Kwenu wataalamu, ni upi uzuri wa gari hii aina ya Probox?

Kwenu wataalamu, ni upi uzuri wa gari hii aina ya Probox?

Mkuu usisahau ikianza kuchoka kuileta huku tarime zinaitwa mchomoko Zina bebaa abiria hata kumi na tano kwenye siti ya mbele wanakaa wanna dereva anakalia tako mojaa....njia shirati au sirari au nyamongo
 
Mafuta ya tisin elfu unatoka tanga unafika chuga na kugeukat probox ni habari ingine ikikolea mwendo nikama tiara mwaka wa 4 huu nimebadili tairi na oil kila ikiisha tu,na ripea za kawaidatu
 
Gari zina kula shuruba Kigoma hizo wao wanazitumia kama daladala zina roho ya paka hizo gari kwa jinsi njia za Kg zilivyo wenyewe wanaziita mchomoko.
Ni Kweli Kigoma Kwenda Manyovu, Kasulu Kwenda Manyovu, Kasulu Kwenda Makele

Serengeti Kwenda Tarime, Utakuta Zinamwaga Moto Rough Road Kama Mgeni Ukiifuata Unaangusha Gari
 
Probox kalivyo kadogo kuosha unachanganya na vyombo!

Halafu kubadili tairi unafanya kunyanyua na mkono mmoja unapachika tairi, unapoendesha vile kibini ilivyo fupi ukiwa mrefu sana inabidi upinde shingo au utoe kichwa nje ili kisiguse kibin,

Kiufupi probox haina stress ingawa taili na rim zake ni nyembamba sana kama za spea taili!
NI GARI NZURI ACTUALLY
aaaaah.mbona unanivunja moyo mkuu,na u tall huu katanifaa kwel
 
Back
Top Bottom