Kwenu wataalamu, ni upi uzuri wa gari hii aina ya Probox?

Kwenu wataalamu, ni upi uzuri wa gari hii aina ya Probox?

Mkuu usisahau ikianza kuchoka kuileta huku tarime zinaitwa mchomoko Zina bebaa abiria hata kumi na tano kwenye siti ya mbele wanakaa wanna dereva anakalia tako mojaa....njia shirati au sirari au nyamongo
[emoji23][emoji23]
Kwamba mchomoko,founder wa hizi ngoma aliwaza sana!
 
Yaani hapo kwenye Probox mjampani aliwaza two in one. Aliunganisha mawazo ya gari mbili na kuziweka kwenye gari moja. Alichukua Kirikuu+IST akapata Probox.
Absolutely..
Nakubali sana,huyu jamaa alichekecha sana.
 
Wakuu habarini,hongereni na poleni kwa harakati + kuelekea kuimalizia wiki.

Wakuu gari hii nimeisikia ni nzuri kwa harakati za hapa na pale haswa kwenye miradi midogo midogo(ufugaji + kilimo) pamoja na kubebea mahitaji ya home.

Hivyo sasa wakuu naombeni kupata ufafanuzi kupitia kwenu mkiwa kama wataalamu katika vipengele vifuatavyo:

1. Uimara wake rough road
2. Upatikanaji wa vipuri
3. Kuhimili safari ndefu
4. Comfortability kwenye lami na rough roads
5. Service

NAWASILISHA.
View attachment 1702224
Nilikuwa naipenda sana hiyo gari kipindi sina pesa, na mara ya kwanza kuiona ilikuwa kipindi nakaa Nairobi, nadhani Tz zilikuwa bado kufika.
 
Mafuta ya tisin elfu unatoka tanga unafika chuga na kugeukat probox ni habari ingine ikikolea mwendo nikama tiara mwaka wa 4 huu nimebadili tairi na oil kila ikiisha tu,na ripea za kawaidatu
Ahsante Chief
Nimekupata.
 
Ni Kweli Kigoma Kwenda Manyovu, Kasulu Kwenda Manyovu, Kasulu Kwenda Makele

Serengeti Kwenda Tarime, Utakuta Zinamwaga Moto Rough Road Kama Mgeni Ukiifuata Unaangusha Gari
[emoji23][emoji23]
 
Probox ndio gari yangu ya kwanza,nilitumia kwa miaka miwili nikaiuza bila kutarajia kutokana na ushawishi wa niliyemuuzia,mpaka leo naitamani gari ile.Na nitainunua tena.
Sawa Boss..
Kwa nukta yako nahisi hii gari itakuwa makini sana.
 
Kama ni mrefu sana kata kibini ongezea bodi juu kidogo ili kichwa kitoshe au kubana bajeti unaweza toboa tundu kichwa kitoke inje halafu unavalia na helmenti wakati unaporndesha!
[emoji16][emoji23][emoji23]
 
Hivi nyuma ina viti vya kukunja!,mi nilidhani ipo wazi tu
Kanza hongera kwa kuwaza kununua Probox.kama nin mtu wa miradi hutajuta kwasababu nyuma ina nafasi ya kutosha kama pickup pindi unapokunja viti.Ina ulaji mzuri wa mafuta kama IST kwani hazipishani ukubwa wa engine.Ikiwa na mzigo utaipenda inavyokamata barabara.Spea zipo za kutosha na kwa bei nafuu.kifupi Ni gari nzuri kwa mtafutaji
 
Back
Top Bottom