.................... Halafu watoto hawa wanapokuwa wanashindwa kujieleza, kuuliza au kuhoji ukubwani tunashangaa!! Baba ukirudi nyumbani kwako kuwa na tabia ya kuongea na wanao (hata kama si maswala ya nyumbani) basi hata mpira- see anavyojielezea kwa uhuru au lah. Anaongea kwa uwoga au hapana? waweke karibu lakini si kuwafanya wakuone wewe chui ilhali mama ni simba.
Mimi nakumbuka baba yetu alikuwa ni mkali kupindukia, ukisikia tu gari lake linakata kona kuja lunch mchana, wote tunatawanyika! mwenye kuingia kwenye mabanda ya kuku haya, kwa ng'ombe hivyo hivyo ilimradi haoni mtu (na hapo chakula chake Mwj1 ashaweka mezani) akimaliza kula, anakwenda kulala ile 30 mins yake ugali ushuke vizuri. Sie kutoka mafichoni ni mpaka usikie tena karandinga lake likimalizia kukata kona ndo mnachomoza mmoja mmoja. Ilikuwa kupitiliza siku mbili hamjaonana ni kitu cha kawaida.
Siku hizi tunamchezea kama Babu! na ukimsimulia alivyokuwa anabisha hakuna mfano akiona mnamzidi point, anawaagizia konyagi!!