Anita Makirita
JF-Expert Member
- Jul 16, 2021
- 1,341
- 2,121
Ushauri kuntu huu....ukisoma kitu una passion nacho masomo yanakua marahisi, hata uki graduate unakua na confidence ya ku practice ulichosomea...sio kuchagua course ngumu,kila siku una sup unagraduate kwa mbinde, hata confidence inashuka, na wale graduates wanaoajiriwa huko makazini halafu wako incompetent ukiangalia kwa makini sababu ni hii ya kulazimisha kusoma kitu hauna interest nacho....Makumbusho na Kariakoo zimejaza wauza simu wengi wenye MD zao na ajira hawajapata sijui nani anapata audacity ya kumshawishi mtu asome kitu fulani sababu kuna ajira ya uhakika. Msimamo wangu kwa wanaosoma ni huu:
1. Soma kitu unachoweza. Usisome kitu kigumu kisa umaarufu au kuonekana gangwe, utatumia gharama nyingi, muda mwingi na uwe average tu kwenye industry. Utakuwa yule daktari anafanya kazi hospitali ya serikali tu hana vituo vya pembeni sababu ni very average kwenye competitive market.
2. Soma unachopenda na uwe na vision nacho. Ukipenda kitu unakifanya kwa ufanisi zaidi, unafaulu kirahisi na unajua potentials zake, future yake, vitu visivyoonekana kwa wengine. Passion ni muhimu kuliko kulazimisha. Usifuate ndoto za wazazi. Mzazi unakuta alitamani awe Engineer masomo yakampiga sasa analazimisha uwe Engineer wakati uwezo huna, mzazi anataka cheo cha kutamkika akatambe kwenye jumuiya wakati wewe ni matter of life. Unless huyo mzazi ni 'muelewa' wa situation ilivyo na atachangia kukua kwako, kama yuko sekta fulani akikushawishi basi anamaanisha.
3. Soma kitu ukijua kuna kuajiriwa au kutoajiriwa. Ukisoma kwa kutegemea kuajiriwa ndio yaleyale ya Petroleum Engineering mtu ana ufaulu wa juu sana ila ana njaa mfukoni kisa hakuna ajira. Mtu aliyesoma Accounting ana uwezo mkubwa sana kujiajiri kuliko aliyesoma Pharmacy. Nina jamaa yangu alisoma Accounting akaiva akaenda kwa ndugu yake nani uko kufundishwa Auditing na vitu vya hivyo, anapiga Audit ya mtaani na anaenda ofisi kwa ndugu yake yuko certified kuchukua mhuri na saini. Hela nyingi anapata (mfano una kampuni uchwara zile mnafungua kwa kiherehere haijauza nusu mwaka unataka kufile tax ile kitendo cha kuthibitisha hujauza kitu unamlipa sijui 50,000 sijui 30,000), yeye alikosa kazi akaamua aongeze skills chache kwenye fani yake. Sasa Pharmacist ukikosa kazi utauza dawa za kienyeji kama application ya ulichosoma?
Mtaji wa kufungua Pharmacy ni mkubwa, huyo jamaa alianzia ghetto kwake na meza, kiti na laptop na vitabu vyao.
4. Usisome kitu kimoja kama unatafuta ufalme wa mbinguni. Soma alafu kuwa na skill nyingine kama graphics, photography, drawing, beautician kama ni mtoto wa kike, n.k. Nina mate wangu alisoma diploma ya Engineering ila ni DJ na analipwa vizuri kwenye u-DJ kuliko kwenye kulishwa vumbi uko kwa mafundi mchundo, na anafanya kazi sehemu nyingi. Side hustle inakusaidia kupata hela wakati umekosa ajira mwanzoni na inakusaidia ukiwa kwenye ajira vilevile. Hata ukipata hela unajua business gani ufanye, kama ni binti anajua ususi akienda kwenye ajira akapata hela anajua mtaji kiasi gani ananunua nini na nini anaanzisha kiofisi anaweka mtu.
N.B: Wakati namaliza chuo Magufuli alishafariki. Ushauri wangu 'ni wa kisasa' unaendana na mazingira ya sasa.
Mimi ningependa kuona mwanafunzi kuanzia mwaka wa kwanza anapata sehemu ya kujishikiza hata kwa masaa mawili kwenye shirika ambalo linatoa ujuzi unaoendana na fani anayosomea, hii inasaidia kumfanya mwanafunzi ajue what to expect mtaani, opportunities,akazanie nini kwenye course yake ambacho kinaendana na demand mtaani, inakua kama feedback system, experience kazini ina consolidate anachosomea mwanafunzi, na akitoka darasani analeta new ideas kazini...akitoka hapo ana Experience + Knowledge + Confidence...graduate anakua ameiva...