Patrice Diounis
JF-Expert Member
- Jul 24, 2023
- 1,086
- 2,254
Kila taifa lililoanguka lilianza kwa ukimya na kunyamazishana.
Hasa pale wanasiasa walipoikamata Intelijensia na wasiochaguliwa pia waliotupwa mkono kikatiba wakaitawala serikali.
Kikubwa taifa huanguka
Hasa pale jeshi likikoma kuwa la wote, likawa la mmoja au kikundi fulani.
Mwanazuoni Edward Luttwak anaeleza kwamba mapinduzi hayafanywi na umati.
Yanafanywa na wale walio ndani ya dola, hasa wenye bunduki.
Ndiyo maana mtawala anayeogopa wananchi huanza kwa kuyafunga majeshi chini ya Uzao wake.
Acemoglu na Robinson wanaonyesha kwamba mataifa hayashindwi kwa laana, hali ya hewa au umaskini wa asili.
Yanashindwa kwa sababu madaraka na utajiri hukusanywa mikononi mwa wachache wenye misimamo na maamuzi duni.
Ukichanganya hayo mawili, unapata njia sahihi ya maangamizi.
Ukweli ambao hakuna atakayekuambia ukiwa Ikulu:
Askari hufa kwa bendera, si kwa jina la ukoo.
Cheo kinaweza kutolewa kwa amri, lakini heshima haitolewi.
Silaha unazomkabidhi mwanao leo ndizo zitakazoamua kama atakuwa mrithi au mfungwa
Wakosoaji wanauita huu "Mradi wa kizimuhoozi". Wao husema nchi inaendeshwa kama mali binafsi za familia. Wahusika wao hukanusha tu.
Taifa halitaporomoka kwa sababu hakuna rasilimali, bali kwa sababu rasilimali zimeelekezwa kulinda kiti, si watu.
Wataalamu na wajuvi wanasema "mataifa yaliyoshindwa" dola hushindwa pale linapokoma kuwalinda raia wake na kuanza kujilinda lenyewe.
Hapo katiba inakuwa karatasi, na bendera inakuwa kitambaa.
Wambura Askari hufa kwa ajili ya bendera maana tumeona Fikra zimeangukia tumboni.
Historia ya Tripoli, Baghdad na Cairo inawaonya kwamba jeshi lisilo la taifa halimlindi aliyelijenga siku ngumu ikifika.
TZ si mali ya ukoo. Ni mali ya kila mtoto atakayezaliwa kesho.
Taifa linaishi Falme huisha