Kwenye hili wakristo mna la kujifunza

Kwenye hili wakristo mna la kujifunza

Kuna jamaa mslamu kaoa ndoa moja simple sana yani, no mc, no mbwembwe!

Wakati wa sa1 kasoro ile kufuturu jamaa kaoa hapohapo, watu wametulia kwenye mkeka na vikombe vya uji wanajitafunia zao maandazi, shehe aliefungisha ndoa kapigwa buku5 tuu ya maji.

Yani ndoa mpaka inakamilika haijazidi hata elfu50.

Hawa jamaa kwa upande huu nawakubali sana.

Wakristo sasa utakuta ndoa inagharimu mamilioni.
Tatizo nini ndugu.

Elewa kitu kimoja kinaitwa furaha, kila mtu anatamani kufanya jambo linalompa furaha.
 
Mkuu mm nilijuaga talaka za waislam zina process maybe shekhe atie mhuri au Hata mashahidi wapitishe hilo.

Ila nikaja kuona talaka tatu za jirani yangu hapa mpemba hv ety n kwenye vipande vya karatasi vimechanwa vipo vitatu, utadhani n vile vikaratasi unaandika namba ili kumuandikia namba wakala atume pesa 😂
Talaka ya kiislamu ni nyepesi sana.
 
Tafuta hela, hali ya uchumi ya wanywa uji na muoaji ikoje??

Haya mambo yanaendana na uchumi mkuu, sio kwamba wakristo wote wanaoa kwa masherehe makubwa wapo wanaooa kwa kidofo walichonacho.
 
Kwamba Rais wa China, Xi Jinping n mkristo?
kwa kawaida maharusi wa kikristo huvaa suti wanapofunga ndoa ila si sheria, ni fasheni tu ndio maana hata waislam wakitoka kwenye makanzu yao huko walikofungiwa ndoa yao na sheikh wao huenda ukumbuni wakiwa wamevaa suti kama wakristo na bi arusi akiwa amevaa shela. Hujawahi kuona harusi ya kiislam ukumbini jinsi walivyovaa? Kule hutaona mavazi ya kiislam wanavalia ki magharibi tu! Labda wawe choka mbaya ndio utaona vivazi vya kiislam ukumbini
 
Tatizo ni pesa tu,hakuna cha gharama ndogo,assume mo dewji anaweza funga ndoa na afanye sherehe inayogharimu budget ya elfu 50?
 
Kituko ni pale mtu anayeishi chini ya dola moja kutaka kufunga ndoa ya mamilioni ya pesa! Anataka kufanya harusi kwa kutegemea mifuko ya watu, huo ni ujinga kupanga bajeti ya harusi kwa kutegemea michango ya watu. Kumbe unaweza kufunga ndoa tu bila kusumbua watu wakuchangie
 
Karamu ya harusi ni utaratibu wa kijamii sio kidini ndugu mleta mada...

Hivyo watu kuvalia mavazi mazuri mazuri, kuweka karamu ya gharama kubwa haina uhusiano wowote na Ukristo bali ni urithi wa taratibu za kijamii ambao umeboreshwa...

Kwenye dini kuna ndoa, kwenye jamii kuna harusi...
 
Talaka ya kiislamu ni nyepesi sana.
ukristuni hakuna talaka, mambo yakikaza na hayarekebishiki unaoneshwa njia ya kwenda mahakamani kutengua ndoa ili kila mmoja awe huru aendelee na maisha yake bila kubughudhiwa na mwenzake endapo atapata mwenza mpya. Kule hakuna kuachana kirahisi. Ila siku hizi wanaachana kimyakimya bila kwenda mahakamani kutengua ndoa. Kimbembe huwa ni mali, kama hakuna mali wanaachana kimyakimya
 
Poa tu, kama mtu ataamua kufanya sherehe kubwa ya harusi yake basi ajigharamie yeye na wazazi wake. Ya nini kuombaomba michango? Watu ni wa kualikwa na kukaribishwa kula tu, ndio ilivyokuwa hivyo miaka ya nyuma. Na si vibaya mtu akafunga ndoa bila kufanya harusi yenye mbwembwe nyingi na anasa kubwa. Mbona bomani wanaenda watu wanne tu tena wamevaa kawaida wanafungiwa ndoa na afisa mwenye mamlaka ya kusajili ndoa kisha wanarudi nyumbani kama mke na mume? Mambo mengine ni fasheni tu
 
ukristuni hakuna talaka, mambo yakikaza na hayarekebishiki unaoneshwa njia ya kwenda mahakamani kutengua ndoa ili kila mmoja awe huru aendelee na maisha yake bila kubughudhiwa na mwenzake endapo atapata mwenza mpya. Kule hakuna kuachana kirahisi. Ila siku hizi wanaachana kimyakimya bila kwenda mahakamani kutengua ndoa. Kimbembe huwa ni mali, kama hakuna mali wanaachana kimyakimya
Ndoa zenye mali huwa mtihani hususani kama mume ndio hustler na mke hajachangia chochote ila kadhamiria kumkomoa mumewe pasipo kujali welfare ya watoto..
 
Back
Top Bottom