilika na hakihitaji msaada wa kutunga maekezo toka kwa kiumbe yyt.

Pili suala la watu wa makkah walizikataa hadith SIO KWELI KABISA na it doesn't make any sense.! Kama nilivyokwambia HADITH NI MAFUNZO YA MTUME (s.a.w)
Sasa unaposema watu wa makka walikataa hadith.

Labda una maana WALIKATAA MAFUNDISHO YAKE! Kitu ambacho sio kweli kabisa!!

Tatu. Kama ndugu yangu Bilal bin Rabah alivyokwambia kuna aina mbili au tatu za HADITH.

Ziko hadith SAHIH (Hizi zinakuwa na perfect chain of narration. ) na zinakubalika kwa waislamu wote.

Hadith dhaif (hizi hadith zinakuwepo na doughty ndani yake kutokana na wake wapokezi wa hii hadith. Na hizi haziwezi kutumika kwenye rullings issues na sio waislamu wote wenye kuzikubali.

Hadith makrooh. Hizi ni hadith za UONGO ambazo maadui wa uislamu wamebuni maneno yao halafu wanamsingizia mtume Muhammad (s.a.w ) KUWA KASEMA wakati yeye hajatamka.

Na utakuta yale maneno machafu wanayotumia wale maadui wanuislam kule jukwaani NI KTK HADITH DHAIFU!

Sasa naomba turudi kwenye uzi/mada.

Asante2q
 
Last edited by a moderator:
Kafiri ukitaka kumuelekeza.mpaka aelewe sharti moja muhimu ni.lazima akaoge kwanza!

Sasa mkuu hebu fanya hivyo mi nakisubiri.

La sivyo hapa tutakesha! Kunielewa huwezi.

Fanya fasta mara moja kabla uzi haujachafuka!

nakusoma doctor
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom