Kwenu wanaJF: Saint Anne ninawashukuru mno

Kwenu wanaJF: Saint Anne ninawashukuru mno

Pole sana kipenzi nimefurahi kuona walau umefarijika. Tuendelee kumuombea mzee wetu apumzike kwa amani. [emoji120][emoji120] [emoji24][emoji24]
Ahsante sana mdogo angu; muendelee kupendana hivyohivyo. Big sis loves you two dearly. Baba yetu aendelee kupumzika kwa amani.
 
Baba Yetu Apumzike kwa Amani, Mungu ni Mwema kila wakati, tuko pamoja Dada.
 
🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾
Natumaini mnaendelea vizuri.

Nikiri msiba unauma jamani. Yaani maumivu niliyonayo nashindwa namna ya kuyaelezea[emoji24]. Nimempoteza mzazi wangu wakati ambao bado nilikuwa namuhitaji ,umri wangu bado ni mdogo kuweza kusimama bila baba[emoji24]

Tumempumzisha tayari mzee wetu na amani ya moyo inaniambia amepumzika salama. Ameondoka usiku wa kuamkia tar29/5/2021. Taarifa ilinipa mshtuko mkali,hadi sasa mapigo yangu ya moyo hayaendi sawa. Mwendo ameumaliza,nina imani kabisa kwamba nitakutana naye Mbinguni.

Baba alipoanza kuugua,nilipokuwa nikiingia katika maombi,kila nikiomba uponyaji,nafsi ilinisukuma sana kuomba naye toba na pumziko Zuri. Nilikosa raha sana lakini Roho wa Mungu alikuwa ananisihi sana kulipokea hilo. Amepumzika.

Baba yangu alikuwa baba mzuri na mtu wa watu,licha ya mapungufu madogo ambayo kila mtu ana yake. Mwezi mmoja kabla hajaugua,alifanya usafi sana nyumbani(Nikiri mzee alikuwa smart sana hasa katika kuweka sawa mazingira ya nyumbani), akaacha ametengeneza bustani nzuri, akatuaga akatuambia anaenda kuhangaikia usafi wa mashamba..akiondoka atakaa muda mrefu bila kurudi. Kumbe alikuwa anatuaga.

Aliwahi kusema kwamba mwanangu nitakuhudumia hadi pale utakapomaliza mambo yako ya shule.
Kweli, alilitimiza hilo, hadi alipokamilisha,akasema sasa mwanangu nimemaliza kazi yangu.

•Shukurani kwa Mungu kwa ajili ya baba:

Namshukuru Mungu kwa ajili yake, kwa neema aliyompa Miaka yote 64 akiwa duniani, Alikuwa mtu wa kujishughulisha mno hasa kutafuta chakula shambani kwa ajili ya familia. Sijui maisha yatakuwaje ila naamini Mungu atafanya njia. Inaniwia ngumu kuamini kama kweli mzee hayupo ila ni kweli ameondoka[emoji24]. Jambo hili ni zito sana kwangu.

Nipo Kwenye depression nzito, sielewi nitatoka vipi. Anayeweza kunisaidia namna ya kuondokana na hili wimbi la mawazo naomba anisaidie. Kiufupi akili yangu nahisi haipo sawa kabisa. Mziwanda wa baba Mimi[emoji24][emoji119]
Nyumbani ni pazito mno, usingizi hauji kabisa.

SHUKURANI ZANGU KWENU:
Kiukweli upendo mliouonyesha kwangu ndugu zangu ni upendo wa ajabu mno hadi nashangaa.
Natokwa na machozi ya huzuni lakini pia natokwa na machozi ya furaha kwa jinsi mlivyonionyesha upendo wa ajabu.

Namshukuru MUNGU sana kwa kunipa marafiki /ndugu wazuri sana namna hii ambao ni nyie. Kuna watu mmekuwa wazazi wangu, dada zangu, kaka zangu..yaani nawaona ni zaidi ya ndugu kwangu. Baba yangu hayupo ila ninaamini humu nitapata baba,nitapata wazazi,ninaamini mimi si yatima.

Baba yangu hayupo tena ila natiwa nguvu sana maana yupo Mungu ambaye ni baba yangu. Amesema yeye ni baba wa yatima[emoji1431].

•Mungu awabariki wote ambao kwa namna moja ama nyingine,mmekuwa karibu na mimi kwa hali zote kunitia nguvu,kuniombea,kunifariji,kuniliwaza na kutoa michango yenu ya mali(rambirambi) kwangu. Yaani sina namna nzuri ya kushukuru zaidi ya kusema Asante.

•Napeleka shukrani zangu kwa dada yangu Heaven Sent. Mungu akubariki sana dada yangu Heaven Sent. Umefanyika kuwa faraja kwangu. Nilipopata msiba,mtu kwa kwanza kumuambia alikuwa ni huyu dada.
Amani ya moyo ilinituma nimwambie yeye. Ni dada ambaye kwa kweli nikimuona namtukuza Mungu maana ananitia moyo mno. Sina namna nzuri ya kumuelezea vile ninavyomuona ila itoshe kusema ni dada ambaye Mungu amenipa.

•Mungu akubariki kaka Mshana Jr kwa moyo wako wa upendo na kujali.

•Mungu akubariki rafiki yangu Karma ..nimefurahi kukuona na ninaona sipo mwenyewe,,nina rafiki anayejali.

•Mungu awabariki wote walionitia moyo kwa namna mbalimbali. Kuna walionitafuta PM,kuna walionitafuta kwa namba yangu ya simu,Kuna walionitia moyo hapa jukwaani..Kila nikisoma comments zenu natiwa moyo mno kwa faraja ninayopata. Natamani nitaje mmojammoja ila naona nitakesha ninataja.

•Nakosa namna nzuri ya kuwashukuru,itoshe kusema Mungu na awabariki mno. Ninaleta shukrani zangu hizi kwenu..ninaomba mzipokee.

Mapenzi ya Mungu lazima yatimizwe,haijalishi yatatuumiza ama yatatufurahisha. Bado Mungu atabaki kuwa Mungu na ninamuamini mno,hata kama hajajibu kwa kadiri ya mapenzi yangu[emoji24][emoji120].


Pia soma: TANZIA - MwanaJF Saint Anne, amefiwa na baba yake mzazi leo
 
Mungu akawe mfariji wako my dear, pole sana, kilichobaki ni mimi na wewe kumuombea na kujiandaa na safari yetu ya mwisho, raha ya milele ummpe ee bwana,........
 
Mkuu nakupa pole tena. Hiki ni kipindi kigumu sana kwako, stay strong, katika maisha tumeumbiwa nyakati mbili; furaha na huzuni, lakini ndiyo moment zinazofanya maisha yakamake sense. .
Vilevile, jitahidi kumuenzi na kumkumbuka kwa mazuri yake. Hapo itakupa faraja sana. Na ukumbuke tu, tunawapoteza ndugu zetu na marafiki physically lakini tukiendelea kuzienzi kumbukumbu zetu, watu hao wataishi kwenye nafsi zetu daima.
Asante kwa faraja.
 
You are such a grateful human being, and you deserve all good things in this life and a good man/husband to be specific. Mungu atakusaidia na maisha yatasonga, jipe moyo.... Again my condolences Annie.

Mimi sijawahi kuishi na baba, Mungu amenipendelea sana kunipa mwenza ambaye naweza kumuita majina mengi mazuri. Nakuombea mdogo wangu.
 
Back
Top Bottom