kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Hata tufanyeje lazima tufanane na wazungu kwenye siasa za vyama vingi. Aina hii ya siasa ililetwa kwetu na wazungu kwakuwa wana kazi nayo, lakini vyama na wanasiasa waliopigania uhuru waliikubali aina hii ya siasa kwa shingo upande kwa kulazimishwa.
Wakati wazungu wanaileta kwetu aina hii ya demokrasia walijuwa kuwa watawala wetu hawataikubali aina hii ya siasa, hivyo kwa vyovyote vile mabeberu watapata kundi la kuunga mkono ili wakati wakigombana wenyewe kwa wenyewe wao wnapata namna ya kutia mkono kwenye bakuli la rasilimali zetu.
Ndiyo maana nchi zote za Kiafrika zenye utajiri mwingi wa mafuta, madini, mbao hazifaidi mali zao hizo badala yake wanaofaidi ni wazungu kwa kupitia kundi linalokandamizwa na watawala. Na hakuna mtawala wala serikali inayoweza kuzuia hili lisitokee. Mfano, Uganda kuko shwari sasa hivi lakini subirini waanze kuyachimba mafuta yao muone timbwilitimbwili lao.
Dawa pekee ya kuzuia hili ni kuukumbatia utanzania wetu, utu wetu na tunu zetu ili zitusaidie wote kumuona, kumchukia na kupambana na adui wa nje tu na vibaraka wao. Na njia pekee ni kutengezena katiba na tume ya uchaguzi imara inayokubalika na wengi, kuendesha uchaguzi wa haki na wazi, kujali maisha na uhai ya kila mtanzania na kuunda taasisi imara za kuilinda katiba yetu. Hii itasaidia kupunguza mianya wanayotumia mabeberu kujipenyeza kwenye mataifa yenye rasilimali nyingi.
Hali ilivyo leo sio nzuri, mabeberu hawapati shida kupata watu wa kuwatumia kuingia Tanzania.
Mwafaka wa kitaifa ni kipaumbele kuliko ziara za mataifa jirani.