Dp800
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 1,793
- 3,709
Pokeeni pongezi zangu za dhati kwanza kwa kuwaza na kuamua kutengeneza chama chenye mlengo na falsafa anuia za Hayati na Kipenzi chetu Dr. Magufuli. Hakika mmefanya jambo kubwa nala kutukuka sana.
Pamoja na pongezi zangu nyingi napenda kuwatahadharisha na kuwaasa kuwa makini sana kwa kila hatua mnayoiendea kwa maana dhamana na imani ya watanzania inakwenda kuwekwa juu yenu. Ni ombi langu kwenu kuwa na dhamiri ile ile ya upendo kwa Tanzania na watu wake huku mkijibidiisha kwa kila namna kuhakikisha Tanzania inapata viongozi wenye kiu na dhamira ya kweli kufikia maono makubwa ya kipenzi chetu Magufuli.
Ni vizuri kufahamu ya kuwa Tanzania ya sasa haina upungufu wa vyama vya siasa au sera nzuri za uendeshaji wa nchi. Hivyo ni budi kwenu kuyasoma na kuyapatia ufumbuzi yote ambayo ni maidhafu ya vyama vya siasa vilivyopo sasa ambavyo vimeshindwa kuonesha dira ya kweli ya Taifa letu kwa miaka 50 hadi 100 ijayo. Magufuli aliipenda Tanzania na kuchukizwa kabisa kwa maneno na vitendo na hali mbaya ya umaskini, ufisadi na dharau ya watawala/mabwenyenye waliojimilikisha nchi dhidi ya tabaka kubwa la watanzania wanyonge.
Ni ombi langu kwenu kutanguliza uzalendo na elimu ya kisiasa kwa watanzania wote wapate kufahamu dira, muelekeo na falsafa za chama. Katika hatua hizi za mwanzo ni muhimu sana kuhakikisha mnatengeneza misingi imara ya kitaasisi kwanza kwa kuhubiri na tena kuonesha kwa vitendo ili watanzania wayaamini hayo mnayapeleka kwao. Pasiwepo na hila midomoni mwenu tena Amani, Upendo,Haki na Mshikamano visipungue katika majukwaa yenu. Njoo na majibu ya namna ambavyo Tanzania itaweza kuendelea kiuchumi, kijamii na kisiasa. Ni muhimu sana kuzisema changamoto zote na kuueleza uma watanzania ni kwa njia gani tutafikia maendeleo ya kweli. Watafuteni wazee wazalendo wawapatie hekima zao, wapongezeni wanaostahili pongezi, wakemeeni wanastahili makaripio.
Karibuni kwenye ulingo wa siasa za Tanzania, karibuni kwenye figisu za CCM, karibuni kwenye hila za CHADEMA, karibuni kwenye kichaka cha wahuni na watakatishaji wa udhalimu.
Umoja ni nguvu, Umoja ni Ushindi, Umoja ni Maendeleo.