Mimi nitaishika kuikagua hadi siku nitakayokufa kwa presha. He is my husband na tunashare Kila kitu including hiyo simu yake. Sijapata sababu ya msingi ya kutokushika simu yake
Kama mtu ni mzinzi; presha utaipata tu hata usipokagua simu yake; unapeleka mbele tu siku zako za kupatwa na presha. Siku utakayoamka umeambukizwa magonjwa aliyoyatoa huko nje, au unaletewa watoto aliozaa nje basi presha itakuchukua tu. Madhara ya uzinzi yapo palepale ni suala la muda tu. Bora hata niikague, unaweza ukazuia madhara mengine yasitokee
Tuache kuzisingizia simu, hazina ubaya wowote; ni sisi ndiyo tunazitumia simu vibaya kufanya ufirauni wetu.
Ntamlinda kwa maombi na kwa "mbwinu" nyingine zozote nazoweza including kufuatilia nyendo zake.