Kwenu wanaume ambao wake zenu wanafanya kazi. Kipi bora mke wako kulea watoto na kutunza familia ama kazi?

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Wakuu huu mwaka 2025 hakuna jiwe litabaki juu ya jiwe yote yatabomolewa na kugeuzwa kwa wakati wake.

Leo mtuambie wanaume ambao wake zenu wanafanya kazi na majukumu yote ya nyumbani kuwaachiwa wadada wa kazi. JE NI KIPI BORA KATI YA KULEA FAMILIA NA KUFANYA KAZI?. Pengine sisi tulioa wamama wa nyumbani tunaonekana ni washamba na tumepitwa na wakati ebu leo tuambieni kwa kina.

Wengi tulio na miaka30+ tumelelewa na mama zetu hata mama akiwa mfanyakazi basi kipindi cha utoto wetu tulikuwa tunalelewa na bibi zetu,shangazi ama mama wadogo (wadogo zake mama).Hii ilileta maana ya kwamba
mtoto atakua katika malezi yaleyale ya kifamilia,kitamaduni na kijamii.

Miaka yote ile sikuwahi ona mtu baki ana lea mtoto wa mtu mwingine sikuwahi ona! Leo hii si ajabu kuona muha analea mtoto wa mchaga au mzaramo analea mtoto wa msukuma. Hapo lazima kuna vitu havitaenda sawa kwa mtoto hasa malezi.

Mbaya zaidi mtoto hadi anajitambua kashalelewa na wadada wa kazi wasiopungua saba ama kumi maana wapo wanakaa miezi2 akiona hapa ni wakali ama kuna kazi nyingi plus hakuna uhuru anaondoka wengine hujikaza walau mwaka1 au miaka2 hawa ni wachache mno kuwapata.

Na katika saba yote hii ya wa dada wa kazi makabila ni tofauti karibia wote hata tabia na malezi yao pia ni tofauti
Ushawahi jiuliza huyo mtoto anayelelewa na mikono ya wadada wa kazi tofauti tofauti atakua na tabia gani?

Zaidi ya yote hayo mtoto akifikisha miaka3-5 tiyari kaanza shule huko nako anaenda kukutana na watoto walio lelewa na ma house girl wengine ongeza na watoto wa masingo maza je unadhani huyu mtoto wako atakuwa na hali gani?

Mifano halisi tuwaangalie wanyama na ndege wawe wa kufugwa waliozoeana na watu ama wa mwituni.
Linapokuja swala la watoto wao hata uwe boss wao lazima uwe na tahadhari kabisa unaposhika watoto wake huwa hawana imani na kiumbe chochote kile hata awe mwenzeke bado hata muamini..

Nafuga kuku. Kuku akitotoa vifaranga maji na chakula utampa atafurahi na hata unaweza kumuitia akaja akala lakini ukigusa kifaranga chake tu dk hiyohiyo hajiulizi mara2 tiyari kashakularua.Kwa walio na watoto wadogo wakorofi watakuwa mashahidi wa hili mtoto akigusa kifaraga tu hata jicho linaweza tolewa maana hawana mchezo kuhusu watoto wao.

Wawindaji wanakuambia ombea yote lakini usikutane na simba,chui na nyati wenye watoto hawana msamaha kabisa.

Kwa mifano hii ya wanyama ni wazi kuwa wao wanathamini sana watoto wao kuliko kitu chochote kile huku kwetu kuna msemo usemao "NGOKO YA BHANA ITALYAGA IGINO" IKIWA NA MAANA YA KUWA "KUKU MWENYE WATOTO HALI WADUDU/FUNZA MWENYEWE BALI HUWAPA WATOTO WAKE!"

Mwanamke umebeba mimba kwa miezi9 kwa mateso yote na taabu zote ukababhatika kujifungua kwa kawaida ama op lakini baada ya kutua hayo mateso tyr akili yako ishawaza kazi.Kipi cha muhimu basi kati ya huyo mtoto wako na kazi? Yaani wewe unathamini kazi yako kuliko huyo mtoto halafu akili yako hiyhiyo inakutuma utafute mwanamke mwingine akulelee mwanao tena huyo binti hajawahi hata kuzaa hajui hata malezi.

Matokeo yake mtoto anaogeshwa saa9 ama 10 muda ambao wewe umekaribia kurudi. Muda wote huo mtoto kashinda kavalishwa pampers kajisaidia hadi yamekaukia na kwa vile hayawezi kutoka basi atashinda nayo hadi muda ukaribie ndo anaogeshwa na kuvalishwa nguo nzuri.

Kama unapinga fanya kushitukiza utakuja hapa nakukubaliana nami. wapo wachache sana wanao tunza vyema watoto wenu.Hayo yote anafanya maana anaona hata aliye mzaa hana uchungu nae ndio maana kamuacha na kwenda kazini mbaya zaidi unatoka kazini halafu unapitiliza kwenye vikoba ama vikundi. Mtoto wa watu unamlipa 50k na matusi juu halafu kabisa unategemea mtoto alelewe vizuri na mwanaume yupo kama hayupo tu ka bariki kwa baraka zote.

Bahati mbaya kuliko zote hela ya mwanamke ni yake binafsi yaani hata huyo house girl una mlipa wewe baba!!!!!?

Mimi nikiwa mmoja wa wanaume ambao tumeoa wamama wa nyumbani hakika tunaona faida ya mtoto kulelewa na mama yao. Kila kitu kuhusu familia unakiona kinaenda vyema na haki kabisa.

EBU SEMENI KIPI BORA WAKUU?
 
Sijasoma ulichoandika ila nadhani ni vizuri mke kufanya kazi
Hii itasaidia pale utakuwa haupo duniani ghafla(kifo) familia haitayumba sana au afanye biashara
Mama mfanyakazi ni furaha kwa watoto wenu(huwa wanarudi na vizawadi zawadi)
 
Hivi mkuu zawadi zina faida gani kama umeharibikiwa na watoto? Mbona swala la kazi limetukuzwa hivi karibuni ina maana wazee wetu sisi walikuwa hawafi? hapo nyumbani huwezi mfanyia biashara hala wanao uza wakawa wengine? huwezi fuga hata kuku wa mayai?
 
Yote unayosema yana maana na kama unaweza kuyafanya hayo sio mbaya so long as yatamfanya awe na life skills za kuweza kutunza watoto ukiwa haupo kwa Bahati mbaya
Kumbuka pia mke unakutana nae akiwa kasomeshwa na wazazi kwa mamilioni ya pesa huko marian na feza tena akiwa kazini crdb au muhimbili Sasa ukimwambia kaa nyumbani ulee watoto ni kumisuse resources
 
Ndio maana nikauliza kipi bora katiya kazi na mtoto. hata kama angekuwa anafanya kazi BOT swali hili ni kwa wanaume wote ambao wake zao wanafanya kazi
 
Wakuu huu mwaka 2025 hakuna jiwe litabaki juu ya jiwe yote yatabomolewa na kugeuzwa kwa wakati wake.

Leo mtuambie wanaume ambao wake zenu wanafanya kazi na majukumu yote ya nyumbani kuwaachiwa wadada wa kazi. JE NI KIPI BORA KATI YA KULEA FAMILIA NA KUFANYA KAZI?. Pengine sisi tulioa wamama wa nyumbani tunaonekana ni washamba na tumepitwa na wakati ebu leo tuambieni kwa kina.

Wengi tulio na miaka30+ tumelelewa na mama zetu hata mama akiwa mfanyakazi basi kipindi cha utoto wetu tulikuwa tunalelewa na bibi zetu,shangazi ama mama wadogo (wadogo zake mama).Hii ilileta maana ya kwamba
mtoto atakua katika malezi yaleyale ya kifamilia,kitamaduni na kijamii.

Miaka yote ile sikuwahi ona mtu baki ana lea mtoto wa mtu mwingine sikuwahi ona! Leo hii si ajabu kuona muha analea mtoto wa mchaga au mzaramo analea mtoto wa msukuma. Hapo lazima kuna vitu havitaenda sawa kwa mtoto hasa malezi.

Mbaya zaidi mtoto hadi anajitambua kashalelewa na wadada wa kazi wasiopungua saba ama kumi maana wapo wanakaa miezi2 akiona hapa ni wakali ama kuna kazi nyingi plus hakuna uhuru anaondoka wengine hujikaza walau mwaka1 au miaka2 hawa ni wachache mno kuwapata.

Na katika saba yote hii ya wa dada wa kazi makabila ni tofauti karibia wote hata tabia na malezi yao pia ni tofauti
Ushawahi jiuliza huyo mtoto anayelelewa na mikono ya wadada wa kazi tofauti tofauti atakua na tabia gani?

Zaidi ya yote hayo mtoto akifikisha miaka3-5 tiyari kaanza shule huko nako anaenda kukutana na watoto walio lelewa na ma house girl wengine ongeza na watoto wa masingo maza je unadhani huyu mtoto wako atakuwa na hali gani?

Mifano halisi tuwaangalie wanyama na ndege wawe wa kufugwa waliozoeana na watu ama wa mwituni.
Linapokuja swala la watoto wao hata uwe boss wao lazima uwe na tahadhari kabisa unaposhika watoto wake huwa hawana imani na kiumbe chochote kile hata awe mwenzeke bado hata muamini..

Nafuga kuku. Kuku akitotoa vifaranga maji na chakula utampa atafurahi na hata unaweza kumuitia akaja akala lakini ukigusa kifaranga chake tu dk hiyohiyo hajiulizi mara2 tiyari kashakularua.Kwa walio na watoto wadogo wakorofi watakuwa mashahidi wa hili mtoto akigusa kifaraga tu hata jicho linaweza tolewa maana hawana mchezo kuhusu watoto wao.

Wawindaji wanakuambia ombea yote lakini usikutane na simba,chui na nyati wenye watoto hawana msamaha kabisa.

Kwa mifano hii ya wanyama ni wazi kuwa wao wanathamini sana watoto wao kuliko kitu chochote kile huku kwetu kuna msemo usemao "NGOKO YA BHANA ITALYAGA IGINO" IKIWA NA MAANA YA KUWA "KUKU MWENYE WATOTO HALI WADUDU/FUNZA MWENYEWE BALI HUWAPA WATOTO WAKE!"

Mwanamke umebeba mimba kwa miezi9 kwa mateso yote na taabu zote ukababhatika kujifungua kwa kawaida ama op lakini baada ya kutua hayo mateso tyr akili yako ishawaza kazi.Kipi cha muhimu basi kati ya huyo mtoto wako na kazi? Yaani wewe unathamini kazi yako kuliko huyo mtoto halafu akili yako hiyhiyo inakutuma utafute mwanamke mwingine akulelee mwanao tena huyo binti hajawahi hata kuzaa hajui hata malezi.

Matokeo yake mtoto anaogeshwa saa9 ama 10 muda ambao wewe umekaribia kurudi. Muda wote huo mtoto kashinda kavalishwa pampers kajisaidia hadi yamekaukia na kwa vile hayawezi kutoka basi atashinda nayo hadi muda ukaribie ndo anaogeshwa na kuvalishwa nguo nzuri.

Kama unapinga fanya kushitukiza utakuja hapa nakukubaliana nami. wapo wachache sana wanao tunza vyema watoto wenu.Hayo yote anafanya maana anaona hata aliye mzaa hana uchungu nae ndio maana kamuacha na kwenda kazini mbaya zaidi unatoka kazini halafu unapitiliza kwenye vikoba ama vikundi. Mtoto wa watu unamlipa 50k na matusi juu halafu kabisa unategemea mtoto alelewe vizuri na mwanaume yupo kama hayupo tu ka bariki kwa baraka zote.

Bahati mbaya kuliko zote hela ya mwanamke ni yake binafsi yaani hata huyo house girl una mlipa wewe baba!!!!!?

Mimi nikiwa mmoja wa wanaume ambao tumeoa wamama wa nyumbani hakika tunaona faida ya mtoto kulelewa na mama yao. Kila kitu kuhusu familia unakiona kinaenda vyema na haki kabisa.

EBU SEMENI KIPI BORA WAKUU?
Endelea kutunza watoto wako wa kike kuwa Mama wa nyumbani. Usilazimishe wengine kufanya unavyotaka wewe.
 
umewahi kuwaza mkeo akikosa cha kuingiza kipato siku ukifa hiyo unayoita familia yako itaishije?
 
Kupata mwanamke wa kutulia nyumbani Kama goli kipa sikuizi ni ngumu.
Kama wewe umepata hongera mkuu [emoji106] itabidi ukifa tumuoe mkeo[emoji12](natania mkuu)
 
Sasa ndio nini?
Muda unaokuwa kazini ndio muda mtoto anakuwa Shule, ukirejea masaa machache nae anakuwa alirejea, au unadhani utoto ni level ya kumnyonyesha tu labda ungeshauri kufauatilia maendeleo na mwenendo wa mtoto pindi unaporejea nyumbani, ila kusema tusifanye kazi tushinde na remote kwa kochi, haha 😆 hapana sasa.
Teknolojia yote hii??, kama unahofu weka cameras fanya followup
 
Kwenye kazi yangu huwa nadeal na issue za mirathi sana. Na kama tunavyofahamu kwa asilimia kubwa wanaume hutangulia kuondoka kabla ya wanawake. Huwa ni huzuni sana mama anapokuwa ameachiwa watoto wadogo na hajawahi hata kufanya biashara ya kuuza maandazi.
Watoto kulelewa na mama wa nyumbani ni jambo jema sana, cha muhimu baba waachie wanao ma investment ambayo hata ukifa ghafla wataendelea kusoma bila shida
 
Back
Top Bottom