Kwenu Kina Baba........................!

Kwenu Kina Baba........................!

Na mimi siku yangu ishaharibiwa na hii thread ya kusikitisha.
Wababa wajitahidi kupata muda wa kuzungumza na watoto wenu muone kama mambo yapo sawa.
Hivi ni lini wanawake mtaacha kujifanya weak and Innocent? hapa zigo la ukatili lote mimi nambebesha huyu mama, Baba anabeba zigo la uzembe na ubwege.
 
Hata mie nilisikitika sana hadi nikataka kuuliza...Hivi kweli akina mama ni wakatili kiasi hicho???
 
Wapendwa
Ni matumaini yangu mlikuwa na weekend yenye Baraka.

Mimi wiki hii MwanajamiiOne nimeianza kwa uchungu huku machozi yakinitiririka barabarani asubuhi wakati nakuja kibaruani. Kwenye taarifa ya habari iliyotangazwa kupitia Radio One. Mama mmoja huko Morogoro aliyekamatwa kwa kosa la kumpiga vibaya Mtoto wa Mume wake (Mtoto wa kambo). Taarifa hiyo ambayo ilisema mtoto huyo mwenye umri wa miaka 3 inasemekana amepigwa hadi kuvunjwa mkono na mguu huku akiachiwa majeraha sehemu za kichwa baada ya kupigwa mateke, kuangushwa chini huku akijipigiza sakafuni na kung'atwa kwa meno mwilini.

Taarifa ilisema mtoto huyo (kwa mujibu wa majirani) amekuwa akichezea matezo hayo karibia kila siku pamoja na kufanyishwa kazi ngumu (Mtoto wa miaka 3??!!). Aliambulia kupigwa (tena kwa kuchangiwa na mama huyo na mwanae) pale anapotumwa kitu mfano mwiko akakosea (Mtoto wa Miaka 3!!).

Sitaki kusema mengi lakini kwa kifupi, kina Baba ambao mna watoto wenu ambao hamuishi na mama zao, NINAWAOMBA muwe japo na kajitabia ka kusoma alama za nyakati. Ni kweli kuwa si mama wote wa kambo ni wabaya lakini you never know just take time kuchungua mazingira.

Ningetamani kweli kujua namna ya kufanya hili liwe kweli lakini sijui, yaani nashuindwa kuwaza kabisa.
KUWENI tu MAKINI.

MBARIKIWE SANA KINA BABA NA MAMA WAZAZI/WALEZI WENYE MIOYO YA UPENDO KWA WATOTO WAO HATA KAMA HAWAJAWAZAA WAO.

Yaani MwanajamiiOne, mimi nilimuona huyo binti kwenye TV jana, yaani nililia nikajiuliza maswali mengi sana!

Kwanza nilimchukia saana saaaana huyo mama wa kambo then nikajiuliza;-
1. Where is mama yake mzazi? Amefariki au?
2. Baba yake yuko wapi na anafanya nini?
3. Huyo mama wa kambo yuko okay upstairs? Au naye anakuwa abused na mume wake that analipiza kisasi kwa mtoto wake.

Nikakumbuka tukio lililotoke Hifadhi ya Taifa Gombe, about askari wa kisukuma aliyekuwa na mke na mtoto wa kike coincidentally ni same age na huyo victim wa Morogoro. Yule askari before Gombe alikuwa Serengeti au Manyara NP, akapata mwanamke wa kiarusha na kumuacha mkewe (msukuma) na kuja huku na huyo binti wa kiarusha. Unaambiwa alivyokuwa huku (Gombe) alikuwa anampiga sana yule binti wa miaka 3, watu wakimwambia mume wake, anasema wanamuonea. It went on mpaka yule mtoto akafariki after kipigo (maana alibleed internally) corruption and all wakasingizia kuwa alikuwa anaanguka kifafa.

lakini yule mwanamke alitoroka. Hivyo kwa kiwango kikubwa wanaume wanachangia sana, mateso ya watoto wao. Swali la msingi kwanini hawawaachi na mama zao wazazi? Matukio kama haya yanachangia sana kina mama kung'ang'ania abusive ndoa kwa hofu ya watoto wao kuteswa na mama wa kambo; pale ambapo hajafukuzwa na ana option ya kuendelea kukaa huyo mume. Lakini sheria inampa mama haki ya kubaki na mtoto akiwa under 7 sijui kwanini hawaondoki nao?

Kifupi inauma saana yaani!
 
Mtoto wa miaka mitatu?????????????

Siku yangu yooote imeharibika kabisa na wala sitaki kuamini.............

Miaka mitatu (3)?????????? Kweli kuna wanawake wanyama Duniani kwanza unampiga mtoto kwanini???
Kha wajameni ai hata nashindwa kuendelea kuandika na imagine alivyo
 
Pole MJ1, kuna wamama wana roho za ajabu sana. Hivi kweli mtoto wa 3yrs ni wakupigwa kiasi hicho? Na nyie kina baba hebu jaribuni kuwa karibu na watoto wenu haswa kama mama anayeishi nae sio mama yake mzazi , msikubali kuleweshwa na mapenzi afu mkasahau watoto wenu. Kuna wamama wazuri wanaoweza kuishi vema na watoto wa waume zao bt pia inategemea na baba wa mtoto alivyo. Kama baba unaondoka nyumbani asubuhi, unarudi usiku wa manane ni mda gani utaelewa udhaifu wa mkeo? Kueni karibu na watoto wenu kuwaepusha na mateso ya wamama waliojaaliwa roho mbaya zisizo na hata chembe ya aibu wala huruma! Hivi kama mama huwezi kulea mwana wa mwenzio si umwambie mumeo amrudishe kwa mama yake? Mungu wabariki wamama wote wenye mioyo ya kibinadamu. Wabariki pia na wababa wote wanaojali na kuwatunza watoto wao.
 
3yrs old anapigwa na watu wawili. Majirani wanajua, wanashndwa kuchukua hatua!!!. Kina mama punguzeni roho mbaya kwani huyo naye ni mtoto sawa na wako.
Mzee..............ninantamani majirani wote nao watiwe kashkash kwa kufumbia macho suala hili kwa siku zote hizo (Ingawa wao ndio waliomfikisha polisi baadae) Lakini kwa mujibu wa shosti wake huiyu mwanamke ni kuwa walikuwa wanamkanya kila siku (Hivi kweli wewe mama mwenye uchungu, unaona mtoto anapigwa mara ya kwanza unavumilia, ya pili unavumilia tena? - angekuwa anachapwa kwa fimbo ningeelewa kuwa pengine anamfundisha -kama alivyokuwa anajibu, lakini ngumi, mateke, meno oh my God.

Tena eti siku moja aliwahikumpiga huku akimwangusha kwenye stuli na meza kisa? alimtuma mwiko mtoto akamletea akampa BILA KUPIGA MAGOTI..........mama anajibu namfundisha tabia za kwetu (Tabora). Jamani mtoto wa miaka 3 anajua magoti ni nini?? tena magoti ya uwoga??

Wanawake tuangalie tusijekuwa kuni za moto wa jehanam.
 
Mtoto wa miaka mitatu?????????????

Siku yangu yooote imeharibika kabisa na wala sitaki kuamini.............

Miaka mitatu (3)?????????? Kweli kuna wanawake wanyama Duniani kwanza unampiga mtoto kwanini???
Kha wajameni ai hata nashindwa kuendelea kuandika na imagine alivyo
Inauma DA haswa kama umeshawahi kuonja uchungu wa kujifungua! Wamama wahakikishe wanaishi na watoto wao wenyewe hata kama hukai na babake.
 
Married to the devil...
Mama crap na shetani....
Baba crap....
Matokeo: Mtoto kuonja ladha ya jehanam akiwa na miaka mi3...
 
Hivi ni lini wanawake mtaacha kujifanya weak and Innocent? hapa zigo la ukatili lote mimi nambebesha huyu mama, Baba anabeba zigo la uzembe na ubwege.

............Shemeji nadhani inatupasa kuweka sheria kali kwa wote, wewe mama unayemnyanyasa mtoto, wewe babab (usiyejua kuwa mwanao ananyanyashwa (ni uzembe) na ikiwezekana hata majirani wanaowazunguka ikijulikana kuwa walifahamu juu ya manyanyaso hayo.

Jamiii yote tunahusika haya mambo ya usiingilie familia yangu (kama ile thread ya Nazdas ya kibao cha UKIJA UJE NA YAKO, YA HUMU UTUACHIE sijui tuyaache. Tuingiliane tu hata hayo ya ndani kama yanahusiana na unyanyasaji na ukatili wa mtoto. !
 
Well said shemeji! Lakini bongo ni kibongobongo tu, tatizo hakuna utawala wa sheria, kwa wenzetu mtoto akionekana anasinzia shule tu basi mzazi unatakiwa ukajieleze kwanini mtoto haumlazi masaa ya kutosha?

Dah!yaani hii sredi imeniharibia mpaka apetaiti ya kutongoza leo.
 
Hivi ni lini wanawake mtaacha kujifanya weak and Innocent? hapa zigo la ukatili lote mimi nambebesha huyu mama, Baba anabeba zigo la uzembe na ubwege.
Kinachoanza siku zote ni uzembe na ubwege wa baba, afu ukatili unapata nafasi ya kuwepo. Nawachukia wanaume mabwege na wazembe! Kwanini baba ukose sauti kwa mkeo? Haya mazingira ya watoto kunyanyaswa na mama zao wa kambo wababa huwa wanayatengeneza wenyewe! Kuweni karibu na watoto wenu bana. Msiwaamini sana hao mama zao wa kambo. Sio kila mwanamke anampenda mtoto wa mwenzie!
 
Married to the devil...
Mama crap na shetani....
Baba crap....
Matokeo: Mtoto kuonja ladha ya jehanam akiwa na miaka mi3...
Inauma! Najaribu kufikiria mtoto wa miaka mi3!!.. Yan sipati jibu kama huyo mama anayemtesa mtoto mdogo hivi akili zake zimetimia kweli...
 
Kinachoanza siku zote ni uzembe na ubwege wa baba, afu ukatili unapata nafasi ya kuwepo. Nawachukia wanaume mabwege na wazembe! Kwanini baba ukose sauti kwa mkeo? Haya mazingira ya watoto kunyanyaswa na mama zao wa kambo wababa huwa wanayatengeneza wenyewe! Kuweni karibu na watoto wenu bana. Msiwaamini sana hao mama zao wa kambo. Sio kila mwanamke anampenda mtoto wa mwenzie!
Hapo red ndio wabeijing nakuwa siwaelewi! mkitaka kumtupia lawama mwanaume mnajifanya "kwanini mume unakosa sauti kwa mkeo?" Lakini mkiona mambo shwari mnajifanya haki sawa kwa wote. All in all, hatujaelezwa situation ya baba kiundani, anajishughulisha na nini? yupo 24/7 nyumbani? anafanya kazi local au mkoani? etc. Uskute baba wa watu kumbe anameza vidonge vya masaa anasumbuliwa na kifaduro au anafanya kazi za kusafiri etc
 
Well said shemeji! Lakini bongo ni kibongobongo tu, tatizo hakuna utawala wa sheria, kwa wenzetu mtoto akionekana anasinzia shule tu basi mzazi unatakiwa ukajieleze kwanini mtoto haumlazi masaa ya kutosha?

Dah!yaani hii sredi imeniharibia mpaka apetaiti ya kutongoza leo.

Utanisamehe tu bure shemeji maana kwa hili, leo hata Mbu hachekewi hapa!! Vumilia utatongoza kesho.

Si ndio hapo sasa, akisinzia sie walimu tunamtandika kujua ni uzembe kumbe kalazwa saa saba akikingishwa maji wakati mama kalala! Wanawake?! Yaani huyu ni mnyama mimi nasema maana kwa waliomuona mtoto kwenye taarifa ya habari wanasema mtoto kang'atwa meno ............huyu mama lazima ni mnyonya damu (Vampire- sijui wazungu mnawaita) kabisa.

Kuna thread moja kuna mtu alilalamika kuwa Ustawi wa jamii, masocial workers wanashinda ofcn wakinywa vyai tu waati matukio kama haya wao ndio tunawategemea wawe mstari wa mbele kuyatambua na kuchukua hatua!

Na nyie wababa, bado nina nyie kuna baadhi yenu huona tu ufahari kumnyang'anya mtalaka wake watoto ilhali bado wadogo. Mnawaadhibu bila kujua wenenu maana hao wanawake wengine mnaowapelekea wawalee ndicho wanachokifanya. Wewe unahangaika kazini unajua mkeo analea vema kumbe ndo watoto wanafanywa ngoma na vitafunwa!!
 
Inauma! Najaribu kufikiria mtoto wa miaka mi3!!.. Yan sipati jibu kama huyo mama anayemtesa mtoto mdogo hivi akili zake zimetimia kweli...
Uskute huyo mama ni member wa JF na yeye anaitwa greti thinka na anaanzisha sredi za malezi bora. heheehhe hapo ndo utajua kwanini nanasi linaitwa painepol
 
Inauma! Najaribu kufikiria mtoto wa miaka mi3!!.. Yan sipati jibu kama huyo mama anayemtesa mtoto mdogo hivi akili zake zimetimia kweli...

Wazazi wengi hawajui majukumu ya uzazi wao....hawajui uzazi ndo wajibu wa kwanza katika maisha yao....
 
Hivi ni lini wanawake mtaacha kujifanya weak and Innocent? hapa zigo la ukatili lote mimi nambebesha huyu mama, Baba anabeba zigo la uzembe na ubwege.

swala sio kujifanya innocent na mimi sijamtetea huyo mama ila iwe tahadhari kwa wababa. Watoe fursa kwa watoto kujadili matatizo yao.
Kwenye kunyanyasa watoto katili ni katili haijalishi kama ni mama/baba mzazi au wa kambo.
 
Well said shemeji! Lakini bongo ni kibongobongo tu, tatizo hakuna utawala wa sheria, kwa wenzetu mtoto akionekana anasinzia shule tu basi mzazi unatakiwa ukajieleze kwanini mtoto haumlazi masaa ya kutosha?

Dah!yaani hii sredi imeniharibia mpaka apetaiti ya kutongoza leo.

Duh, hii kali
 
Hapo red ndio wabeijing nakuwa siwaelewi! mkitaka kumtupia lawama mwanaume mnajifanya "kwanini mume unakosa sauti kwa mkeo?" Lakini mkiona mambo shwari mnajifanya haki sawa kwa wote. All in all, hatujaelezwa situation ya baba kiundani, anajishughulisha na nini? yupo 24/7 nyumbani? anafanya kazi local au mkoani? etc. Uskute baba wa watu kumbe anameza vidonge vya masaa anasumbuliwa na kifaduro au anafanya kazi za kusafiri etc

SHEMEJI AKSANTE KWA HII POST. Lengo zima la kuiweka hii thread (na hasa kuwalenga wababa) lipo hapo kwenye red. Sikuwa na nia ya kuwaharibia siku wala kuwatia hasira wala haikuwa lengo langu kulaumu au kuendeleza lawama (Sheria ishaingilia kati na tunaamini itachukua mkondo wake). Lengo lilikuwa ni kuangalia namna ya kuhamasisha ufuatiliaji wa watoto (with special attention wale ambao wanaishi na wamama wa kambo -whether awe mwenye roho mbaya au la)..Hivi kweli baba hakuna njia unazowezafanya ili kufuatilia ukuaji na malezi ya mwanao? (From the Child's perspective) Sio kila siku ukirudi unaishia tu kuuliza "Wanaendeleaje hao?"; "Wameshindaje hao"??
 
Back
Top Bottom