Kwenye biashara usiogope majina makubwa yaliyokutangulia; Hill water, mabasi ya Tilisho ni somo kubwa la kuingia sokoni ukiwa mpya

Kwenye biashara usiogope majina makubwa yaliyokutangulia; Hill water, mabasi ya Tilisho ni somo kubwa la kuingia sokoni ukiwa mpya

Kilicho muumiza mengi alijisahau wenzake wakatumia mwanya huo lakini maji ya Kilimanjaro mpaka sasa bado ni bora zaidi pamoja na maji ya afya maji mengi yana chumvi akijipanga akashusha bei mbona bado jina analo tu mtu akikaa sokoni kwa muda mrefu kumshusha iko kazi labda afanye uzembe
Hujawahi kunywa maji ya Kilimanjaro yanayouzwa Nyanda za Juu Kusini,utatamani ni kheri ungepewa maji yaliyochotwa mtoni.
 
Ila chupa za hili water zinavutia sana kwenye macho. Kamfanya mmiliki wa maji ya Uhai kashusha bei hakika biashara kuna kupanda na kushuka.

Sasa ni wakati wa Hill water
Zina muonekano wa kike zaidi yaani chupa za vipodozi.
 
Juzi nimetoa 1000Tsh dukani wanipe maji
Nikashangaa napewa kilimanjaro 1 litre na chenji 300😂

Kutoka buku 2 hadi 700!!
Mhh!! Haya maji si ziku zote bei ya 1.5Lt ni elf1, sio ajabu 1lt kuwa 700. Ukiwa bar na hotel ndio inabadilika

Huku kaskazini imejaa 0.5lt na 1.5 Lt
1lt nadra sana. Binafsi skumbuki kuiona
 
TILISHO na yeye hakuogopa.. kaja sokoni mpya kwa mbinu ya wahudumu mabinti wapenda social media.. mwisho wa siku kaiteka njia bus zake kila siku zinajaa
Nadhani ni mtu na mtu. Mf mimi bila BM/ kidia one, sisafiri. Kama ni ulazima sanaaaa nazama Extra Luxury..
 
Hujawahi kunywa maji ya Kilimanjaro yanayouzwa Nyanda za Juu Kusini,utatamani ni kheri ungepewa maji yaliyochotwa mtoni.
Huyo jamaa nahisi hajawahi kuonja maji ya Kilimanjaro,ndio maji yalikuwa mabaya sokoni,chumvi nyingi. Kuna muda ilifika nilikuwa nikiagiza maji naomba yeyote isipokuwa tu Kilimanjaro.
 
Huyo jamaa nahisi hajawahi kuonja maji ya Kilimanjaro,ndio maji yalikuwa mabaya sokoni,chumvi nyingi. Kuna muda ilifika nilikuwa nikiagiza maji naomba yeyote isipokuwa tu Kilimanjaro.
Mkoa gani? Nadhani haya maji yana mkoa na mkoa. Ya Arusha mbona mazuri tu, maana hata dogo alikuja akayakuta. Alistaajabu kwamba hayafanani na yq Dar
 
Mkoa gani? Nadhani haya maji yana mkoa na mkoa. Ya Arusha mbona mazuri tu, maana hata dogo alikuja akayakuta. Alistaajabu kwamba hayafanani na yq Dar
Nimekaa Dar na Mwanza,kama huyo dogo amekunywa hivi karibuni inawezekana wamebadili,sababu wiki mbili zilizopita na mimi nilikuwa Sehemu moja hawauzi maji zaidi ya Kilimanjaro,nilivyokunywa ile chumvi sikuisikia kabisa,nilibaki najiuliza.
 
Sisi wazee wa Dew Drop kutoka Mjini Swax huu Uzi hautuhusu.
hiyo brand ilishauzwa kitambo kwa sasa inatengenezwa dar pale buguruni , kimsingi yalikuwa maji ya kueleweka sana na bardiiii kama ya chem chem ila kwa kutengenezewa dar tayari wameshalikoroga, maana hata kilimanjaro yenye chumvi ni yale ya dar wanayopaki pale mikocheni pamoja na Dasani
 
Back
Top Bottom