FirstLady1
JF-Expert Member
- Jul 29, 2009
- 16,789
- 5,401
- Thread starter
-
- #201
kawaida mtu anapokosea inawezekana haelewi au kuna kitu kimemsukuma kufanya jambo ambalo halikubaliki kwa mwenzake na yey akaona ni sahihi kwa wakati huo hivyo ni lazima kumweleza nini na wapi alipokosa ..
haaaaaaaaaa hivi mtu mzima na meno 32 aliyeamua kwa ridhaa yake mwenyewe kuoa ,na hatimaye kumwacha wife na kuelekea anapokujua na nyumba ndogo ,huyo ndo wa kusema umweleweshe alipokosea dah napata kigugumizi...sipati picha kamili
hahah sasa wewe unatarajia umkimbize au udhaniyo wewe naye atakuwa nayo sawa??
hivi vip wale wanaokwenda kutafta maisha kwingine na aliondoka vizuri lakini akifika huko mawasiliano taratiibu yanakatika? Na anarudi after some many yearz empty handed na unasikia amezaa na mtu huko alikokuwa?
yuko mmoja walirudiana after 17 years of separation. Wakirudiana sitashangaa.
VS ... can u pls share with us maisha yao na furaha yao ilikuwaje baada ya ku re-unite?? manake hapa wengi tunaweka uzio wa kibinadamu mbele yetu kwa kushindwa kusameheana makosa ambayo though ni makubwa kwa macho yetu, lakini yana sameheeka kwa kuangalia dhamira moja na iliyo kuu, lengo hasa la ndoa ni nini?? na unategemea unapoamua kufunga ndoa na unapoanza maisha ya ndoa yenyewe?? ni nini maana ya uvumilivu katika ndoa??
Yaani hapa hata nispomsamehe mungu ananiona kwa nn anitende namna hiyo harafu apate shida anirudie ,mbona kukumbuka wakati wa raha,nitamsamehe lakini apotee ,awe anakuja kusalimia wanae tu
ila watoto wakiweka misimamo mnaweza kurudiana hata kama hampendi ...
ni kweli in most cases, lkn ukiwa na wazazi wenye misimamo ya akina Dina, Canty na FL1, inakuwa ngumu kidogo ... matokeo ni watoto tu kuteseka sababu ugomvi/makosa ya mzazi wao mmoja yao yanawahusu nini??
kawaida matatizo ya wazazi huwa yanawaacha watoto wakiwa, wanakosa mwelekeo na huathirika sana kisaikolojia na hasa zile mbegu zinapokuwa zimemea zaidi na kukuta hakuna mawasiliano kabisa kwa wazazi
umenena vema kabisa ...
Mimi namkaribisha tu,Ila ndoa hamna.
Salama kaka,naona jana ukakimbia sred gafla!asante
Kashengo salama mkuuu!hivi vip wale wanaokwenda kutafta maisha kwingine na aliondoka vizuri lakini akifika huko mawasiliano taratiibu yanakatika? Na anarudi after some many yearz empty handed na unasikia amezaa na mtu huko alikokuwa?
Acheni hizo, maisha yako hivyo. Mungu huwa ana mipango yake kwa kila jambo linalotokea. Ningepanda kama mkisoma kitabu kinachoitwa "the power of now" na "power of letting go" Ni vizuri vinaelezea namna ambavo tunatakiwa kuishi kwa kupractise letting go. Hata kama huyo mwanaume asingeomba msamaha na kuamua kuishi kivyake lazima kuna hisia atazipata mamaa. Kumbukeni wamezaa nae watoto 3! Halafu kwa wanawake mnatakiwa kujua kuwa mumeo naye ni mwanao eeeh! Ukimsamehe ni kama umesamehe mwanao!
Ningekua mimi ningemsamehe na kuanza kuishi kwa tahadhari.
Huyo mimi binafsi nisingethubutu hata kumpa nafasi ya kuomba msamaha
we napingana na wewe mumeo sio mwanao na wala hata huwezi fananisha mme na mtoto uchungu wao ni tofauti aende kwa mama yake atampokea lakini si kwa mke wake