Hasa kwa wale wenye malengo ya kuja kuajiriwa kwasababu ukweli mchungu wa mfumo wetu wa elimu yetu inaandaa zaidi wahitimu kuajiriwa serikalini, wachache sana wamevunja mwiko huu kwa kutumia elimu zao kujiajiri kwa hiari
Ni kwanini form 6 ilitokea kuwa maarufu zaidi ?
Hapo zamani nchi ilikuwa na uchumi mdogo sana wa kuendesha vyuo na watu wachache sana walioelimika kufundisha vyuoni (wenye elimu walitumika zaidi mambo mengine ya serikali), Kuendesha chuo ni gharama kubwa sana kuanzia kulipa walimu mishahara ya milioni 3, umeme na majenereta, hostel za kisasa, vifaa vya taaluma, majengo ya gharama, kujaza vitabu maktaba, n.k. kukabiliana na hili serikali iliona mbadala ni shule za A Level kwasababu ni gharama rahisi zaidi kulipa mishahara ya walimu, hakuna haja ya umeme na majenereta, mabweni ya bei rahisi, majengo bei rahisi, n.k.
Vyuo vilikuwa ni vichache sana vinavyopokea wanafunzi wa Form 4 na ni wale wanaosomeshwa na serikali, ilikuwa ni jambo la kushangaza sana mwanafunzi wa form 4 kwenda chuoni, Ni takribani asilimia 1 tu walichaguliwa vyuoni, wote waliobaki walipelekwa form 6. kwa wanafunzi wengi sana walipitia njia hii, form 6 ilipata umaarufu mkubwa sana hadi leo hii kuna shule za gharama kubwa.
Zama zimebadilika, Mambo yamebadilika, wahi fasta chuoni !!
Siku hizi kuna vyuo vingi, Wanafunzi wanaweza kuanza kujifunza taaluma zao mapema, kwa bahati mbaya kuna lile zimwi la kuipa umaarufu mkubwa form 6 bado linaandama baadhi ya wanafunzi wengi sana, Unaweza kukuta mwanafunzi kwao wana uwezo wa kumsomesha chuoni lakini bado atangangania form 6, anaacha kwenda chuoni kusomea taaluma.
Chuoni unaenda kusomea taaluma form 6 unasomea masomo sio taaluma, Chuoni utasoma certificate mwaka moja, Diploma miaka miwili, Degree miaka mitatu hadi mitano, Wale wa form 6 taaluma yao wengi ni degree pekee.
Ni jambo la hekima zaidi kuanza mapema kusomea kazi, hayo utaweza kuyatimiza kwa kuanza kusoma chuoni mapema mara tu baada ya kumaliza form 4 kwasababu form 6 hakuna taaluma yoyote inayosomewa, form 6 ni kombi za masomo.
Kwa maandalizi ya mapema kwenye selection za form 4 vipe vyuo kipaumbele zaidi, ukikosa selection tuma maombi binafsi chuoni
Nenda form 6 kama
Ni kwamba ukienda chuo mapema una advantage kwasababu una sifa za kufanya kazi za certificate na diploma, Degree hawaruhusiwi kwasababu hawana vyeti husika vya taaluma, hivyo wewe una uwanja mpana zaidi na unaweza kuingia kazini kwa diploma baada ya muda kukawa na uhitaji wa watu wenye degree huwa wanaanzia kuangalia watu wa ndani hio ni advantage.
Halafu pia CV ya mtu aliewahi kuanza chuo ni nzito kwasababu inaonyesha kasomea taaluma miaka mingi zaidi, kafanya mazoezi ya kazi ya vitendo mengi zaidi, ana vyeti vingi zaidi vya taaluma, n.k. Unaweza kuta mhitimu mwenye cheti kimoja cha taaluma cha degree yupo anaiweza kazi zaidi lakini cv inamuangusha, kuna mameneja / mabosi wanavutiwa zaidi na cv iliyoshiba.
Uwanja mpana wa Ajira kwa mifano halisi
A.
inatokea mhitimu wa form 6 na diploma wote hawana ada / mkopo wa kwenda degree, Mwenye Diploma ana taaluma na kigezo cha kuajiriwa, Form 6 ndio imetoka hio !! hata kama mshahara utakuwa mdogo lakini Diploma at least ana uhakika wa kuajiriwa kwa taaluma, Ni kweli diploma analipwa kidogo kuzidi degree lakini si haba, Sehemu ambayo Degree analipwa milioni 1 diploma anaweza kulipwa laki 7, better for something than nothing.
B.
Kuna kazi mbili:
Pepsi - Diploma mshahara laki 7
Coca - Degree mshahara milioni 1
Form 6 mwenye degree pamoja na mwenzake form 4 mwenye Diploma na degree wanaenda Coca kuomba nafasi ya degree, kwa bahati mbaya wote wanaikosa kazi ya degree, Lakini yule form 4 mwenye Diploma na degree anaweza kuomba na kuipata kazi ya Pepso mshahara laki 7, form 6 mwenye Degree anarudi mtaani, akianza kumwambia mwenzake kwamba kazi aliyopata ina mshahara mdogo wakati yeye yupo kitaa tutamwelewa ?

- Kwenu hakuna pesa ya kukusomesha chuoni, Form 6 za serikali ada elf 70
- Una malengo ya kusomea degree yako nje ya nchi, vyuo vizuri vipo Marekani na Ulaya, ada na gharama za kuishi kwa mwaka ni takribani milioni 40+, vyuo kama havard milioni 100 kwa mwaka
- unataka kuwa mwalimu wa form 6, ni njia itayokupa uzoefu zaidi ikiwa utakuja kuwa mwalimu wa form 6.