Kweli tunapiga vita ugaidi au ni vita dhidi ya uislam?

Kweli tunapiga vita ugaidi au ni vita dhidi ya uislam?

Status
Not open for further replies.
That is islaam that the world has lived with for centuries until the arrival of Osama bin laden and the likes. Arab and palestinian resistence to occupation has always taken a secular ideology until islamic fundamentalists took the stage and refused to put a difference between western imperialism and christianity and hence starting a hate campaign against christians. So what I am making reference to is the present time.
ya kale ni dhahabu na sisi tumechimba na kuacha mashimo, ...hatuwezi kurudi huko tena mkuu. tufikirie namna ya ku-deal na present and future
 
Sio maneno yangu, ni ripoti ya CIA.
Mpendwa LwamboEee, FYI, umeiamini CIA kwa kuwa CIA ni mbadala ya BIBILIA?!! UmeiAmini CIA kwakuwa inaboronga UN na kuaminisha agenda zao!! Umeamini CIA kwa kuwa wanajitolea kulisha masikini na watu duni wasio na uwezo ilimradi waonyesha utu wao!! nk,nk... Mkuu FYI sasa hao CIA ni genge la Mjangili na makatili wasio na mfano hapa DUNIANI !! Lakini wamejivisha vazi la MOTHER THREZA na kuvaa mabawa ya WHITE ANGELs. Usisahau haohao CIA walihalalisha vita vya IRAQ ambayo hadi sasa miaka 12 damu inatiririka barabarani..haohao CIA hubambikiza wamtakae na humpakizia wamtakae !! Ohh my God ..Poor people....be fair
 
Mkuu post iliyoanzisha mada haiko Balance, samahani Kwa Kusema hivyo! Na pia Kwa kutumia Hilo bandiko na Taarifa ya gazeti la Nipashe aliyo leta ndugu Bopwa! Tunaweza pata uhalisi Wa tukio na kuweza kuchangia!

Asante!

Naomba nioneshe hizo sentensi kwenye hiyo post ambazo unaamini kuwa zinaondoa "balance".

Mimi nakuuliza tena kutokana na gazeti ulilosema na post iliyoibua hii mada, Jee, mgambo akiuliwa hukumu yake ni misikiti kuvunjwa, kuchomwa moto, nyumba kuteketezwa na Qur'an kuchomwa moto?
 
Thx
Kwa Mwenye hekima akipitia Taarifa zote hizo mbili ya gazeti na bandiko la MS atapata picha ya tukio karibu lote!

Unaniuliza maswali ya hitimisho la tukio kwanini usijiulize wewe Swali dogo tu Kua kukataa kulipa kodi Au ushuru uliowekwa kisheria Kwa Madai Kua dini hairuhusu ni kosa?

Na pia huoni km tukio la kumuua Mgambo aliekua anatekeleza wajibu wake ni kosa!? Kwanza hapa kuna vitu viwili kumzuia mtu asitekeleze wajibu wake na pia mauaji!

Ndugu Yangu hili swala si la kuegemea upande wowote! Km chanzo ndio hivyo kila upande Una makosa! Waliogoma kulipa ushuru na kuua na kumjeruhi Polisi na ata Polisi nao km walitekeleza Oparesheni Yao Kwa nguvu kupita kiasi nao pia walikosea km ni kweli hayo maswali unayouliza! Tusiegemee upande mmoja ndugu Yangu ktk hili Tujaribu Kua Wa kweli na kusimamia haki!

Naamini haki itakuja kupatina Kwa wale Wote waliokumbwa na kadhia Hiyo! Maana Mfano Tumeona Oparesheni tokomeza!
 
Hizo ni propaganda za magazeti ya Tanzania Kwahiyo wewe unayaamini sana hayo yaliyoandikwa kwenye gazeti kuliko haya yaliyo letwa na mzee MS.
 
Hizo ni propaganda za magazeti ya Tanzania Kwahiyo wewe unayaamini sana hayo yaliyoandikwa kwenye gazeti kuliko haya yaliyo letwa na mzee MS.

Mkuu kuna maelezo ya ndugu Crabat nae amekielezea chanzo km gazeti lilivyo eleza na ata pia ndugu Bopwe amepost Hiyo Taarifa ya gazeti na huenda akiamini Kua huenda ikawa Ina ukweli na akaiwekea maswali matano Ivi!

Ndugu Yangu ni vema hili swala kuliangalia bila kuegemea upande wowote huo ndio msimamo wangu! Km kuna uonevu ulifanywa na vyombo vya dola ktk kutekeleza majukumu Yao Hilo ni kosa na km Hao rai waliua na kujeruhi Askari Kwa risasi nalo ni kosa!

Alafu Mbona ndugu MS hayasemi haya na yeye km yuko huko kabisa na anajua chanzo na kadhia yote kwanini hazungumzii vitu hivi? Ilipaswa atujulishe chanzo halisi Cha matatizo haya!
 
Mfumo kristo ni nini? Mfumo wa damu umeitwa mfumo kwa sababu damu imeenea kote mwilini. Watu wa dini ya kikristo imehodhi asassi zote za nyeti za uongozi na mamlaka katika nchi hii, sehemu zote za nguvu/maamuzi ya dola zimeshikwa na wakristo tangu uongozi wa juu ikulu mpaka kiongozi wa mtaa uongozi wote umeshikwa na mfumo kristo. Na hao walioshika hizo nyadhifa wanazitumia kuuendeleza ukristo na kukandamiza uislamu.

Angalia hapa kazi ya mfumo Kristo tuanze na Benki ya Posta nimegusa kiduchu tu kwenye Management Wakirto watupu unadhani hili limefanyika kwa bahati mbaya.

MR. SABASABA KITEWITA MOSHINGI
Chief Executive Officer and Managing Director

MR SOSTENES NYENYEMBE
Director of Internal Audit
MS. BERNADETHE JOSEPH GOGADI
Director of Strategic Planning

MR. MOSES MANYATTA

MR. DEOGRATIUS KWIYUKWA

Director of Marketing and Business Development

MR. MICHAEL MWAKYANDILE

Director of Credit

MR. PETER MAPIGANO

Director of Human Resources

Mr. JEMA MSUYA

Director of Operation and Technology

Ms. REGINA SAMAKAFU
Ag. Director of FinanceMrs. Mystica Mapunda Ngong
Director Legal Services
Ms. NOVES MOSES
Chief Manager, Corporate Affairs

MR.BERNARD MWANDU

Chief Manager Procuremen

Takuja na Mashirika yote na taasisi zote za serikali pamoja na wizara si umetaka kujua mfumo Kirtsto ni nini.

Mkulu nashukuru kwa kuelezea kile unachofikiri na kilichoko moyoni mwako........ umeeleza tafsiri ya mfumo kristo..... lakini kama mfumo kristo unamaanisha ni kushika dola ya nchi..... mimi ninavyoielewa biblia huo si mfumo kristo..... ni kitu kingine..... maana katika ukristo DINI HAIPASWI KUFUNGANISHWA NA SIASA..... NA hata ukikumbuka Yesu walipotaka kumfanya kuwa mfalme wa Wayahudi kutokana na Kazi zake zenye nguvu...... Yeye alikataa na kusema Ufalme wake si sehemu ya ufalme huu..... yaani yeye ufalme wake ni ule Ufalme wa Mungu ambao alifundisha tusali uje.... Yaani Baba yetu uliye mbinguni ufalme wako uje.... yaani Ufalme wa Mbinguni......

Sasa hao ambao wanafanya jitihada za kuingiza dini kwenye siasa..... siyo agizo la Mungu.... wanafanya kwa utashi wao na kwa manufaa yao.... na pia kama huo mfumo kristo upo..... sidhani kama kila mkristo anaunga mkono hiyo movement...... ni wenyewe..... Watanzania wengi tanachojua nchi yetu haina dini (secular state) lakini wananchi wake wana dini..... na hili baba wa Taifa hili Mwl. Julius K. Nyerere alilizungumzia bila kumung'unya maneno....

Labda nikuulize maswali .....

1. Katika wale uliowaorodhesha majina toka Benki ya Posta...... una uhakika gani kuwa wale ni wakristo??? (au wakristo jina??)

2. Je una ushahidi kuwa walitumia kigezo cha udini kuwaajiri???

Kuhusu mfumo wa uongozi wa nchi

3. Rais wetu (ambaye kwenye uchaguzi wa 2005 alichaguliwa kwa kishindo) ni muislam na makamu wake... je inamaanisha waislam ndiyo pekee waliomchagua tukizingatia kuwa ulieleza kuwa mfumo kristo uliasisiwa kuukandamiza uislam... je kwa nini mfumo kristo haukumuangusha rais Kikwete ambaye ni muislam????

4. Rais wetu ni muislam na makamu wake..... ina maana no watakuwa na jukumu la kujenga mfumo islam????

5. Ukiangalia kiuwiano kati ya idadi ya wakristo na waislam..... huoni kuwa katika kila nyanja uwiano huo utaendelea kujitokeza???

Ni hayo tu ndugu yangu.....
lakini kikubwa ninachoamini kuwa kupata elimu..... ajira au kuwa maarufu hakutegemei dini ya mtu.... kinategemea kujituma kwa mtu mwenyewe..... ingekuwa hivyo basi tusingekuwa na akina Jakaya M. Kikwete kama Rais, Dr. Mohamed Bilal (I use to call him the scientist), Zito Kabwe (The revolutionalist) Dr. Kawamba, Dr. Idrisa, The late Prof. Harub Othman, Dr. Salim A. Salim (I use to call him the diplomat). Na wengine wengi....
Hivyo cha msingi tuwaambie vijana wasome ili wawe na uwezo wa kupambana na mazingira yanayowazunguka..... Hilo la udini ni la kufikirika.... na kama lipo, basi lipo kwa nasibu na si la kimpango mkakati, pia kama lipo basi hali wakilishi wakristo wote.... na pia kama lipo halipo kwa msingi wa biblia maana biblia hairuhusu kuchanganya dini na siasa....maana ukisoma kwenye ufunuo falme zote hizi zitaangamizwa.... zipo kwa kipindi kifupi...
 
Mfichuasiri,
Maneno hayo yako yote ni sawa kabisa na wala mimi sikupingi katika hilo.

Lakini hao Al Shabab hawajapata kuwapo popote nchini kwetu.
Kisingizio cha ugaidi kinatumika kwa chuki kuupiga vita Uislam.

Hadi leo serikali haijawaonyesha Waislam ushahidi wa kuwapo kwa Al Shabab
huko Madina, Dibungo na Lwande.

Hata kesi iliyofunguliwa Handeni dhidi ya Waislam kosa la ugaidi halipo katika
charge sheet.

Na Waislam tulionya siku nyingi kuhusu hatari hii ya vyombo vya dola kutumika
kama ''armed wing of the Church.''

Haya nisemayo si maneno ya maskhara.

Tukifanya mchezo tutaja uana na mwisho wa siku sote tutakuwa tumepoteza
na watakaokuja kutupatanisha ni hawa hawa Wamerekani.

Mwanzo wa mvua manyunyu.
Mwanzo wa nyimbo lelelelele.

Mwisho.
Umeandika vyema ukitoa neno ''upuuzi.''

Penye nyekundu hapo nyie ndo mna-develope chuki za kidini ili wajinga wajinga wajitokeze kwenye kile kitu mnakiita Jihad...... Hivi Kanisa linaingiaje hapa????? Baadhi ya Waislam ni walalamishi sana binfsi nahisi Waislam ili wawe Confortable hawatakiwi kujichanganya na watu wa dini tofauti haiwezekani Serikali ichemshe kitu dhidi ya Uislam na waislam alafu unajitokeza mtu unalichomekea kanisa... Sipati Picha Kikwete na Makamu wake wangekuwa Wakristo sijui Serikali ingelalamikiwa kwa kiwango gani hivi Kanisa lina Influence yeyote kwa dola?
 
you hit the bull eye.safi sana
 
na kwa nini kuwe na mfanano wa matukio kilindi na Lushoto?je,huko Lushoto ilikuwa wananchi wote au wananchi waislam?kwa kweli kama ishu iko hivi alivyoileta Bopwe,hapa inabidi tuwe waangalifu!huenda kuna mengi yamejificha nyuma ya pazia.Ni tukio linalohitaji uchunguzi kwa kweli ila kuna umuhimu sasa wa yale maswali yetu kujibiwa na bin Rabah.Nilivyoelewa mimi tukio la kumuua mgambo wakati akitekeleza wajibu wa kuzilinda sheria,pamoja na kushambuliwa na watu wenye silaha msikitini ni provocation iliyosababisha watumie nguvu.Sasa kama hii violent resistance waliipata kutoka kwa kundi moja la wananchi,ilibidi kulifuatilia kundi hilo na ndipo hapa maswali ya Ntuzu hapo juu yanapokuwa ya maana na kama hizo elements zipo basi huu ni ugaidi haijalishi jina gani limetumika kuupendezesha iwe waislam,iwe wananchi n.k cha msingi kabisa,twende kwenye root cause,je,huo ushuru wa hiliki ni utaratibu halali kisheria hapo?ni basis gani aliyepinga alizisimamia kama sababu ya kupinga?je,hizo sababu ni rational?

Kuna uwezekano wa kuwa kata nzima wananchi na Waislam.
Kuna mchangiaji mada mwanzoni aliyeainisha demographics za mkoa wa Tanga.
Kilindi ni eneo ambalo ni predominantly Muslim
 
Penye nyekundu hapo nyie ndo mna-develope chuki za kidini ili wajinga wajinga wajitokeze kwenye kile kitu mnakiita Jihad...... Hivi Kanisa linaingiaje hapa????? Baadhi ya Waislam ni walalamishi sana binfsi nahisi Waislam ili wawe Confortable hawatakiwi kujichanganya na watu wa dini tofauti haiwezekani Serikali ichemshe kitu dhidi ya Uislam na waislam alafu unajitokeza mtu unalichomekea kanisa... Sipati Picha Kikwete na Makamu wake wangekuwa Wakristo sijui Serikali ingelalamikiwa kwa kiwango gani hivi Kanisa lina Influence yeyote kwa dola?

Hizo ni personal feelings zako!
Unanpopewa jibu ni mawili. Aidha uridhike na hilo jibu! Au kama kuna kitu hukuridhika nacho uulize.
Sio kudadavua kwa kuonyesha kile UNACHODHANI WEWE KUWA NDICHO KILIPO!
Hio statement aliyokujibu Mzee Mohamed Said wewe badala ya kutoa hitimisho. Ulitakiwa uulize. Je! Kwanini mzee umeandika hivyo??
Sio kuandika. Ohhh ingekuwa kiongozi huyu dini hii ingekuwaje!
Au yule dini ile ingekuwaje!

Hio tunaita "dhana" na mara nyingi utakuta hizi dhana zinakupeleka.kusiko takiwa!

Na kwa kumalizia. Kama ulikuwa hujui Influence ya kanisa ndani ya dola yetu. Basi kijana una kazi kubwa sana ya kueleweshwa.
 
Me naona kanisa kama kanisa halina influence yoyote katika dola yetu kwa sababu ser8kali haina dini bali wananchi wake wana dini.

Naona tusirubane kwa ajili ya dini. bali tuangalie maendeleo ya taifa letu
 
Thx
Kwa Mwenye hekima akipitia Taarifa zote hizo mbili ya gazeti na bandiko la MS atapata picha ya tukio karibu lote!

Unaniuliza maswali ya hitimisho la tukio kwanini usijiulize wewe Swali dogo tu Kua kukataa kulipa kodi Au ushuru uliowekwa kisheria Kwa Madai Kua dini hairuhusu ni kosa?

Na pia huoni km tukio la kumuua Mgambo aliekua anatekeleza wajibu wake ni kosa!? Kwanza hapa kuna vitu viwili kumzuia mtu asitekeleze wajibu wake na pia mauaji!

Ndugu Yangu hili swala si la kuegemea upande wowote! Km chanzo ndio hivyo kila upande Una makosa! Waliogoma kulipa ushuru na kuua na kumjeruhi Polisi na ata Polisi nao km walitekeleza Oparesheni Yao Kwa nguvu kupita kiasi nao pia walikosea km ni kweli hayo maswali unayouliza! Tusiegemee upande mmoja ndugu Yangu ktk hili Tujaribu Kua Wa kweli na kusimamia haki!

Naamini haki itakuja kupatina Kwa wale Wote waliokumbwa na kadhia Hiyo! Maana Mfano Tumeona Oparesheni tokomeza!

Kwa hiyo kama mtu kakataa kulipa kodi kwa ajili ya "dini yake" na "akamuua" mgambo hukumu yake ndio misikiti ibomolewe, ichomwe moto, nyumba za watu ziteketezwe na Qur'an ichomwe?

Na huyo mtu aliyakataa kulipa kodi ndio anakuwa gaidi?
 
Mkuu karibu kila mtu ametoa mchango kadri awezavyo na kuna mchango mmoja Wa ndugu Assuredly4 ulikua mrefu na mzuri na huenda ungekua Ndo hitimisho la mada hii!

Kwanza kabisa napenda ufahamu msimamo wangu juu ya swala hili Kua siegemei upande wowote! Ila napendekeza haki itizamwe kote!

Nikija ktk maswali yako!
Kumekua na vita nyingi duniani na wakati mwingine maadui wanaotafutwa hukimbilia ktk maeneo ya raia na huduma za jamii km vile mahospital, mashuleni, makanisani, misikitini na wengine kutumia watoto km ngao kujikinga! Na wakishambuliwa hutoka kuutangazia ulimwengu Kua tunaonewa! Au majeshi Fulani hayajali haki za binadamu etc!

Sasa sitaki Kusema kile kilichotokea huko Kilindi ni vita na Labda Yule mtuhumiwa na watuhumiwa Wa mauaji na waliokataa kulipa ushuru walikimbilia msikitini unategemea nini kingetokea na km Hiyo mbinu nilivyokuonyesha hapo juu? Simaanishi Kua hivi ni ndivyo ilivyo Nataka tujenge picha km ndio ivyo unategemea nini!? Na Bado Polisi wakawaweka chini ya ulinzi Hao waliokua msikitini na Polisi akashambuliwa na risasi! Wewe unafikiri muoendelezo Wa kuwatafuta Hao walio leta vurugu ungekuaje?

Tuangalie hili Jambo Kwa kina na si kuegemea upande wowote! Na ingekua vyema ndugu Mohamed Said akatusaidia kupata chanzo Zaidi!

Iwapo Chombo Cha dola kilitekeleza majukumu yake vibaya basi watakua na makosa na Hao ambao ni chanzo Cha vurugu na wao wanamakosa! Polisi hawawezi kukurupuka tu na kufanya hujuma bila sababu yeyote!
Asante!
 
Mhe. Rais aliyajua haya ndiyo maana akawawekea IGP muislamu,naamini angekuwa mkristo mngesema hujuma za wakristo.Je sasa muislamu mwenzenu anafanya vita dhidi ya uislamu? mm niwashauri waislamu msiwe wepesi kukimbilia kutaja udini katika matukio ya aina hii. mm siamini kuwa waliotendewa huo unyama ni waislamu peke yao kwani waislamu wana ndugu ambao sio waislamu na wengine hawana dini ambao wengine matukio haya yaliwakumba

mbona hauzungumzii vijiji viwili au vitatu vya Serengeti zilivyofutwa kwa nguvu ya polisi(nyamuma) na haya mnayolalamikia yalifanyika kule? je wakristo nao waamini kuwa ile ilikuwa hujuma dhidi ya ukristo iliyofanywa na waislamu? jibu ni hapana

tukumbuke ripoti ya kamati ya bunge ya juzi watu wametendewa unyama na uovu mkubwa ambao mwingine hata mkoloni asingeweza kuwatendea watu hawa lakini wametendewa. katika watu waliotendewa uovu walikuwemo watu wenye dini na wale wasio na dini. je hapa napo tuamini kuwa hayo yametokea kwasababu ya kutaka kuhujumu dini ya mtu, jibu sio kweli. tatizo naliona liko kwa watendaji wanaotumwa, inaonekana hawana uweledi wa taaluma yao hivyo wanafikiri wakifika wakachoma nyuma na kuwatendea watu uovu watakuwa wamewafurahisha mabosi zao na watapandishwa vyeo

mm niwashauri vijana wenzangu, kuwa udini sio mzuri kuuendekeza mwisho wa siku tutauana kwa madai ya kutetea dini zetu. hakuna vita mbaya duniani kama vita ya udini, mtu anaweza kufanya chochote ili kutetea dini yake

ushauri wangu ni kuwa nchi yetu imekumbwa na matukio mengi ya mauaji na utesaji wa watu na hakuna mtu ambaye hata leo amewajibishwa watu wakaona kweli hatua muhimu zimechukuliwa. la msingi kama nchi tujiulize ni wapi tulipokosea? kubwa zaidi hakuna uwajibikaji miongoni mwetu na viongozi wetu,kwani kuna makosa mengi yanafanyika ambayo watu walitakiwa washitakiwe hata kufungwa kabisa lakini hakuna hatua iliyochukuliwa hadi sasa.

naishauri ccm yenye serikali, iache mchezo kwenye maisha ya watu, kama ilivyoanza kuwashughulikia mawaziri mizigo na watendaji wasiofaa iongeze nguvu haya tunayoyaona yatatoweka kabisa. Lakini ccm ikijisahau wananchi wataendelea kuumia na matokeo yake wataifanya jamii iwachukie na kuwapenda wapinzani

nasema haya unayosema, si haki mtu kutendewa,tuwasiliane na watetezi wa haki za binadamu ili hatua zichukuliwe na wanaohusika wawajibishwe haraka iwezekanavyo. Naamini Mhe. Rais hatayafumbia macho, atachukua hatua ya haraka kama alivyofanya kwa mawaziri waliokiabisha chama, Serikali na Watanzania kwa ujumla. hakika hawa ndugu zangu wanastahili fidia kwa kadiri utu wao ulivyodhalilishwa

kingine tuombe taarifa ya uchunguzi ya kina sio kama ulivyoandika naona imekaa kiuchokozi sana, waandishi wapelelezi wafanye kazi yao kisha watuletee taarifa kwanini hatua hizo zilichukuliwa. unaweza kushangaa wale unaowatetea wao ndio wakawa wenye makosa? tuombe tume ifanyie kazi hili itueleze ukweli bila aibu, ndipo tutakuwa katika nafasi nzuri kuhitimisha mjadala huu

Mkuu Zomba Naomba usome haya maoni ya Huyu ndugu huenda ukapata chochote!

Asante!
 
Mkuu karibu kila mtu ametoa mchango kadri awezavyo na kuna mchango mmoja Wa ndugu Assuredly4 ulikua mrefu na mzuri na huenda ungekua Ndo hitimisho la mada hii!

Kwanza kabisa napenda ufahamu msimamo wangu juu ya swala hili Kua siegemei upande wowote! Ila napendekeza haki itizamwe kote!

Nikija ktk maswali yako!
Kumekua na vita nyingi duniani na wakati mwingine maadui wanaotafutwa hukimbilia ktk maeneo ya raia na huduma za jamii km vile mahospital, mashuleni, makanisani, misikitini na wengine kutumia watoto km ngao kujikinga! Na wakishambuliwa hutoka kuutangazia ulimwengu Kua tunaonewa! Au majeshi Fulani hayajali haki za binadamu etc!

Sasa sitaki Kusema kile kilichotokea huko Kilindi ni vita na Labda Yule mtuhumiwa na watuhumiwa Wa mauaji na waliokataa kulipa ushuru walikimbilia msikitini unategemea nini kingetokea na km Hiyo mbinu nilivyokuonyesha hapo juu? Simaanishi Kua hivi ni ndivyo ilivyo Nataka tujenge picha km ndio ivyo unategemea nini!? Na Bado Polisi wakawaweka chini ya ulinzi Hao waliokua msikitini na Polisi akashambuliwa na risasi! Wewe unafikiri muoendelezo Wa kuwatafuta Hao walio leta vurugu ungekuaje?

Tuangalie hili Jambo Kwa kina na si kuegemea upande wowote! Na ingekua vyema ndugu Mohamed Said akatusaidia kupata chanzo Zaidi!

Iwapo Chombo Cha dola kilitekeleza majukumu yake vibaya basi watakua na makosa na Hao ambao ni chanzo Cha vurugu na wao wanamakosa! Polisi hawawezi kukurupuka tu na kufanya hujuma bila sababu yeyote!
Asante!

Naona umezungusha maneno kila upande, maswali ni rahisi mno:

Kwa hiyo kama mtu kakataa kulipa kodi kwa ajili ya "dini yake" na "akamuua" mgambo hukumu yake ndio misikiti ibomolewe, ichomwe moto, nyumba za watu ziteketezwe na Qur'an ichomwe?

Na huyo mtu aliyakataa kulipa kodi ndio anakuwa gaidi?
 
Wewe umekubali kuwa ni mkiristo ambae HUNA FAIDA NA HUO UKRISTO WAKO!
Na hilo wala halinishangazi hata kidogo!
Wanaofaidika na huo Ukristo ni wale wachungwaji na makatikista na mapadri!

Wanakusanya mahela yenu wanaongeza manyumba tu!
Na zile ruzuku zinazotoka vatican wewe mtu wa chini huwezi kuziona!
Vumilia tu na bado adhabu ya Mungu inawangoja!

Unashauri na kulialia kuwa "wewe hupendi watu watoa kashfa" na hilo umeliona kwangu tu!!
Hebu msome huyu mtumishi wa kanisa aitwae Eiyer ambae ana tabia ya kuchungulia wanawake wenye vinguo vifupi anavyoandika.!

Alivyokosa malezi kutoka kwa wazee wake. Anamjibu hivyo mtu mzima sawa na baba yake!

Mimi watu kama hawa nawafananisha na mizoga ya nyamafu!
Faida hawana. Zaidi ya kujaza vyoo tu!
Na wewe usiwe mnafiki! Km unapenda haki basi na hao makafiri wanaotoa kashfa wafahamishe kuwa Yesu hapendi. Na hio ni tabia ya KAFIRI PAULO!

Now back to the thread.
Thank you.

Usiwe ukibadilisha maneno...... mimi SIJASEMA SINA FAIDA NA UKRISTO WANGU BALI NIMESEMA SIFAIDIKI NA HUO UNAOUITA MFUMO KRISTO.......MFUMO WA KUFIKIRIKA....... na sijaona ushahidi wowote kuhusiana na kuwepo kwa mfumo huo.... na hata ukiwepo ni mfumo ambao upo kwa nasibu......bila mpango mkakati..... na pia hata ukiwepo ni mfumo ambao si rasmi kwa wakristo wote (wakristo walio wengi hawaufahamu na hata wakiufahamu hawata ukbali)....... na mwishoe hata ukiwepo huo mfumo kristo si kwa mujibu wa biblia... maana maandiko hayaruhusu kuunganisha dini na siasa.... hata Yesu waipotaka kumfanya mfalme wa Wayahudi.... Yeye alikataa kwa kujua kwamba falme hizi zote za binadamu ni batili.....zipo kwa muda tu...... bali Ufalme wa Mbinguni ambao Mungu wa Mbinguni atausimamisha ndiyo utakaotawala baada ya kuzivunja falme zote hizi......

Lingine ni kuwa usipende kudharau wengine..... kwa kuwaita wanafiki..... Mbona wewe ni mnafiki na dhaifu hatukusemi...... unajifanya kutetea uislam wakati hata mara moja huonekani wazi kuanzisha mjadala wa kitaifa wa jinsi ya kuweka usawa kwa watanzania wote bila kujali imani zao.... unabaki kujificha kwenye kompyuta na kuanza kuandika uchochezi miongoni mwa watanzania..... kama wewe kweli una nia ya dhati kurekebisha hali jitokeze kwa wazi..... eleza jinsi unavyohisi.... na hata hapa kwenye JF weka jina lako kamili.... vinginevyo wewe ni kunguru tu ambaye utaishi miaka mingi lakini ya kiunafiki.....
Yaani muoga hivyo halafu... unathubutu kuwasema vibaya mtu kama Mtume Paulo ambaye alikuwa jasiri na mpaka akafa kwa kusimamia imani yake......

Hata unamshambulia kwa maneno makali Mwl. Nyerere kwenye JF wakati hata 1/8 ya IQ yake huifikii... eti bla bla bla... wewe ambaye wala hufahamiki unafanya nini .... unakaa wapi na labda unafanya nini ili kuiendeleza nchi yako......
unajificha ficha tuuu.... jiweke wazi kama kina Nyerere ujulikane na watu wajue kama wewe kweli una jambo jema kwa taifa hili....

Kama kweli wewe ni mpigania haki wa kweli achana nahiyo kazi ya kubebba maboksi halafu uende nyumbani ukijenge Tanzania yako....
 
Naona umezungusha maneno kila upande, maswali ni rahisi mno:

Kwa hiyo kama mtu kakataa kulipa kodi kwa ajili ya "dini yake" na "akamuua" mgambo hukumu yake ndio misikiti ibomolewe, ichomwe moto, nyumba za watu ziteketezwe na Qur'an ichomwe?

Na huyo mtu aliyakataa kulipa kodi ndio anakuwa gaidi?

Mkuu Mimi ktk maelezo Yangu nimegusia pande zote mbili!

Narudia tena Polisi km walitekeleza majukumu Yao vibaya walikosea na pia Na wale ambao ni chanzo Cha vurugu Hiyo na wao wanamakosa!

Sasa hapo Bado huelewi?
 
Hizo ni personal feelings zako!
Unanpopewa jibu ni mawili. Aidha uridhike na hilo jibu! Au kama kuna kitu hukuridhika nacho uulize.
Sio kudadavua kwa kuonyesha kile UNACHODHANI WEWE KUWA NDICHO KILIPO!
Hio statement aliyokujibu Mzee Mohamed Said wewe badala ya kutoa hitimisho. Ulitakiwa uulize. Je! Kwanini mzee umeandika hivyo??
Sio kuandika. Ohhh ingekuwa kiongozi huyu dini hii ingekuwaje!
Au yule dini ile ingekuwaje!

Hio tunaita "dhana" na mara nyingi utakuta hizi dhana zinakupeleka.kusiko takiwa!

Na kwa kumalizia. Kama ulikuwa hujui Influence ya kanisa ndani ya dola yetu. Basi kijana una kazi kubwa sana ya kueleweshwa.

Na fursa pekee ya kueleweshwa ni hii hapa Jamvini ili kama unanipotosha kila mtu aone na aku-challenge nijuavyo mimi watu wengi wamekuwa wanapotoshwa kwenye vinyumba uchwara vya ibada ibada za kishetani mpaka inafika mahala vijana wanaamini na wanafikia hatua ya kujitoa Mhanga kupigania hizi imani potofu kabisa, haiwezekani unamshawishi mtoto wa mwenzio akajiue kwa ajiri ya Imani eti mwisho wa siku ataenda peponi as if hao viongozi wa hizo Imani hawataki kwenda peponi kwanini wasijitoe wao, wanawapotosha watoto wa watu wanakufa huku wao wakiendelea kutwanga Mvinyo na nguruwe rost duniani, Ninaamini kabisa hapa duniani kusingekuwa na Imani za kishenzi kama hizi, dunia ingekuwa salama sana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom