assuredly4
JF-Expert Member
- Nov 7, 2011
- 1,216
- 220
Miezi michache iliyopita vyombo vya habari vilisheheni taarifa ya magaidi waliokuwa katika vijiji vya Handeni.
Taarifa zilifika Tanga kuwa kulikuwa na magaidi wanaishi katika mahandaki na operesheni maalum ilikuwa ikifanyika kuwateketeza.
Propaganda ikaenezwa kuwa walikuwa hawaitambui serikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Habari zilivuja Tanga mjini na vitongiji vyake kuwa kuna vijiji vimeteketezwa.
Kwa hakika kuna watu waliletwa Hospitali ya Bombo wakiwa na majeraha ya risasi.
Kwa watu waliofika Hospitali ya Bombo kwa kweli waliwaona vijana waliokuwa wamefungwa pingu wakiwa katika vitanda vyao huku wakilindwa na askari.
Taarifa zikafika vilevile kuwa kuna watoto wadogo wamefikishwa Tanga baada ya kukutwa porini.
Watoto hawa walikuwa wamehifadhiwa katika moja ya shule za hapo mjini.
Katika hali kama hiyo vilevile zikafika taarifa tofauti kwa Waislam wa Tanga kuwa hao walioletwa Hosptali ya Bombo na watoto waliookotwa porini ni Waislam wa vijiji vya Madina, Dibungo na Lwande walioshambuliwa na askari pasi na sababu.
Juhudi za Umoja wa Taasisi za Kiislam Tanga (SHITA) chini ya Mayor Omari Guledi na Katibu wake Ahmed Mustafa kukutana na Mkuu wa Mkoa Chiku Galawa kupata ukweli zikagonga mwamba.
Hali ikawa tete baada ya Sheikh Rajab Ramadhani Chambuso mmoja katika masheikh vijana mjini Tanga kukamatwa na kuwekwa rumande kisha kuhamishwa Handeni ambako alifunguliwa kesi ya ''kushawishi mauaji.''
Ikavuma kuwa patakuwa na maandamano kushinikiza kuachiwa kwa Sheikh Chanmbuso.
Askari wa FFU walizingira misikiti kadhaa Ijumaa hiyo lakini hapakuwa na maadamano yoyote.
Alipopata dhamana na kuachiwa Sheikh Chambuso alikuja Tanga na habari za kutisha kuhusu dhulma iliyopita katika vijiji vya Madina, Dibungo na Lwande.
Habari hizi alielezwa na mahabusi wendake katika hivyo vijiji vilivyoshambuliwa.
Sheikh Chambuso katika hotba aliyotoa katika moja ya misikiti maarufu Tanga aliwafahamisha Waislam kuhusu misikiti iliyovujwa na kuchomwa moto, Qur'an zillizochoiwa moto na nyumba za Waislam zilizoteketezwa kwa kisingizo cha ugaidi.
Wananchi jioneeni wenyewe yote hayo katika hizi picha.
PS: Weka cursor kwenye picha click utapata na maelezo ya picha.
Mhe. Rais aliyajua haya ndiyo maana akawawekea IGP muislamu,naamini angekuwa mkristo mngesema hujuma za wakristo.Je sasa muislamu mwenzenu anafanya vita dhidi ya uislamu? mm niwashauri waislamu msiwe wepesi kukimbilia kutaja udini katika matukio ya aina hii. mm siamini kuwa waliotendewa huo unyama ni waislamu peke yao kwani waislamu wana ndugu ambao sio waislamu na wengine hawana dini ambao wengine matukio haya yaliwakumba
mbona hauzungumzii vijiji viwili au vitatu vya Serengeti zilivyofutwa kwa nguvu ya polisi(nyamuma) na haya mnayolalamikia yalifanyika kule? je wakristo nao waamini kuwa ile ilikuwa hujuma dhidi ya ukristo iliyofanywa na waislamu? jibu ni hapana
tukumbuke ripoti ya kamati ya bunge ya juzi watu wametendewa unyama na uovu mkubwa ambao mwingine hata mkoloni asingeweza kuwatendea watu hawa lakini wametendewa. katika watu waliotendewa uovu walikuwemo watu wenye dini na wale wasio na dini. je hapa napo tuamini kuwa hayo yametokea kwasababu ya kutaka kuhujumu dini ya mtu, jibu sio kweli. tatizo naliona liko kwa watendaji wanaotumwa, inaonekana hawana uweledi wa taaluma yao hivyo wanafikiri wakifika wakachoma nyuma na kuwatendea watu uovu watakuwa wamewafurahisha mabosi zao na watapandishwa vyeo
mm niwashauri vijana wenzangu, kuwa udini sio mzuri kuuendekeza mwisho wa siku tutauana kwa madai ya kutetea dini zetu. hakuna vita mbaya duniani kama vita ya udini, mtu anaweza kufanya chochote ili kutetea dini yake
ushauri wangu ni kuwa nchi yetu imekumbwa na matukio mengi ya mauaji na utesaji wa watu na hakuna mtu ambaye hata leo amewajibishwa watu wakaona kweli hatua muhimu zimechukuliwa. la msingi kama nchi tujiulize ni wapi tulipokosea? kubwa zaidi hakuna uwajibikaji miongoni mwetu na viongozi wetu,kwani kuna makosa mengi yanafanyika ambayo watu walitakiwa washitakiwe hata kufungwa kabisa lakini hakuna hatua iliyochukuliwa hadi sasa.
naishauri ccm yenye serikali, iache mchezo kwenye maisha ya watu, kama ilivyoanza kuwashughulikia mawaziri mizigo na watendaji wasiofaa iongeze nguvu haya tunayoyaona yatatoweka kabisa. Lakini ccm ikijisahau wananchi wataendelea kuumia na matokeo yake wataifanya jamii iwachukie na kuwapenda wapinzani
nasema haya unayosema, si haki mtu kutendewa,tuwasiliane na watetezi wa haki za binadamu ili hatua zichukuliwe na wanaohusika wawajibishwe haraka iwezekanavyo. Naamini Mhe. Rais hatayafumbia macho, atachukua hatua ya haraka kama alivyofanya kwa mawaziri waliokiabisha chama, Serikali na Watanzania kwa ujumla. hakika hawa ndugu zangu wanastahili fidia kwa kadiri utu wao ulivyodhalilishwa
kingine tuombe taarifa ya uchunguzi ya kina sio kama ulivyoandika naona imekaa kiuchokozi sana, waandishi wapelelezi wafanye kazi yao kisha watuletee taarifa kwanini hatua hizo zilichukuliwa. unaweza kushangaa wale unaowatetea wao ndio wakawa wenye makosa? tuombe tume ifanyie kazi hili itueleze ukweli bila aibu, ndipo tutakuwa katika nafasi nzuri kuhitimisha mjadala huu