Kwenu wazazi mnaosomesha Watoto, Msisitize watoto wasomee Udaktari, Sheria, Engineer ama Uhasibu. Soko la ajira ni gumu ila huku kuna Nafuu

Ushauri kuntu huu....ukisoma kitu una passion nacho masomo yanakua marahisi, hata uki graduate unakua na confidence ya ku practice ulichosomea...sio kuchagua course ngumu,kila siku una sup unagraduate kwa mbinde, hata confidence inashuka, na wale graduates wanaoajiriwa huko makazini halafu wako incompetent ukiangalia kwa makini sababu ni hii ya kulazimisha kusoma kitu hauna interest nacho....

Mimi ningependa kuona mwanafunzi kuanzia mwaka wa kwanza anapata sehemu ya kujishikiza hata kwa masaa mawili kwenye shirika ambalo linatoa ujuzi unaoendana na fani anayosomea, hii inasaidia kumfanya mwanafunzi ajue what to expect mtaani, opportunities,akazanie nini kwenye course yake ambacho kinaendana na demand mtaani, inakua kama feedback system, experience kazini ina consolidate anachosomea mwanafunzi, na akitoka darasani analeta new ideas kazini...akitoka hapo ana Experience + Knowledge + Confidence...graduate anakua ameiva...
 
unapotosha watu mkuu, vitu kama hivi kama huhusiki na kada ni bora unyamaze
Yupo sahihi Computer Engineering ni ina-deal na Electronics zaidi unacheza sana na ma-hardware kufumuafumua mavifaa ya Computer na kufanya marekebisho, HESABU za kufa mtu km hupendi HESABU achana nayo soma tu CS utengeneze ChatGPT ya kwako basi
 
Hii wapo wanaofanya Ila ni wale wenye CONNECTION TU
 
Hao computer science hawawezi kuwa hata fundi TV ama simu mtaani ndio uwalinganishe na computer engineering ? upo serious wewe ?
Una point Ila uwasilishaji wako tu ndio una tatizo

Computer Engineering na Computer Science vinategemeana Ila Computer Engineering ni zaidi ya Computer Science kwenye masuala ya Electronics & Hardware's tu Ila vingine vyote ni sawa ingawa soko la ajira linawahitaji sana wale waliosomea Computer Science
 
Computer science ndio yenye ajira nyingi na ndio nzuri zaidi
Zote zina Ajira Computer Science & Computer Engineering utofauti ni mmoja ata-deal na hardware's (CE) na mwingine ata-deal na softwares (CS),

Ingawa aliesoma Computer Engineering anaweza kufanya kazi za mtu aliesomea Computer science Ila aliesoma Computer Science hawezi kufanya baadhi ya kazi za mtu aliesoma Computer Engineering

Kwa hio ukiangalia hapo mwenyewe utaona mwenye wigo mpana ni yule aliesomea Computer Engineering
 

Nliisha acha kuwashauri wath wasome nini
Baada ya kugundua mtaji ni watu sio taaluma

Soma chochote hakikisha una watu basi
 
Computer engineering ina soko kubwa zaidi, ndio kozi baba kwenye mambo ya computer ikifuatiwa na hizo zingine.

Compuuterengineer anaweza kuwa fundi mitambo pia kwenye hardware, ama hata fundi wa simu na laptops upande wa software na hardware.
Wewe unaongea kitu usichokijua
 
Sheria hakuna kitu
 
Kwanini kuzamia kwenye statistics na computer science/IT?


Sent using Jamii Forums mobile app
Computer Science ni field pana ajabu!

Msingi wa mafanikio ya hii field ni Statistics maana the now and future is all about data. Data bila statistics haziendi.

Ukiniuliza kuhusu statistics, nitakwambia unapaswa kujua mean, mode and median. Mengine yote yanaanzia hapa (hasa kwenye mean).

Well, anayesoma Computer Science leo hii bila kufikiria habari za data modeling aka machine learning ambayo msingi wake ni statistics hana budi kutafakari upya mtazamo wake.

Hivyo basi, statistics adds an edge to computer Science candidate. Bila in-depth statistics - yaani candidate asome HTML,CSS na JavaScript - hela iko ila sio kihiivyo.

Chaguo ni lako mkuu!
 
In short computer science ni tawi la hesabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…