Darlingtone
JF-Expert Member
- Jan 9, 2011
- 390
- 146
Utanisamehe tu bure shemeji maana kwa hili, leo hata Mbu hachekewi hapa!! Vumilia utatongoza kesho.
Si ndio hapo sasa, akisinzia sie walimu tunamtandika kujua ni uzembe kumbe kalazwa saa saba akikingishwa maji wakati mama kalala! Wanawake?! Yaani huyu ni mnyama mimi nasema maana kwa waliomuona mtoto kwenye taarifa ya habari wanasema mtoto kang'atwa meno ............huyu mama lazima ni mnyonya damu (Vampire- sijui wazungu mnawaita) kabisa.
Kuna thread moja kuna mtu alilalamika kuwa Ustawi wa jamii, masocial workers wanashinda ofcn wakinywa vyai tu waati matukio kama haya wao ndio tunawategemea wawe mstari wa mbele kuyatambua na kuchukua hatua!
Na nyie wababa, bado nina nyie kuna baadhi yenu huona tu ufahari kumnyang'anya mtalaka wake watoto ilhali bado wadogo. Mnawaadhibu bila kujua wenenu maana hao wanawake wengine mnaowapelekea wawalee ndicho wanachokifanya. Wewe unahangaika kazini unajua mkeo analea vema kumbe ndo watoto wanafanywa ngoma na vitafunwa!!
Nashindwa kuelewa kabisa, sitaki kusema ni shetani kuna haja ya kuanza kuchunguza akili za watu za watu linapokuja suala la maleziWapendwa
Ni matumaini yangu mlikuwa na weekend yenye Baraka.
Mimi wiki hii MwanajamiiOne nimeianza kwa uchungu huku machozi yakinitiririka barabarani asubuhi wakati nakuja kibaruani. Kwenye taarifa ya habari iliyotangazwa kupitia Radio One. Mama mmoja huko Morogoro aliyekamatwa kwa kosa la kumpiga vibaya Mtoto wa Mume wake (Mtoto wa kambo). Taarifa hiyo ambayo ilisema mtoto huyo mwenye umri wa miaka 3 inasemekana amepigwa hadi kuvunjwa mkono na mguu huku akiachiwa majeraha sehemu za kichwa baada ya kupigwa mateke, kuangushwa chini huku akijipigiza sakafuni na kung'atwa kwa meno mwilini.
Taarifa ilisema mtoto huyo (kwa mujibu wa majirani) amekuwa akichezea matezo hayo karibia kila siku pamoja na kufanyishwa kazi ngumu (Mtoto wa miaka 3??!!). Aliambulia kupigwa (tena kwa kuchangiwa na mama huyo na mwanae) pale anapotumwa kitu mfano mwiko akakosea (Mtoto wa Miaka 3!!).
Sitaki kusema mengi lakini kwa kifupi, kina Baba ambao mna watoto wenu ambao hamuishi na mama zao, NINAWAOMBA muwe japo na kajitabia ka kusoma alama za nyakati. Ni kweli kuwa si mama wote wa kambo ni wabaya lakini you never know just take time kuchungua mazingira.
Ningetamani kweli kujua namna ya kufanya hili liwe kweli lakini sijui, yaani nashuindwa kuwaza kabisa.
KUWENI tu MAKINI.
MBARIKIWE SANA KINA BABA NA MAMA WAZAZI/WALEZI WENYE MIOYO YA UPENDO KWA WATOTO WAO HATA KAMA HAWAJAWAZAA WAO.
SHEMEJI AKSANTE KWA HII POST. Lengo zima la kuiweka hii thread (na hasa kuwalenga wababa) lipo hapo kwenye red. Sikuwa na nia ya kuwaharibia siku wala kuwatia hasira wala haikuwa lengo langu kulaumu au kuendeleza lawama (Sheria ishaingilia kati na tunaamini itachukua mkondo wake). Lengo lilikuwa ni kuangalia namna ya kuhamasisha ufuatiliaji wa watoto (with special attention wale ambao wanaishi na wamama wa kambo -whether awe mwenye roho mbaya au la)..Hivi kweli baba hakuna njia unazowezafanya ili kufuatilia ukuaji na malezi ya mwanao? (From the Child's perspective) Sio kila siku ukirudi unaishia tu kuuliza "Wanaendeleaje hao?"; "Wameshindaje hao"??
Unajua shemeji hapa kuna mambo mengi sana yanaizunguka hii kadhia na nadhani sio suala la kutatuliwa kwa ushauri ni suala ambalo hutatuliwa kwa kusimamiwa na sheria ya nchi kupitia ustawi wa jamii kama ulivyosema. Kuna binadamu wanazaliwa na animal traits kama huyu mama, kuna wengine wanaathirika kisaikolojia through life experience na wapo wanaobehave hivi kutokana na wivu na chuki zao binafsi tu. Masuala kama haya ni tabu kuyaondoa kwenye damu za watu bila adhabu. Sasa acha nikubaliane na wewe kwamba hao ustawi wa jamii ndio wa kuwajibishwa na through wao ndio wawajibishwe wamama makatili , wababa wazembe na majirani pia.
Dah! bro wangu Mbu leo namuona laivu analazwa mzungu wa nne
Pole sana kwa uchungu Mj1,na sisi wababa tumeuchukua ushauri wako kwa uzito mkubwa_lakn ni bora zaidi pia unge wa adress wamama kwani wao ndio wafanyaji wakubwa wa vitendo hivi vya kinyama,...wewe kama mama mwenzao ungechukua nafasi hii kuwaomba waache kuwatesa watoto ambao hawaja wazaa,....ila inasikitisha na kuuma sana
Shem! sio kila mwenye mtoto ni mzazi/baba/mama. Ukiangalia maana ya mzazi kwa upana wake utagundua kwamba hakuna mzazi atakaeruhusu upuuzi huu na ndio maana nikasema adhabu inahitajika ili kuwanusuru watoto kutokana na bahati mbaya ya wao kuletwa duniani na watu wasiojua wajibu wao wa kuwalinda na kuwatetea.Well said Shemeji. Nakubaliana kabisa na wewe kuwa sababu za ukatili huu ziko nyingi. Tunauzuiaje sisi kama wazazi wahusika?
Shemeji unaye mwanao/wanao wanaishi na mama yao wa kufikia. Ili uhakikishe kuwa wanapewa malezi unayoyafikiria unafanyaje?? unachunguzaje kama pesa ya kilo ya nyama uloiacha kwanza inanunulia nyama kama ulivyoagina na watoto hao wanakula kama unavyofikiria??
Mbu ana bahati hii nimeisikia asubuhi, ama sivyo angekesha akinibembeleza hili jilio!
Kesi ya huyu ni tofauti lakini tukitoka nje ya box, wapo kina mama ni qualified pretenders, hauwezi kubaini kirahisi. na hutumia vitisho kuwafumba midomo watoto.
BTW nadhani shem wewe unawaongelea wale waliokuwa baba kabla kuwa tayari kuwa baba, na hili ni janga la taifa jengine.
.................... Halafu watoto hawa wanapokuwa wanashindwa kujieleza, kuuliza au kuhoji ukubwani tunashangaa!! Baba ukirudi nyumbani kwako kuwa na tabia ya kuongea na wanao (hata kama si maswala ya nyumbani) basi hata mpira- see anavyojielezea kwa uhuru au lah. Anaongea kwa uwoga au hapana? waweke karibu lakini si kuwafanya wakuone wewe chui ilhali mama ni simba.
Mimi nakumbuka baba yetu alikuwa ni mkali kupindukia, ukisikia tu gari lake linakata kona kuja lunch mchana, wote tunatawanyika! mwenye kuingia kwenye mabanda ya kuku haya, kwa ng'ombe hivyo hivyo ilimradi haoni mtu (na hapo chakula chake Mwj1 ashaweka mezani) akimaliza kula, anakwenda kulala ile 30 mins yake ugali ushuke vizuri. Sie kutoka mafichoni ni mpaka usikie tena karandinga lake likimalizia kukata kona ndo mnachomoza mmoja mmoja. Ilikuwa kupitiliza siku mbili hamjaonana ni kitu cha kawaida.
Siku hizi tunamchezea kama Babu! na ukimsimulia alivyokuwa anabisha hakuna mfano akiona mnamzidi point, anawaagizia konyagi!!
Mimi ningependa kuuliza kwa mwenye uelewa wa historia, hivi hizi kadhia za mateso ya mama wa kambo ni tangu na tangu au zimeibuka zama hizi zetu?
Shem! sio kila mwenye mtoto ni mzazi/baba/mama. Ukiangalia maana ya mzazi kwa upana wake utagundua kwamba hakuna mzazi atakaeruhusu upuuzi huu na ndio maana nikasema adhabu inahitajika ili kuwanusuru watoto kutokana na bahati mbaya ya wao kuletwa duniani na watu wasiojua wajibu wao wa kuwalinda na kuwatetea.
Sahihisho: huyu tunaemzungumzia hapa si baba, huyu ni mtu alietia mimba na akaleta mtoto duniani bila kujielewa
Shem, mimi si mwelewawa historia lakini kutokana na kuwa kila ajabu ninalolishangaa siku hizi naambiwa hata zamani yalikuwepo sema tu hayakuwa yakitangazwa kutokana na press coverage haikuwa kubwa na mambo ya haki haki yalikuwa bado machanga!
Lakini kwa hili la unyanyasaji wa watoto kidogo nahizi kama halikuwepo na hisia zangu zinachangiwa na ile kumbukumbu kuwa enzi hizo mtoto hakulelewa na baba na mama tu ndani ya nyumba bali hata majirani na jamii iliyowazunguka hivyo naamini ingekuwa vigumu mwanamke kuny'anyasa mtoto kiasi hiki halafu ikapotezewa tu!
Sijui lakini ni hisia zangu.
Hata mie nilisikitika sana hadi nikataka kuuliza...Hivi kweli akina mama ni wakatili kiasi hicho???
Wee acha tu shem!Nimekuelewa shemeji aksante kwa kunielewesha vizuri. Sasaa dah hata sijui niulizeje maana na hili wimbi la mimba za watoto (watoto wadogo kupeana mimba kabla ya kufikia uwezo wa kuwa baba) si tutayashuhudia mengi sana haya jamani?!
Wapendwa
Ni matumaini yangu mlikuwa na weekend yenye Baraka.
Mimi wiki hii MwanajamiiOne nimeianza kwa uchungu huku machozi yakinitiririka barabarani asubuhi wakati nakuja kibaruani. Kwenye taarifa ya habari iliyotangazwa kupitia Radio One. Mama mmoja huko Morogoro aliyekamatwa kwa kosa la kumpiga vibaya Mtoto wa Mume wake (Mtoto wa kambo). Taarifa hiyo ambayo ilisema mtoto huyo mwenye umri wa miaka 3 inasemekana amepigwa hadi kuvunjwa mkono na mguu huku akiachiwa majeraha sehemu za kichwa baada ya kupigwa mateke, kuangushwa chini huku akijipigiza sakafuni na kung'atwa kwa meno mwilini.
Taarifa ilisema mtoto huyo (kwa mujibu wa majirani) amekuwa akichezea matezo hayo karibia kila siku pamoja na kufanyishwa kazi ngumu (Mtoto wa miaka 3??!!). Aliambulia kupigwa (tena kwa kuchangiwa na mama huyo na mwanae) pale anapotumwa kitu mfano mwiko akakosea (Mtoto wa Miaka 3!!).
Sitaki kusema mengi lakini kwa kifupi, kina Baba ambao mna watoto wenu ambao hamuishi na mama zao, NINAWAOMBA muwe japo na kajitabia ka kusoma alama za nyakati. Ni kweli kuwa si mama wote wa kambo ni wabaya lakini you never know just take time kuchungua mazingira.
Ningetamani kweli kujua namna ya kufanya hili liwe kweli lakini sijui, yaani nashuindwa kuwaza kabisa.
KUWENI tu MAKINI.
MBARIKIWE SANA KINA BABA NA MAMA WAZAZI/WALEZI WENYE MIOYO YA UPENDO KWA WATOTO WAO HATA KAMA HAWAJAWAZAA WAO.
edson....ubarikiwe kwa hilo hapo jekundu. Halafu uchaji MUNGU unaouzungumzia hapa edson wa siku hizi ni balaa tu. Tena usijeshangaa mmama huyu ni mzee wa sehemu anayosali au kiongozi wa wakina mama kanisani!!mkuu kwa asli mwanamke ni katili sana..tena sana....wenye neema na heri ni wachache hasa wale wenye uchaji wa Mungu kana kima mwanajamii1.....na matukio kama haya ni megi sana kuna moja nilishuhudia kimara mwisho mwaka jana ilikuwa balaa yule mama tulimpeleka hadi polisi sisi majirani...